Niliwahi kufukuzwa kwenye kampuni moja nikiwa kama salesman baada ya miaka saba ya kuipigania kampuni katika hali na mali nikikabidhiwa piki piki tu kufanya shughuli zangu.......
Nilikuwa nafanya mauzo makubwa makubwa kwa faida ya kampuni kwa malipo kiduchu Sana........
Mwisho wa siku nikapewa barua ya kufukuzwa kazi kama kibaka..........
Iliniuma sana lakini nikapiga moyo konde........
Wateja wakawa bado wananitafuta kutoa oda zao.....nikawaa nakwambia ukweli......kutokana na uaminifu wangu na uchapakazi baadhi ya wateja walisikitika sana na baadhi Yao wakanipa kazi ya kuwakusanyia mizigo Yao wakija kufunga mzigo huku mjini.......wananiwekea pesa kwenye akaunti yangu na mimi nazunguka kuwatafutia bidhaa na kuwapelekea kwa transporter wao......
Nashukuru Mungu mpaka leo naishi vizuri bila kero wala bughudha na muda mwingi niko free na napata pesa mara kumi ya ule mshahara wangu nikiwa nimeajiriwa.........
Rai yangu ni kwamba kila changamoto ni mlango wa mafanikio, kaza moyo endelea na harakati za maisha, huzuni na majuto vinakufanya usione mlango uliowazi mbele yako.......