Figisu Hatimae kufukuzwa kazi

Uko sahihi mkuu.na mimi ilinitokea nikawa naona giza ila saiv niko zangu NGO nzuri tu life linaenda.
 
Angekuwa mwingine angewaza kukimbia nazo kumbe kuna maisha mazuri unajiharibia.
Hakika ndugu......

Ukiudhibiti moyo wa tamaa utajiepusha na mengi na utafaidi vingi Sana.......

Kuna ndugu yangu alikuwa anabeba zege kwenye kampuni ya ujenzi ya kichina.......

Kwenye ile kampuni kuna mchina alikuwa na wazo la kufungua kampuni yake ya kuuza piki piki.... kipindi hiko piki piki so nyingi........

Nyota ikamuangukia ndugu yangu..... uaminifu, upole na uchapakazi vikamuongezea sifa.......

Yule mchina alifungua kampuni kubwa ya kuuza piki piki na spare zake maeneo ya Arusha kwa jina la yule ndugu kwenye kila document.....akiwa kama mmiliki mwenza......

Biashara ilivyo kuwa inakwenda vizuri mchina akaamua kurudi China kazi yake ikawa kutuma mzigo na anakuja kwa mwaka mara mbili tu..... imagine maisha yanavyo change.........

Sasa hivi jamaa ni miongoni mwa watu wanaojiweza Arusha........
 
Kampuni ni ultravetis?
 
Na ukitaka kumuwin mchina akupe maisha kuwa muaminifu aisee utaona hii dunia hakunaga shida, wakati wenzio wanalalamika pesa hakuna unawasapoti kuongea ila unachekea pembeni..!!
 
Kujari, hajari, sijuhi, akatukabizi, alfu, ko, mbaka..... hata kama ni mimi ningekufukuza tu kazi. Kuandika huwezi halafu unataka kuleta janjajanja kwenye biashara ya boss... kosa ulilotaka kufanya sio wizi bali ni UHUJUMU WA BIASHARA. Kosa la uhujumu ni kubwa kuliko wizi. Boss ana akili nyingi sana kuondoa kirusi kama wewe kwenye biashara yake.
 
Pole sana. Watu wa sales huwa wanapigwa sana fitina. Ukikuta kampuni ina ndugu na watoto wa boss hali huwa mbaya zaidi. Mimi nishawahi kuwa mtu wa sales nikawa napigwa fitina na ndugu wa boss ikabidi siku moja boss aniite na kunisomea tuhuma zangu zote kama alivyopelekewa.. nikamwambia boss mimi siwezi kujitetea lolote ila bank statement ya kampuni ndo initetee. Kiukweli mauzo kupitia mimi yalikuwa makubwa kwahiyo boss akaniambia wewe endelea na kazi. Ila haikupita miezi mingi niliacha kazi mwenyewe.
 
haya
 


Kazini kuna maadui sana, pole
 
Kazi ya sales ni kazi ya kitumwa sana iliyojaa lawama, matusi na masimango huku mshahara ukiwa kiduchu.........cha ajabu wewe ndio unaendesha kampuni kwa juhudi zako huko mtaani.........

Mimi niliacha na nikaapa sitofanya tena kazi ya kuajiriwa......nikaamua kuwa mtu wa kati kwa kuwa nayajua machimbo mengi ya bidhaa kwa bei nafuu na nina wateja wa mikoani.....mtaji wangu ni uaminifu tu
 
Ni muda Sasa wa kuweka focus kwenye mambo yako binafsi uliokuwa unafanya kujipatia kipato nje na ajira uliokuwa nayo.
 
Hajari=Hajali,,kutukabizi=kutukabidhi,,,Sijuhi=Sijui nk nk,,,Songa mbele,,pole kwa changamoto iliyojitokeza katika mlolongo mzima wa Maisha yako
 
Kiswahili sahihi ni kipi? Mbaka au Mpaka? Maana watu wa mbeya kiujumla mnanichanganya sana.
 
Kweli kabisa sales mate wangu wengine walipelekwa polisi.
 
Kuwa replaced is not a reason. Kwa namna hii muajili anaweza akamleta yeyote wakati wowote kum-replace mtu. Lazima barua iseme makosa yako
Hiyo sababu alio isema kamwe muajiri hawezi akaiandika maana anajua jamaa akienda CMA muajiri ataahindwa kuthibitisha hilo kosa then itamgarimu.
Hapo saaana watamuandikia Unhonest/Dishonest.
Kumbuka mahakama/tume ya usiluhishi hua inataka muajiri athibitishe kosa la kumfukuza kazi mhusika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ