Hawa vinyamkela wengine kwani unafikiri wanabisha facts basi?
Wanabisha kwa roho ya korosho tu, yani wakisikia Al-Watan kapiga dola elfu kadhaa katika siku moja huku kakaa anakunywa juisi na kuangalia TV Jumapili jioni wao roho inawauma saaana.
Wanakuwa hawapendi kusikia hivyo.
Wanazusha ume copy paste kutoka Ast, unawaambia nipe link nime copy paste wapi, wananywea.
Wengine wanakuwa hawaamini, wanaomba screenshot, na mwanao Al-Watan alivyo walii hata kukataa hajui, unataka screenshot, hiyo hapo, nimewapa.
Sasa sijui watakuja na nini.
Hii roho ya wivu wa kijinga ni mbaya sana, mtu akionyesha njia na kuwaambia wengine jamani nimepiga hapa maelfu haya ya dola, huyo ni wa kuona anawatakia wenzake mema, badala ya kumuuliza umepigaje, tuonyeshe na sisi tupige, watu wanamuwekea roho ya kijicho na kumuita tapeli.
Ndiyo maana watu wengine wanaamua kufanya mambo yao kimyakimya.
Mi nikipiga dollar zangu bila mlavumbi kujua nitapungukiwa nini?
Kichwa changu nakiamini hakuna semina niliyoenda wala kufundishwa na mtu nimekomaa mwenyewe kwenye demo na vitabu na kusoma news.
Huyo mlavumbi akikataa wakati hela zipo katika akaunti yangu nitapungukiwa nini?
Tatizo sitaki upotoshaji tu hapa kusema hamna trading Jumapili.
Kama kijijini kwao nyumba hazina taa za umeme basi asifikiri dunia nzima ndiyo iko hivyo.