Asprin
JF-Expert Member
- Mar 8, 2008
- 68,223
- 96,083
Basi sawa. Msalimie sana...Yuko njema pia[emoji2957]
Naamini hajapiga picha na mwendazake. Kama alipiga mwambie awahi chanjo
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Basi sawa. Msalimie sana...Yuko njema pia[emoji2957]
Alikua ni anti-mwendazake. Hana jema naye[emoji23]Basi sawa. Msalimie sana...
Naamini hajapiga picha na mwendazake. Kama alipiga mwambie awahi chanjo
Ah kumbe Van ana akili sana.Alikua ni anti-mwendazake. Hana jema naye[emoji23]
Hahaaaa nitamfikishia salamuAh kumbe Van ana akili sana.
Mwambie aungane nami kwenye kampeni ya kuifanya Chattle eapoti uwe uwanja wa ng'ombe kuotea jua ili wapate vitamin D
Mkurugenzi wa Kampuni ya Fresho Investment Company (1999) Ltd ya Mjini Shinyanga Fredy Shoo maarufu Fresho amefariki dunia siku ya Jumatano Julai 28,2021 wakati akiendelea kupata matibabu jijini Dar es salaam.
Mwekezaji Mzawa Fredy Shoo ndiye mmiliki wa kiwanda cha kuchambulia pamba , kiwanda cha vifungashio na kiwanda cha kuchakata mafuta ya pamba pamoja na uwanja Mpya wa Kisasa uliopewa jina la ‘Fresho Complex’ uliopo katika eneo la Ugweto kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga,Pia ni kaka mkubwa wa Hillary Shoo mwenye viwanda vya Maji ya HILL,Hill Feeds na Kiwanda cha vifungashio cha Hill...
Na mdogo wao Harold Shoo maarufu HARSHO wa Moshi mwenye kiwanda cha Vifungashio Kwa Sadala Moshi kama HARSHO Packaging maarufu kwa Mifuko ya Super Sokoni.
Mungu Ailaze Mahali Pema Peponi Roho ya Marehemu Fresho. Amina
View attachment 1875353
Pichani: Aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati John Magufuli akikata Utepe kuzindua Kiwanda cha Vifungashio cha FRESHO Shinyanga mwaka 2017 kushoto kwake mwenye Jaketi la Bluu bahari ni Marehemu Fredrick Shoo.
View attachment 1875371
View attachment 1875372
View attachment 1875373
Marehemu kawabeba ndgu zake wote wamekua matajiri,alikua mtu poa sana
Frester ni mwehu mmoja hivi,huyu alikua na ukwasi wa kutosha,alikua na ginnery,kiwanda cha mifuko ya kubebea mazao,kiwanda cha mafuta ya kulaApumzike kwa Amani aisee
Hivi ndie mwenye mabas ya Frester eeeh...
Dah, So sad
Amewainua wadogo zake wote wamekua mabilionea,ndio familia za kichaga hupenda kunyanyuanaRIP
Kweli familia yao iko njema
Nilioa uchagani sijutii kabisa. Mungu alinipa mke ambaye kwa umoja wetu tuliufuta umaskini wangu na ndugu zangu. Kuna siku nilisema hapa kuwa baada ya Mimi kuoa mchagga na rafiki zangu na ndugu wakashuhdia maisha yetu mazuri mno ya kuelewana na upendo basi ndugu zangu wa kuzaliwa tumbo Moja wote tumeoa wachagga. Ndugu wa ukoo wengi wameoa wachagga. Best friends zangu nao walioa wachagga. Kifupi sote tulioa wachagga tumebadili kila kitu kimaisha na kijijini tutokapo. Wazee wangu kabla ya kufariki walituita wakaomba kuwa sote tumuite mke wangu "Mama". Hivyo mke wangu haitwi Wifi wala shemeji. Na Mimi ninamuita mama na simkumbuki siku nimemuita kwa jina lake. Mungu akubariki mama BahatiAmewainua wadogo zake wote wamekua mabilionea,ndio familia za kichaga hupenda kunyanyuana
Ila watu muwe na aibu kwa uongo uliokithiri.angekuwa anawapiga vita angekubali kuwa mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa kiwanda, kama angekuwa anawapiga vita wazawa je angepa Bakhresa eneo kubwa la kulima miwa na kujenga kiwanda cha sukari huko Bagamoyo?unapokuwa muongo usiwe msahaulifu.Ndivyo ilivyo mkuu,halafu mwendazake alikuwa akiwapiga vita mno kutokana na majina yao ya ukoo,hakufahamu tu kuwa hawa ndiyo waliokuwa wakimsaidia kutimiza ndoto yake ya tanzania ya viwanda.
Uongo unakusaidia nini? Fred was a friend to Magu hata kabla ya Urais wa Magu..Ndivyo ilivyo mkuu,halafu mwendazake alikuwa akiwapiga vita mno kutokana na majina yao ya ukoo,hakufahamu tu kuwa hawa ndiyo waliokuwa wakimsaidia kutimiza ndoto yake ya tanzania ya viwanda.
Basi wamefanana majina..au mwenye Frester atakuwa ukoo mmoja na marehemu.Frester ni mwehu mmoja hivi,huyu alikua na ukwasi wa kutosha,alikua na ginnery,kiwanda cha mifuko ya kubebea mazao,kiwanda cha mafuta ya kula