Hii ni changamoto, yaani utoke chuo usifanye mambo kilegevu au huku unaona noma. Kuna graduqte mmoja mtaani kwetu alifungua duka, anaideas nyingi sana. Akaanza kutuuzia juice ameweka na udambwiudamwi flani. Cha ajabu yeye leo ipo kesho haipo, sababu haipo matunda yamejaa sokoni. Anajiona kama hastahiri anachokifanya, anatakiwa kuwa juu kuliko hapo.
Wakati huo mama anayetuuzia mchicha miaka sita hii kila siku atapita muda uleule iwe mvua iwe jua. Anaconsistency ya kimataifa. Huyu wa flemu qnashindwa nini huyu?