Fountain Gate yainunua Singida Big Stars. Klabu hiyo sasa kuitwa Singida Fountain Gate Footbal Club

Uongozi wa Singida Big Stars umefanya maamuzi ya kuiuza timu hiyo kwa wamiliki wa Fountain Gate ambapo sasa timu hiyo imebadilishwa jina na kuwa “Singida Fountain Gate Footbal Club.”

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Singida Big Stars ambaye kwa sasa ni Mjumbe wa Bodi ya Singida Fountain Gate, John Kadutu amesema sababu ya kuiuza timu hiyo kwa Fountain Gate ni kutokana na changamoto mbalimbali za uendeshaji pamoja na nia ya kutaka kuipeleka mbali zaidi timu hiyo.

“Mnafahamu Fountain Gate wana timu nzuri ya Championship, wana timu nzuri ya vijana wa sekondari, ni mabingwa wa Afrika. Kwahiyo tukazungumza na watu ambao wanajua nini kinatakiwa kufanyika, usimtwishe mzigo mtu ambaye hajui shida zake,” amesema.

Aidha, Kadutu amesema moja kati ya masharti makubwa waliyowapa Fountain Gate ni kwa timu hiyo kuendelea kubaki mkoani Singida pamoja na kutumia jina la Singida ili kuwaenzi wote walioisapoti timu hiyo.

Naye, Rais wa Singida Fountain Gate, Japhet Makau amesema Fountain Gate imechukua asilimia 100 ya umiliki wa Singida Big Stars na Fountain Gate FC itaendelea kuwepo pia, huku akieleza kuwa hakuna tatizo lolote kwa timu hiyo kuendelea kubaki Singida kwani ilikuwa ndani ya mpango wao kufanya hivyo.
Huenda Mwigulu amehisi anaweza kutolewa hazina
 
SI mgesema tu mmebadilisha jina.
Una nunua kitu alafu kinabaki kwa mwenye nacho!
 
Utaratibu wa CAF timu yoyote inayoshiriki mashindano Yao lazima imiliki timu ya wanawake ya Soka. Sio kweli singida imeuzwa Bali ni kamchezo ka kuhalalisha ushiriki wao wa mashindano ya CAF
Nilivyofuatilia. CAF wametoa machaguo mawili hivyo kuchagua moja.

Ama timu shiriki kuwa na timu yake ya wanawake au timu shiriki kuingia makubaliano na timu yoyote ya wanawake.

Hao SBS wana mambo yao tu, wanajua wao.

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
CAF walizipa timu zisizo na timu za wanawake option ya kuingia makubaliano na timu nyingine ya wanawake ili kukidhi vigezo vyao. Nadhani hilo ndiyo limefanyika hapa.

Hata AZAM siku yoyote tutasikia wamenunua timu ya wanawake maana mchakato wa kuanzisha timu from scratch ni mrefu zaidi.
Kwahiyo kulikuwa hakuna namna ya kuingia makubaliano bika kununua timu nzima?

Kwahiyo mashindano yakiisha SBS itarudi?

Nafikiri kuna tofauti kati ya "Kununua" na "Kuingia Makubaliano" ukizingatia CAF walitoa option mbili zote

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
CAF walizipa timu zisizo na timu za wanawake option ya kuingia makubaliano na timu nyingine ya wanawake ili kukidhi vigezo vyao. Nadhani hilo ndiyo limefanyika hapa.

Hata AZAM siku yoyote tutasikia wamenunua timu ya wanawake maana mchakato wa kuanzisha timu from scratch ni mrefu zaidi.
hujui? azam wameshanunua timu ya wanawake kitmbo tu
 
Mwigulu amewapoteza maboya...
Rejea kigezo cha kubaki Singida...utagundua hesabu ilichakatwa
 
Isije ikawa ni kutafuta namna ya “kutakatisha”…. Nawaza tu[emoji3]
 
Singida wajanja wameona kwamba kwa sheria za CAF ili kushiriki mashindano ya caf lazima uwe na timu ya wanawake wameamua kuungana
Asante, sijui kwanini hao wasanii wasituambie ukweli wanajizungusha kama vile kutokuwa na timu ya wanawake ni dhambi...

Bahati mbaya Mwigulu atakuwa bado yupo hapo, na ataendeleza ushemeji wake na utopolo.
 
hivi huyu jamaa ana uwezo kulipa mishahara wachezaji, kwa hizo shule tu. nampongeza.
 
Timu ya soka iliyodaiwa inamilikiwa na Waziri wa Fedha Dr Mwigullu PhD Singida Big Stars Imeuzwa

Hata hovyo Dr Mwigullu PhD alishakanusha bungeni kwamba yeye hamiliki Timu yoyote ni mdau tu wa Michezo

Source Ayo tv
 
Hii nchi inabidi kuwa makini uza uza imezidi sana.......

Unaweza ukaamka asubuhi ukajikuta una mb*o plain bila p*mbu huku elfu hamsini wameisukumiza ndani ya chup na sms kwenye cm ikisema IYO ELFU HAMSIN ENDELEA KUITUMIA TUSHANUNUA HIZ MBUPU
Kweli wewe ni DUBULI HASA!!!😁😁
 
Uongozi wa Singida Big Stars umefanya maamuzi ya kuiuza timu hiyo kwa wamiliki wa Fountain Gate ambapo sasa timu hiyo imebadilishwa jina na kuwa “Singida Fountain Gate Footbal Club.”

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Singida Big Stars ambaye kwa sasa ni Mjumbe wa Bodi ya Singida Fountain Gate, John Kadutu amesema sababu ya kuiuza timu hiyo kwa Fountain Gate ni kutokana na changamoto mbalimbali za uendeshaji pamoja na nia ya kutaka kuipeleka mbali zaidi timu hiyo.

“Mnafahamu Fountain Gate wana timu nzuri ya Championship, wana timu nzuri ya vijana wa sekondari, ni mabingwa wa Afrika. Kwahiyo tukazungumza na watu ambao wanajua nini kinatakiwa kufanyika, usimtwishe mzigo mtu ambaye hajui shida zake,” amesema.

Aidha, Kadutu amesema moja kati ya masharti makubwa waliyowapa Fountain Gate ni kwa timu hiyo kuendelea kubaki mkoani Singida pamoja na kutumia jina la Singida ili kuwaenzi wote walioisapoti timu hiyo.

Naye, Rais wa Singida Fountain Gate, Japhet Makau amesema Fountain Gate imechukua asilimia 100 ya umiliki wa Singida Big Stars na Fountain Gate FC itaendelea kuwepo pia, huku akieleza kuwa hakuna tatizo lolote kwa timu hiyo kuendelea kubaki Singida kwani ilikuwa ndani ya mpango wao kufanya hivyo.
Unauza timu kwa asilimia mia halafu unaweka condition kwamba ibaki Singida.
 
Back
Top Bottom