Mkuu!
Kiwango cha pesa inategemea broker na broker, wengine wanahitaji minimum 5USD, wengine 30usd wengine 50usd mpaka 100usd na zaidi!!
Lakini, Kabla hujaanza kuwaza kiwango cha fedha nakushauri atleast upitie vitabu ili uwe na basics za forex trading, hata sio ngumu kuielewa kama utaweza nia na juhudi!!
Okey, japo kwenye forex tunatumia applications kutrade ila forex sio program wala application, forex ni biashara kama biashara nyingine mfano mtu anaposema biashara ya magari au biashara ya nyanya and the alike.... sasa forex kwa lugha nyepesi ni biashara ya fedha za kigeni. Yaani unauza na kununua fedha za kigeni kama euro, pound, dola ili kupata faida (sometimes kuna hasara pia)!!
Biashara ya forex unaweza kuifanyia kwenye simu au kompyuta baada ya kujisajili kwa broker!!
Once again, usikimbilie kuweka pesa, jitahidi utafute vitabu viko humu (ukikosa sema upewe) download uanze kusoma taratibu!!ukisoma kama wiki moja utakua umepata mwanga kuhusu forex trade!! nenda youtube andika "forex trade" angalia videos pia zitakupa mwanga kuhusu forex!!
Kila la heri na karibu sana mkuu!!