JE UNAUNGUZAJE ACCOUNT?
Kwanza nianze kwa kutoa pongezi kwa umoja wa nchi za ulaya maana this week shiling yao imefanya vizuri sana, pia nitoe pole kwa USA ambaye week hii shilingi yake imepitia wakati mgumu sana!!
Leo nimeona si mbaya tukijulisha ni vipi unaweza unguza account?? na je ni vipi unaweza jiepusha na kuunguza account??
Tuanze na hii interface ya MT4 kama inavyoonekana...
Kutoka kwenye picha...
Balance.
Hii inaonyesha kiwango ulichoweka ukijumlisha na faida. Open positions hazina effect kwenye balance. Balance inabadilika ikiwa tu ume close position either kwa loss au faida!
Equity/Trading equity.
Hiki nikwango cha pesa utachobaki nacho ikiwa positions zote zimefungwa. Kwa lugha rahisi ni jumla inayobaki baada ya kutoa hasara na ukijumlisha faida katika kila position zinazo-run (unrealized profit and loss).
Equity = Balance – unrealized loss or profit.
So ukiwa
huna running positions, Equity = Balance.
Kama ukiwa na open trades/position mara nyingi balance inakua kubwa kuliko equity.
Margin
Ni kiasi cha pesa kinachohitajika ili ku-open positions. Ukiwa na margin ndogo huwezi kufungua position au hutaweza kufungua trades! Hiki kiasi kinatolewa kwenye equity ili uweze ku-open new positions.
Margin Level
Hii ni ratio ya Equity na Margin
Margin level = (Equity/Margin) *100
Equity ikiwa kubwa margin level pia inakua kubwa, Margin ikiwa kubwa Equity inakua ndogo.
SASA NI VIPI UNAUNGUZA ACCOUNT?
Kabla sijasema ningependa niongeze maneno mawili ili twende pamoja!
Rejea hii formula…
Margin level = (Equity/Margin) *100
1. Margin call
Hii ni level ya
margin level ambayo ikifikiwa tu, kwanza unapewa warning na broker wako kwamba hauna kiasi cha kutosha kufungua new positions au kuhimili positions zinazorun hasa zinazorun in loss!! Kila broker ana level yake ya marginal call,
wengi ni 50% ila wengine mpaka 100% of marginal level!
Ikiwa equity ni ndogo kuliko margin, hapa ndio tatizo linapoanza. Na ikiwa kiwango cha equity ni nusu ya margin hapa utapewa warning na broker wako!!
Stop out level
Hii level inafikiwa ikiwa Equity level ni ndogo sana kuliko margin. Mfano margin level ikifika 20% (hii inategemea na brokers, inatofautiana) hapa ndio utaona moto unawake kwenye account yako! Wataanza kufunga position moja baada ya nyingine! Mara nyingi wanaanza na position yenye loss kubwa!!
Jua wakiwa wanafunga positions wanakata ile loss ya kila position mfano kama una loss ya -12 USD wataikata kwenye balance yako mpaka zote ziishe!!
Na ikifikia hii level jua ndio account imeungua!!
JUST A PIECE OF ADVICE!
Wakati unachagua broker usiangalie tu mwenye bonus jitahidi pia kuangalia broker mwenye margin call ndogo na Zaidi ya yote angalia broker mwenye margin stop out level ndogo kwa usalama wako!!
Na wakati una trade hakikisha marigin level haishuki chini ya 50%
Angalia leverage unayotumia isiwe kubwa sana(unaweza pia kuchagua kubwa ila uwe makini), pia kuwa makini unapofungua positions (zenye position size kubwa) nyingi zinazorun katika loss maana hizi mara nyingi ndio chanzo cha kuunguza account!!!
Tuko pamoja!!
Lodrick Thomas (Eng.)