Forex: Biashara Yenye Utajiri Mkubwa Zaidi Duniani Ambayo Hakuna Benki Itataka Uijue!

Forex: Biashara Yenye Utajiri Mkubwa Zaidi Duniani Ambayo Hakuna Benki Itataka Uijue!

Status
Not open for further replies.
View attachment 532904

Analyisis yangu kwenye EUR/JPY 15min chart inanionyesha Falling wedges pattern. Nitabuy trend yangu ikibreak upper line kwenye green arrow, Stop loss yangu itakuwa chini ya hiyo candle itakayobreak kwenye green arrow, na take profit yangu itakuwa sawa na distance ya blue dots. Niko sahihi bosses Bavaria na ONTARIO ?

Haupo sahihi kabisa mkuu.

15 minutes ni muda mfupi sana kiasi kwamba unamaliza kufanya analysis zako chat zimeshabadilika..

Ulitakiwa uanze na time frame kubwa, ndo uje kwenye timeframe ndogo kwenye kufungua position zako.

Analysis fanyia kwa Monthly, Weekly and Daily.

Open your position at H4 and H1.

For scalpers may use 30, 15 and 5 minutes kwenye kufungua position zako..

Hapo umeingia chaka..
 
Hakuna news yeyote, kwa experience traders walikuwa wanaona kabisa Euro ipo kwenye over bought na siku yeyote wakati wowote itaanguka..

Next week tegemea Euro kuanguka vibaya sana mpaka demand and supply zimeet at equilibrium.
But kuna news za unemployment Germany nadhani zimeangusha sana Euro Leo mkuuu
 
63b5fdb2bb16806d834f420e805b2c6f.jpg

Kesho nazipeleka First National Bank Kwa ajili ya forex trading,nitaanza kutrade baada ya ONTARIO kuniruhusu; ni ka $1000 nadhani katatosha Kwa kuanzia.
KA DOLA 1000 duuh umetisha arifu!!

BTW una undugu na chenge??
 
JE UNAUNGUZAJE ACCOUNT?

Kwanza nianze kwa kutoa pongezi kwa umoja wa nchi za ulaya maana this week shiling yao imefanya vizuri sana, pia nitoe pole kwa USA ambaye week hii shilingi yake imepitia wakati mgumu sana!!

Leo nimeona si mbaya tukijulisha ni vipi unaweza unguza account?? na je ni vipi unaweza jiepusha na kuunguza account??

Tuanze na hii interface ya MT4 kama inavyoonekana...



View attachment 533296

Kutoka kwenye picha...

Balance.


Hii inaonyesha kiwango ulichoweka ukijumlisha na faida. Open positions hazina effect kwenye balance. Balance inabadilika ikiwa tu ume close position either kwa loss au faida!

Equity/Trading equity.

Hiki nikwango cha pesa utachobaki nacho ikiwa positions zote zimefungwa. Kwa lugha rahisi ni jumla inayobaki baada ya kutoa hasara na ukijumlisha faida katika kila position zinazo-run (unrealized profit and loss).

Equity = Balance – unrealized loss or profit.

So ukiwa huna running positions, Equity = Balance.

Kama ukiwa na open trades/position mara nyingi balance inakua kubwa kuliko equity.

Margin

Ni kiasi cha pesa kinachohitajika ili ku-open positions. Ukiwa na margin ndogo huwezi kufungua position au hutaweza kufungua trades! Hiki kiasi kinatolewa kwenye equity ili uweze ku-open new positions.

Margin Level

Hii ni ratio ya Equity na Margin

Margin level = (Equity/Margin) *100

Equity ikiwa kubwa margin level pia inakua kubwa, Margin ikiwa kubwa Equity inakua ndogo.

SASA NI VIPI UNAUNGUZA ACCOUNT?

Kabla sijasema ningependa niongeze maneno mawili ili twende pamoja!

Rejea hii formula…

Margin level = (Equity/Margin) *100

1. Margin call

Hii ni level ya margin level ambayo ikifikiwa tu, kwanza unapewa warning na broker wako kwamba hauna kiasi cha kutosha kufungua new positions au kuhimili positions zinazorun hasa zinazorun in loss!! Kila broker ana level yake ya marginal call, wengi ni 50% ila wengine mpaka 100% of marginal level!

Ikiwa equity ni ndogo kuliko margin, hapa ndio tatizo linapoanza. Na ikiwa margin ni nusu ya margin hapa utapewa warning na broker wako!!

Stop out level

Hii level inafikiwa ikiwa Equity level ni ndogo sana kuliko margin. Mfano margin level ikifika 20% (hii inategemea na brokers, inatofautiana) hapa ndio utaona moto unawake kwenye account yako! Wataanza kufunga position moja baada ya nyingine! Mara nyingi wanaanza na position yenye loss kubwa!!

Jua wakiwa wanafunga positions wanakata ile loss ya kila position mfano kama una loss ya -12 USD wataikata kwenye balance yako mpaka zote ziishe!!

Na ikifikia hii level jua ndio account imeungua!!

JUST A PIECE OF ADVICE!

Wakati unachagua broker usiangalie tu mwenye bonus jitahidi pia kuangalia broker mwenye margin call ndogo na Zaidi ya yote angalia broker mwenye margin stop out level ndogo kwa usalama wako!!

Na wakati una trade hakikisha marigin level haishuki chini ya 50%

Angalia leverage unayotumia isiwe kubwa sana(unaweza pia kuchagua kubwa ila uwe makini), pia kuwa makini unapofungua positions (zenye position size kubwa) nyingi zinazorun katika loss maana hizi mara nyingi ndio chanzo cha kuunguza account!!!

Tuko pamoja!!

Lodrick Thomas (Eng.)
Mkuu samahan kwa usumbufu unaweza kuelezea na pip kidogo na jinsi ya kungalia
Sijui ni ngeli inasumbua[emoji119] [emoji119] [emoji119]
 
KA DOLA 1000 duuh umetisha arifu!!

BTW una undugu na chenge??
Hivyo ni tuviela tudogo tu we ngoja uje kuwa guru wa forex utanikubali ninachokwambia,kama ONTARIO anapiga pesa ya mafuta ya gari yenye CC2400 ndani ya masaa kadhaa,sembuse ivyo tuviela vya mboga,ila simaanish ni pesa ndogo ni nyingi ila naamin tutamilik zaidi ya hiyo,FX sio mchezo wa nguvu ya buku, FX ijue nguvu ya PIPs,
 
Wewe unatumia Bank gani?
Mkuu me bado sijajishusha kwa live Acc.. Coz bado najinoa.. Ila ukipitia nyuzi utaona kuna baadhi ya bank wadau wamezitaja.. Kama FNB bank, , na nyingine ambazo wanatoa master card,/Visa card..
 
Haupo sahihi kabisa mkuu.

15 minutes ni muda mfupi sana kiasi kwamba unamaliza kufanya analysis zako chat zimeshabadilika..

Ulitakiwa uanze na time frame kubwa, ndo uje kwenye timeframe ndogo kwenye kufungua position zako.

Analysis fanyia kwa Monthly, Weekly and Daily.

Open your position at H4 and H1.

For scalpers may use 30, 15 and 5 minutes kwenye kufungua position zako..

Hapo umeingia chaka..

Thanks mkuu imeeleweka, inabidi nikae chini nijifue tena top down analyisis. mdogo mdogo tutafika tu
 
Inaweza ikawa. Ila sio kila kitu news inahusika.

Demand and Supply nayo inahusika pia..
Kweli mkuu demand na supply ni factor muhimu pia.
Hebu chukulia Qatar anaamua kufanya manunuzi ya vifaa vya kivita kwa taslimu kwa gharama ya $10B na malipo yakatakiwa kufanyika basi lazima soko litikisike kidogo kwa mahitaji hayo ya pesa kwa hizo nchi zitatumia central bank zao kufanya biashara ya hizo hela
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Fungua uzi wako.[emoji84] [emoji84]
Ohhhh shit nilitaka kupaste sehemu nyingine niusome maana nilitoa kwa mdau ameupost hapo juu. Ngoja niufute maana unapotosha sikuwa najua mkuu.
Naomba pia ufute hii comment kwani itaendelea kuonesha. thanks sana
 
Naomba Msaada wa kufungua demo account nianze kucheza nayo huku nikiendelea kujifunza, Ontario, Complex and any other who knows how to do it please mnisaidie.
Mkuu Mimi nipo nasoma kitabu ili niijue Saudi hii Forex
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom