Fiston Mayele tumepigwa mchana kweupe

Fiston Mayele tumepigwa mchana kweupe

Yule Djuma Shabani ni mtu na nusu sana, ana mwendo mno yaani anapandisha vizuri mashambulikama inavyotakiwa kwa full back wa kisasa!

Halafu kuna Yanick Bangala, jamaa ni kiraka mzuri! Anacheza kwa usawia akicheza kama beki wa kati na hana tofauti akicheza kama kiungo mkabaji. Ana sambaza sana pasi za upendo, ana utulivu wa hali ya juu sana! Huyu akiwa As Vita ndio alikuwa akimuweka benchi Mukoko kwenye nafasi ya kiungo mkabaji.

Mchezaji mwingine mwenye kitu cha ziada ni Heritier Ebenezer Makambo atafunga magoli ya kutosha hasa ukizingatia udhaifu wa mabeki wetu katika ligi ya bongo.

Waliobaki hao akina Fiston Mayele hamna kitu, yaani tumepigwa mchana kweupe, Ukibisha wewe bisha ila mwezi wa 11 mje hapa kufukua huu uzi, Mayele Tu-Me-Pi-Gwa
[emoji38][emoji38][emoji38]
 
..hata mie nashangaa, unawezaje kum-judge mchezaji kwa mechi moja tuuu?
Rejea ya Obrey Chirwa na wengineo, ambao walihitaji muda kuzoea. Wachezaji wako wa aina mbili kuu..Kuna wanaozoea mazingira mapya kwa haraka zaidi na wanaohitaji muda mrefu kidogo kuzoea mazingira. Hawawezi wote wakawa sawa ndugu. Ila kiushabiki waweza ongea chochote upendacho, Ila kiufundi iko hivyo kama nlivyoeleza
Sijui huko alipo kwa sasa anajisikiaje 😄
 
Back
Top Bottom