TANZIA Fredrick Shoo (FRESHO) Mmiliki wa Kampuni Tanzu za FRESHO INVESTMENT LIMITED Afariki

TANZIA Fredrick Shoo (FRESHO) Mmiliki wa Kampuni Tanzu za FRESHO INVESTMENT LIMITED Afariki

Mkurugenzi wa Kampuni ya Fresho Investment Company (1999) Ltd ya Mjini Shinyanga Fredy Shoo maarufu Fresho amefariki dunia siku ya Jumatano Julai 28,2021 wakati akiendelea kupata matibabu jijini Dar es salaam.

Mwekezaji Mzawa Fredy Shoo ndiye mmiliki wa kiwanda cha kuchambulia pamba , kiwanda cha vifungashio na kiwanda cha kuchakata mafuta ya pamba pamoja na uwanja Mpya wa Kisasa uliopewa jina la ‘Fresho Complex’ uliopo katika eneo la Ugweto kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga,Pia ni kaka mkubwa wa Hillary Shoo mwenye viwanda vya Maji ya HILL,Hill Feeds na Kiwanda cha vifungashio cha Hill...
Na mdogo wao Harold Shoo maarufu HARSHO wa Moshi mwenye kiwanda cha Vifungashio Kwa Sadala Moshi kama HARSHO Packaging maarufu kwa Mifuko ya Super Sokoni.

Mungu Ailaze Mahali Pema Peponi Roho ya Marehemu Fresho. Amina

View attachment 1875353
Pichani: Aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati John Magufuli akikata Utepe kuzindua Kiwanda cha Vifungashio cha FRESHO Shinyanga mwaka 2017 kushoto kwake mwenye Jaketi la Bluu bahari ni Marehemu Fredrick Shoo.

View attachment 1875371

View attachment 1875372

View attachment 1875373

RIP big man.

One thing for sure is you've loudly left a lesson, one can be rich without bieng famous!

To the young thirsty bloods out there, aim for the money Not the fame!!!
 
Amewainua wadogo zake wote wamekua mabilionea,ndio familia za kichaga hupenda kunyanyuana
Nilioa uchagani sijutii kabisa. Mungu alinipa mke ambaye kwa umoja wetu tuliufuta umaskini wangu na ndugu zangu. Kuna siku nilisema hapa kuwa baada ya Mimi kuoa mchagga na rafiki zangu na ndugu wakashuhdia maisha yetu mazuri mno ya kuelewana na upendo basi ndugu zangu wa kuzaliwa tumbo Moja wote tumeoa wachagga. Ndugu wa ukoo wengi wameoa wachagga. Best friends zangu nao walioa wachagga. Kifupi sote tulioa wachagga tumebadili kila kitu kimaisha na kijijini tutokapo. Wazee wangu kabla ya kufariki walituita wakaomba kuwa sote tumuite mke wangu "Mama". Hivyo mke wangu haitwi Wifi wala shemeji. Na Mimi ninamuita mama na simkumbuki siku nimemuita kwa jina lake. Mungu akubariki mama Bahati

Endeleeni kuwabeza wachagga Ila niseme tu Wachagga ni taifa lingine kabisa. Tena kwa sasa vijiji uchagani utafikiri ni Miji mikubwa. Hata maisha ni kama mjini mpaka hata mapishi Yao.
 
Ndivyo ilivyo mkuu,halafu mwendazake alikuwa akiwapiga vita mno kutokana na majina yao ya ukoo,hakufahamu tu kuwa hawa ndiyo waliokuwa wakimsaidia kutimiza ndoto yake ya tanzania ya viwanda.
Ila watu muwe na aibu kwa uongo uliokithiri.angekuwa anawapiga vita angekubali kuwa mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa kiwanda, kama angekuwa anawapiga vita wazawa je angepa Bakhresa eneo kubwa la kulima miwa na kujenga kiwanda cha sukari huko Bagamoyo?unapokuwa muongo usiwe msahaulifu.
 
Back
Top Bottom