Force Account inawamaliza mabosi wa Serikali, Waziri Mkuu anashuhudia madudu ya kutisha

Safi sana ulivyoidadavua, lakini ulichoongea ni hewa tupu.
Unawezaje kujenga kwa Force Account mradi hadi wa bilioni 10 kwa kumtumia Afisa manunuzi, fundi Maiko na wasimamizi Kamati ya Ulinzi na Usalama.

Halafu leo tunashangaa TAKUKURU wanaitwa kila mradi wa Force Account!
Tunaona makosa lakini hatuelewi!!

Huu ndio ujinga usiokifani watu kujijengea uhalali wa kusimamia fedha za miradi ambapo sasa tunampa Waziri Mkuu kutembelea miradi akiambatana na TAKUKURU badala ya kusimamia proffessionals wa Project Management na Supervision.

Kwa hii hoja hata ukiamua kujitengenezea utaratibu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama kusimamia urukaji wa ndege ni sawa tu maana wanajitengenezea ulaji.

Kwa kifupi hoja hii haina mantiki wala uhalali.
 
Force account imejenga miradi mingi sana ya zahanati nchi nzima
umeelewa kilichoandikwa ? hatuzungumzii namba tunazungumzia ubora? kwanini kuna sheria ya manunuzi? aliyeleta/ruhusu matumizi ya force account ni mpumbavu mmoja aliyekuwa anajidai kujua kila kitu. ni kweli force Account imo kwenye sheria lakini si kuna sababu na mazingira ya kuitumia?
hongera kwa kuwa mjinga kwa kiasi chako
 
Ha ha ha!
Asante mkuu, kuna watu kuelewa kitu , toka utotoni mwao ni kwa viboko tu!
 
Je hawa NCC wanaweza kujenga chumba cha darasa kwa 20mil ikatosha? Nijibu kwanza ndio tuendelee.

Usijeneralize kwamba kila halmashauri wanakunywa pesa za umma.

Sipingi tabia za wanasiasa kujiona wajuaji.

Sipingi serikali kupenda bei chee, chee ambayo inalighalimu taifa hasara katika sekta ya ujenzi kitaalam.
 
FORCE ACCOUNT ili fail hata kabla ya kuanza. Sasa hivi ndiyo matokeo yake yanaanza kuonekana kwa walio wengi
Vyama huru vya kitaaluma, ACET, -Association of Consilring Engineers, AAT-Association of Architecs, Associstion of Quantity Surveyors, na hata vya kikandarsi CATA, ACCT, TACECA na vyama vingine vilipaza sauti kupinga Force Account katika sekta ya Ujenzi.
Serikali sikivu ikaweka pamba kwenye masikio.

Sasa tunavuna kile tulikiwa tuna onya, masikini Waziri Mkuu ziara zake zote anaambatana na TAKUKURU.
Masikini TAUKIRU hawana la kufanya zaidi ya kuwafunga watuhumiwa wa wizi kwa mfumo mbaya wa Force Account
 
Watamalizwa hao watumishi kwa makosa yawazi kabisa. Kitendo cha ku implement hiyo force account kilikuwa ni suicidal mission kwa upande wao.
Tulishakosea kama inchi. Tuachane nao na tuanze upya kwa kulitoa hilo pepo la Force Account. Ingelikuwa ni ajabu sana kama FORCE ACCOUNT ingelileta sustainable results.
Watumishi wataishia kusimamishwa na kuchunguzwa hivyo kutapelekea ombwe la watumishi na kuyumba kwa huduma za kijamii.
Hili dude tulishalikosea, ni kosa la inchi siyo lawatumishi tena. Tuanze upya
 
Umejaribu kufafanua kitu ambacho hakitekelezeki Kwa kizazi hiki Cha Tanzania. Hizo kamati za ujenzi, manunuzi na mapokezi haziko na wataalam wa ujenzi bali zimeundwa na watumishi ambao hawana utaalam wowote wa ujenzi. Mfumo wa Force account unataka wahusika wawe na uzalendo na je huo uzalendo upo? Kumbuka hao wajumbe hawalipwi chochote eti watangulize maslahi ya nchi mbele seriously? Ndo maana wanaamua kujilipa Kwa njia hiyo. Ni Bora mpe mkandarasi mwenye utaalam kazi huku ukiweka sheria za nchi vizuri ili akikosea awajibishwe kuliko hii kitu ambayo ni ujenzi wa hovyo kabisa kutokana na wahusika kutokuwa na ujuzi wa kutosha.

Binafsi nimeshiriki katika ujenzi wa majengo mengi Kwa mfumo huu wa force account kama mjumbe kwenye kamati ya ujenzi na manunuzi. Nakwambia bora mfumo wa kumtumia mkandarasi kuliko huu. Yaani kitu kinachouzwa elfu 50 watu wanaenda kununua laki 2 kumbe wamenunua laki hamsin ya mwenye duka Ili awaandikie rist fekina wao wanabaki na laki. Kujenga majengo Kwa kutegemea eti wahusika watangulize uzalendo Kwa Tanzania hii ni sawa na kuota ndoto umekuwa rais wa urusi.
 
Mkuu huyo alitoa maoni ni mwanasiasa.
Tatizo kubwa watu alimradi wamechaguliwa basi wanajiona wana akili za ziada.
Watu kwenye hii fani ya ujenzi wan usomi hadi kiwango cha PhD lakini wanasiasa wanadharau ushaur wao kitaalm.

Hii force Account matke yake bado hatujayaona.
Philosophy ya Construction ni Economy, Method, Durability, Safety na Quality.
Sasa ita Kamati ya Ulizi na Usalama ili iyadadavue na tupate jumba au daraja lenye tija nchini.
 
Kumtumia Mkandarasi si ndiyo hayo ya kibanda cha mabati 15m? NI LAZIMA TUJENGE UZALENDO....

PROCURING ENTITIES zina Wataalam wa mipango, fedha, Manunuzi, sheria, uhandisi.... je ni kipi ambacho kinashindikana kwenye Force Account?

Kamati ya usimamizi ipo chini ya ushauri wa MHANDISI wa PROCURING ENTITY wakati mwingine YEYE ndiye katibu wa kamati

Manunuzi wanashauriwa na AFISA MANUNUZI wa PROCURING ENTITY wakati mwingine YEYE ndiye katibu wa kamati

Kamati ya UKAGUZI na mapokezi wanashauriwa na Mjandisi [technical specifications] na AFISA Manunuzi [nyaraka na raratibu] na wakati wataalam hawa ni wajumbe wa hizi kamati..

Shida siyo KAMATI KUKOSA UELEWA, SHIDA NI UPIGAJI NA KUKOSA UZALENDO!!!!

Mbona majengo BINAFSI WANAJENGO tena mtu moja bila Kamati???? Hatujiulizi hili???

Hata tukitumia Kampuni ni YALE YALE TU!!! Panapohitajika condo 18mm mtakubaliana mnaweka 12mm, panapohitaji condo 5 mtaweka 3, Paso OP ohitaji clearing, cut an feel mtaeeka imefanyika!!!

All in all bila kudhibiti UPIGAJI NA KUJENGA UZALENDO HAKUNA KITU....
 
Force account haina shida, shida ni WATU KUKOSA UZALENDO.....
 
Kamati za mradi na sii kamati ya ULINZI na USALAMA!!!!!

Kwani ukitumia Mkandarasi wanaoandaa nyaraka za Manunuzi Michoro, BOQ na Mikataba si ndiyo hao hao WATAALAM unaosema HAWAWEZI KUSIMAMIA?

Si ndiyo tender Documents ambazo zinatengenezwa zikiwa na MAPUNGUFU MAKUSUDI ili kila SIKU ZIZALISHE MAVARIATIONS ILI KAMPUNI NA WAHUSIKA MPIGE HELA!!!????

Ili Mkandarasi aandikiwe CERTIFICATE na Alipwe, au akabidhi mradi ni LAZIMA HAO WATAALAM WA PROCURING ENTITY wakakague, Je UKISEMA hawawezi kusimamia Force Account wataweza kumsimamia Mkandarasi mwenye utaalamu wake?

HOJA SIYO FORCE ACCOUNT, HAPA HOJA NI NYOYO ZA WIZI NA UPIGAJI!!!

BOQ inasema kitasa kiwe UNION au ORLANDO halafu wanaenda kununua MAVITASA YA OVYO HALAFU MNAKUJA KUMSINGIZIA FUNDI MAIKO; HAMUONI AIBU????

BOQ inasema hard Wood nyie mnaweka mimbao ya ovyo HALAFU MNASINGIZIA FORCE ACCOUNT!!!!!! Ovyo Kabisa!!!!!

Mnajificha kwenye shamba la karanga!!!!

Kama hoja ni kukosa maarifa na ujuzi mbonaikifika kujenga MAJUMBA YENU MNAJUA VIZURI NA VIBAYA? MNAJUA MOAKA NA RATIOS!!!!

Sheria zetu za kukabiliana na vitendo vya RUSHWA na UHUJUMU MCHUMI xina mapungufu.... kelele nyingi za force ACCOUNT ni feki na wala siyo HALISIA. .

wanasema tutumie WAKANDARASI, Shwali ni Je Mkandarasi huyu asiye MALAIKA atasimamiwa na nani ili akidhi ubora wa mradi? Mtasema tuajiri CONSULTANT amsimamie, Na huyu CONSULTANT akicollude na contractor si ndiyo TUTALIA???? maana mpaka wanasheria nguli wanao......

Jamani shida ni WATU WAMEKUWA WABINAFSI SANA.... hata ukitumia contractor watapiga tu UNLESS we rectify the core causes!!!!
 
 
Tumeyaona mengi HATA KWA KUWATUMIA WAKANDARASI,,

rates anazoqoute Mkandarasi ni rate za juu kuzidi market rates, tender Documents zinaandaliwa na mapungufu makusudi ili hela zipigwe, wakati wa utekelezaji ratios zinachakachuliwa, vifaa kama nondo badala ya kuweka mfano 18mm inayouzwa 50k plus zinawekwa 12mm zinazouzwa 20k plus, badala ya kuweka nondo 4 zinawekwa 3 na madudu mengine mengiii.....

Tusimamie MALI ZETU WATANZANIA VINGINEVYO HAKUNA SUNGU SUNGU WAKUTULINDIA MALI ZETU....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…