Flemu nyingi za biashara huku mitaani kwa asilimia kubwa zimejaa watu wa namna hii

 
Nakubaliana na wewe, aliyeko salama ni innovator hasa kwenye field ya teknolojia.
Maduka mengi hasa yale ya mitaani ambako hakujachangamka ni kama mawakala wa kuuza bidhaa za vuwandani tu huku wao wakiambulia vichache kama sio negative profit au kumnufaisha mmiliki wa flemu. Hesabu ni muhimu sana.
 
Nimetoa ushauri kama mteja sio kama mfanya biashara. Wahusika wanaweza kuleta changamoto kwa haya niliyoobserve.
Uko sahihi sana na uache uongo. Wewe ni mfanyabiashara fulani au uliwahi fanya biashara. Wateja siku zote huona wafanyabiashara wanafaidi, wewe huwezi pangilia hoja hivi kama hujawahi jaribu biashara. Umeandika ukweli ukapitiliza
 
Uko sahihi sana na uache uongo. Wewe ni mfanyabiashara fulani au uliwahi fanya biashara. Wateja siku zote huona wafanyabiashara wanafaidi, wewe huwezi pangilia hoja hivi kama hujawahi jaribu biashara. Umeandika ukweli ukapitiliza
🤝
 
Biashara nzuri ni betting fremu simu Yako shelfu bando MTAJI stake na utataijirika ila ukitaka maonesho kagungue duka kubwa siku nzima umeuza 2000
Betting sio biashara ni bahati. Hakuna bilionea wa kubeti mkuu labda kama awe ni insider anapanga matokeo.
Mtu haishi kwa bahati nasibu anpaswa kuishi kwa mipangokazi thabiti.
 
Betting sio biashara ni bahati. Hakuna bilionea wa kubeti mkuu labda kama awe ni insider anapanga matokeo.
Mtu haishi kwa bahati nasibu anpaswa kuishi kwa mipangokazi thabiti.
Hawa ni wakina nani au unaropoka vitu usivyo vijua kufuata mkumbo wa watu mitandaoni
 

Attachments

  • Screenshot_20240827-114615.jpg
    561.6 KB · Views: 4
Hawa ni wakina nani au unaropoka vitu usivyo vijua kufuata mkumbo wa watu mitandaoni
Bill hajatajirika kwa kubet. Ni kwa kudelelop computer software ambayo inatumika kwenye mbio za farasi ambako ndio mchezo anachezea kamali.
Ndio maana mwishoni nilisema labda awe ni insider.
Watu wanamambo mengi alafu unaonyeshwa moja la kinyonge ili wakuokote.
 
Wewe akili timamu huna kama hajatajirika Kwa betting kwanini awekwe kwenye list hivi unaakili timamu kweli
 
Ndio maana huko juu umeshauriwa kuepuka kutoa ushauri technical kwa mambo ambayo hujayafanya ama kutumia japo masaa yako 12 kuyafanya.

Uko serious unalinganisha biashara ya juice center na Muuza Mchicha wa kwenye beseni?

Huyo Muuza Mchicha anatambulika na TRA? Analipa kodi ya Pango la fremu? Ametumia mtaji kiasi gani kuwekeza kwenye huo Mchicha kulinganisha na mwenye fremu ya juice?

Jiepushe sana kushauri jambo ambalo hujawahi kuliishi wala huna uzoefu nalo japo wa lisaa limoja tu.
 
Ndugu mchambuzi wa mafremu hiyo namba nne ilinikuta sehemu kuna kabinti kamesomeshwa kupitia kamgahawa fulani pale maeneo yangu ya kujidai mpaka chuo basi kale kabinti kalikua kanahudumia kizungu zungu bhana ukifika kanauliza" hellow hiiii unataka sauuuup? Na chapaaaait ngaaaaaipi? Basi full uzungu wakati asilimia kubwa ya wateja wa pale ni kama wa kawaida tu
 
Nalinganisha katika level ya utoaji wa huduma. Mimi ndiye ninayehudumiwa.
Wa flemu hana consistency ya uuzaji wa moja ya product yake ambayo wateja ni wengi kuliko hata uwezo wake wa kuzalisha. Hata sasa alishaga acha siku nyingi kwa sababu ambazo ziko ndani ya uwezo wake. Kila kitu anacho hadi nguvu na nauli ya kufatia matunda. Wala sio masikini.

Muuza mchicha yeye na product yake bila kujali ukubwa au udogo wake kila siku iko sokoni.

Hapo TRA anamzuiaje mtu kuamka na kutuletea bidhaa mfano. Nisome context sio content yangu mkuu.
 
Kumfungulia wife biashara home akiuza na watoto kuna shida gani?

Nimetoka chuo nikajiunga na machinga hatimae nikapata kiflem kuna shida gani? N.k

Hayo ya kutoa huduma mbovu ni tabia ya mtu tu hata angefungua kwa motivation zingine zaidi ya hizo
Mkuu naona imekutouch
 
Biashara nyingi,,,,haziwezi kujiendesha na kutoa matumizi ya kila siku kwenye familia.
Tatizo linalowakabiri wengi ni kutaka kuchukua faida kwenye biashara ambayo haina hata Mwaka mmoja kwenye game!

Umefungua biashara June, leo August unataka nauli na pesa ya msosi itoke hapo hapo kwenye mtaji wa hiyo biashara, lazima ife tena inakufa kifo baridi.

Biashara ni Sawa na mtoto, inaanza as an idea (conception + mimba), then inafunguliwa rasmi baada ya research and planning (anazaliwa mtoto) na baada ya kufunguliwa ndipo inasimamiwa kuhakikisha ile idea inaenda Kama ilivyokusudiwa na kuonwa (vision = mission) (mtoto analelewa na kufundishwa misingi ya kwanza ya ubinaadam, kula, kutambaa na hatimaye kutembea) hapo tayari ni miezi imekata.

Kwenye process yote hiyo ni lazima kuhakikisha mtaji unarudi kwenye mzunguko na faida yake pia huku matumizi na mengineyo yakitoka kwenye mfuko mwingine.

Sasa mimba uitunge leo, mtoto azaliwe leo, atambae leo, kutembea na kukimbia juu leo leo?

Hiyo ni biashara kichaa not otherwise.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…