Baada ya kijana mwenzetu ndugu Ontario kuamua kuwasaidia vijana wenzake kuwapa elimu juu ya Forex ili waweze kujikwamua kiuchumi, kumeibuka niseme kama kundi fulani ambalo naona ni organized kabisa ambalo wanapinga juhudi hizi ama harakati hizi za Ontario, labda sababu ya chuki tu ama roho ya husda ama roho za kwanini kwamba vijana wengine waendelee kimaisha.
Watu hawa wanaanzisha na thread kabisa na wengine hutumia hata lugha chafu na za kejeli(mmeshuhudia katika comments mbalimbali) ili tu kuwa dissapoint wale wanaondelea kwa kasi kujiunga kuipata elimu hii adhimu. Wengine wanadiriki hata kuweka na links sjui za kuaminisha ni utapeli lakini hakuna la maana,wengine kutunga stori za watu waliofilisika yote haya ili tu vijana walioamua kuwekekeza muda wao na akili zao kujikwamua kimaisha wanashindwa na waendelee kukaa tu na kuirushia lawama serikali.
Nachoshangaa ni kwamba wao waliofanikiwa wamefanya nini kuwasaidia vijana? Utakuta hamna kitu, hizi ndo roho za baadhi ya watanzania na pengine afrika kwamba inamuuma sana kumuona mwingine either anaamua kujikwamua kiuchumi au anafanikiwa.
Vijana mlioamua kuwekeza nguvu zenu kujikwamua kiuchumi, endeleeni na nguvu hio, achananeni na kelele hizi za hawa wenye husda, wao nina uhakika 80% wengine wanafanya, lakini sasa ile roho ya kwanini inawasumbua sana mana wao wanataka wafanikiwe wao tu. Watu wenye moyo kama wa ndugu Ontario ni wachache sana, mtu alie tayari kuhakikisha maisha ya vijana wengine yanainuka kama ambavyo yeye imemsaidia.
Just imagine mtu anatoa hoja kwamba hawezi kumsifia mwanaume mwenzake, mtu kama huyu tukimuita ignorant ama roho ya husda tutakua tunakosea? Hizi juhudi ilifikia ontario na cabinet yake kuonana na ndugu Max, hivi kweli JF iweke kitu ambacho ni utapeli kweli? Yani matapeli waweze kuonana kweli na uongozi wa JF ? Sidhani na hamna kitu kama hicho.
Nachofurahi ni kwamba watu wanaendelea.kujiunga na hii ni positive vibe kwamba baadhi ya vijana wanaojielewa wanaamka na kuacha lawama kwa serikali, kuamua kubaki maskini ama kufanikiwa kimaisha ni uamuzi wako.
Mods": huu uzi utakua edited, hawa watu tutakua tunawataja kabisa, mana hawana lengo zuri kabisa mana wameanza kutumia mgongo wa ontario vibaya.