Forbes Africa: MO Dewji ndiye tajiri namba 1 Afrika Mashariki na Kati

Forbes Africa: MO Dewji ndiye tajiri namba 1 Afrika Mashariki na Kati

Ila Tanzania ni nchi mojawapo masikini duniani ukilinganisha na Kenya
30-most-and-least-developed-countries-according-to-human-v0-o2yjdjyjneq81.png
 
Basi hapa watakuja watu kusema ni pesa za urithi na kwamba eti Bakhresa na Mengi ndio matajiri self made

Kwanza watu wanakosea sana kumfananisha Mo na kina Bakhresa kwa sababu hawa sio rika moja, kama tunataka kumfananisha Said Bakhresa basi tumfananishe na Gulam Dewji, Baba yake Mo ambaye naye ni self made hao ndio rika moja

Mo anatakiwa afananishwe na Watoto wa kina Said Bakhresa kama akina Yusuph ambao ndio rika moja na ambao obviously nao utajiri wao ni wa kurithi toka kwa Baba zao hawa
[/QUOTduuuuuuh p
 
Hii na kutangaza mwanafunzi bora kitaifa inafaida gani? inamsaidia nini mtzd wa kawaida hata aliyeajiriwa kwenye kampuni zake na kuendelea kupuchwa mshahara, hovyo.
 
Kwanza siyo muaminifu na bakhresa (chawa wake) yupo radhi kuua biashara yako ili yake iendelee.

Mfano; baharini, yaani chawa wa bakhresa wanahonga kwa manahodha wa boat nyingine ili wazitie chumvi vife vyake viendelee kuwepo, hataki ushindani, but kwenye mpira kachemka kakutana na magwiji Yanga na Simba!.

Juzi alikuwa radhi kumuaribia bwana mdogo Feisal, kisa pesa!.
Huyo wa kwenye mpira ni mtoto wa Bakhresa, si Bakhresa mwenyewe.

Sent from my TECNO CG6 using JamiiForums mobile app
 
Kwa Tanzania tajiri namba moja kila mtu anamjua ni SSB,..hizo nyingn ni michongo tu, labda kama umetoka mbwinde juzi.
 
Ripoti ya utafiti iliyotolewa na Forbes Januari 30, 2023, Mo Dewji alikuwa nafasi ya 15 hapo awali, amepanda kwa nafasi mbili kutokana na utajiri wake unaokadiriwa kufikia Dola 1.5 bilioni (Sh 3.5 trilioni).

Mwekezaji wa Klabu ya Simba, Mohammed Dewji 'MO Dewji amepanda kwa nafasi mbili katika orodha ya watu matajiri zaidi Afrika kwa mujibu wa jarida la Forbes akishika nafasi ya 13 kwa sasa huku akiongoza chati hiyo kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Katika ripoti ya utafiti iliyotolewa na Forbes jana, Mo Dewji alikuwa nafasi ya 15 hapo awali, amepanda kwa nafasi mbili kutokana na utajiri wake unaokadiriwa kufikia Dola 1.5 bilioni (Sh 3.5 trilioni).

Mo ambaye anamiliki kampuni mbalimbali za vyakula, vinywaji baridi pamoja na kilimo amekuwa kichocheo kikubwa kwenye ukuaji wa uchumi na kukuza ajira nchini hasa kwa vijana.

Akizungumza baada ya kutajwa kwenye orodha hiyo, Mo amesema mkakati wake ni kuendelea kuongeza ajira kupitia kampuni zake ambapo, kwa sasa ameongeza ajira kutoka 28,000 hadi 35,000.

Hata hivyo, amesema kuwa mkakati wake ni kuzalisha ajira 100,000 ifikapo mwaka 2029.

“Tunashukuru mazingira ya biashara ni mazuri sana kwa sasa, azma yangu ni kuendelea kuongeza uwekezaji na kusaidia jitihada za Serikali kuzalisha ajira za kutosha,” alisema Mo Dewni.

Bilionea wa Nigeria aliyefanya uwekezaji wa uzalishaji saluji hapa nchini, Aliko Dangote anaongoza orodha hiyo ya watu matajiri zaidi Afrika akiwa na utajiri wa Dola 13.5 bilioni akifuatiwa na Johann Rupertwa Afrika Kusini mwenye utajiri wa Dola 10.7 bilioni.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (Caf), Dk Patrice Motsepe ambaye anamiliki klabu ya soka ya Mamelodi Sundowns, anashika nafasi ya tisa katika orodha hiyo akiwa na utajiri wa Dola 3.2 bilioni.

Ni orodha ambayo 10 bora yake imetwaliwa zaidi na mabilionea kutoka nchi za Nigeria, Afrika Kusini na Misri mtawalia.

Nafasi ya tatu katika orodha hiyo inashikiliwa na Nicky Oppenheimer(Afrika Kusini), nafasi ya nne yupo Abdulsamad Rabiu (Nigeria), nafasi ya tano kuna Nassef Sawiris (Afrika Kusini), akifuatiwa na Mike Adenuga (Nigeria), Issad Rebrab (Algeria), Naguib Sawiris (Misri), Motsepe (Afrika Kusini) na Mohamed Mansourwa misri.
View attachment 2501750
Tajiri wa jarida la Forbes huyo! Ukija kwenye uhalisia, Mwamedi ni mtoto mdogo sana.

Angekuwa ndiyo tajiri namba 1, asingekuwa anahangaika ku copy na ku paste bidhaa za wenzake. Ubunifu 0! Anatembelea tu nyota ya mbumbumbu fc.
 
Kweli hata dini umesoma kidogo?
Wataka kusema nn? Uislamu ni mmoja hakuna dhehebu la uislamu achaga zako ..Leta izo Aya kuonyesha Mungu kaleta madhehebu ndani ya uislamu kwamba hata msikitini mmoja hawawezi kushare na vitabu tofauti.
 
Back
Top Bottom