Nina mashaka na uwezo wako wa kufikiri unaonekana unaishi kwa kukariri sana. Akina Bakhresa wametajirika kwa kuinvest kwenye foods na beverages so what...kila mtanzania anayetaka kutajirika SHARTI awekeze huko? Ila sishangai ndio maisha ya watanzania wengi..kuigana na kukopiana tu mtu mmoja kaamua kupika maandazi anauza vizuri baada ya wiki moja mtaa mzima unapika maandazi...no ubunifu no mawazo mapya, kwa hili sikushangai...This is 21st Century bro /sister kila mtu anapambana na hali yake hebu toka kwenye hilo box kwamba Ili mtu atoke kimaisha ni lazima akalime tikiti.
Eti tufanye kazi...kwako wewe kazi ni lazima mtu akimbiekimbie na mafaili kwenye korido au avuje jasho. Hivi unadhani wanaotrade forex hawafanyi kazi...hebu tenga muda kidogo ujifunze.
Ushauri wa mwisho..leave us alone. Tukitapeliwa tukiibiwa wewe inakuuma nini mbona ninyi watu mnawashwawashwa kama wastaafu eeh, huwa najaribu kufikiria ajenda yenu haswa ni nini na kwa nini mnaonekana kuumia kuhusu hata sisi wenyewe? Au uliunguza account[emoji23] [emoji23] [emoji23] vumilia ndio kujifunza mimi mwenyewe nimeunguza ila sina mpango wa kuacha sasa kwa nini wenzetu mnakuwa na hasira hivi, zilikuwa dola ngapi? Elfu?