Donnie Charlie
JF-Expert Member
- Sep 16, 2009
- 16,908
- 19,123
Fisi huyo aliyeua mtoto wa mwaka mmoja na nusu baada ya kuvamia nyumba katika Kijiji cha Kangeme wilayani Kaliua alijeruhi pia watu watatu ambao inaelezwa wanaendelea vizuri.
Diwani wa kata ya Zugimlole, Ramadhan Balikeka amesema kuwa wananchi waligawana nyama na haelewi walienda kufanya nini.
"Watu baada ya fisi kuuawa walidai watamshughulikia na kuchukua nyama huenda walienda kuila,"amesema.
Balikeka amesema kuwa tukio la fisi huyo na namna alivyokuwa mahiri kukwepa risasi, limehusishwa na imani za kishirikina, wananchi wakidai ni fisi wa aina yake.
Katika taarifa yake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Safia Jongo alisema kuwa fisi huyo alivamia kwenye nyumba katika kijiji hicho na kuua mtoto wa mwaka mmoja na nusu na kujeruhi watu watatu.
Pia aliongeza kuwa polisi na askari wanyamapori walimuua baada ya kutumia risasi arobaini na tisa.
Kwa mujibu wa Diwani Balikeka, tukio hilo la fisi ni la kwanza mwaka huu katika kata yake.
Chanzo: Mwananchi