Kwa nini unasema kuna ushindani? Wakati timu zote za EPL zina viwango vibovu? Sasa hiyo Leicester city yenu inayovimbia hizo timu mnazoziita kubwa inaweza kujilinganisha na A. Madrid?
Kitu kingine unaposema La liga ni timu mbili tu zinachukua ubingwa kwani EPL kabla ya man city haijanunuliwa na billionea si timu mbili tu Man U na Chelsea ndo zilikuwa zikipokezana ubingwa? Kila ligi lazima iwe na wababe nchi zote. Ujerumani kuna B. Munic na B.Dortmund, Ureno ni Portal na Benifica, England ni Man U na Chelsea sema tu sasa hivi pesa zimevuruga hadi man city imeingilia kati. Asernal ni average timu ni level za Sevilla au Valencia. Liverpool inabebwa na historia tu lakini hamna kitu ishajifia kama Ac Milan.
Namalizia kwa kusema Bayern Munic, Real Madrid na Barcelona hizi ni level nyingine, miaka iliyopita ningeweka hata Man u. Hizi ni timu ambazo ni aggressive katika mafanikio na zinasajiri world class players hivyo usishangae kunyanyasa timu za kwenye ligi yao tofauti kwa sasa ligi ya EPL haina hicho kitu. Wachezaji wa timu za EPL kwa sasa ni average players tofauti na zamani ndo maana zinashikana mashati na wewe unakuja kubwabwaja hapa eti EPL ni ngumu. Let say mechi ya jana Liverpool vs Asernal zmetoka sare. Hiv ww unafikiri kwa mchezo wao mojawapo ingekutana na Barca si ingekula goli kumi😎