Ni rahisi. Mfano leo Bongo US$ 1 inauzwa kwa tshs 2250 na kununuliwa kwa tshs 2200. Sasa mtu anaweza kutarajia Dola itapanda thamani kwa maana kufikia kuuzwa kwa tshs 3000 ifikapo December mwaka huu, hivyo akanunua sasa hivi labda dola zake 1000. Atakuwa ametumia tshs 2,250,000. Akasubiri ikafika hiyo December kweli dola 1 ikawa imepanda mpaka kuwa inauzwa tshs 3000. Huyo mtu akauza zile dola zake 1000 na kupata tshs 3,000,000. Hapo atakuwa amepata faida ya 750,000 nzima kutoka 2,250,000 aliyonunulia.
Kinyume chake kinawezekana, kwa maana alitegeme dola ipande thamani ifikapo december lakini ikashika chini ya aliyonunulia, mfano ikashuka mpaka tshs 2000 kutoka tshs 2250 aliyonunulia. Sasa akitaka kuuza zile dola zake 1000 wkt huo atapata tshs 2,000,000 na hivyo kuw amepata hasara ya 250,000 ktk huo muamala.
Sasa huu mchakato unafanyika globally kwenye system the forex. Broker ndio mnunuzi na muuzaji wako. Ni kama vile unavyoenda Bureau de Change...ukiwa na shikingi unataka dola unapata, ukiwa na dola unataka shilingi unapata.
Natumai nimekujibu swali lako.