Fredrick Sumaye mbona yeye haonekani na hasikiki au kapigwa ban ya Jumla?

Fredrick Sumaye mbona yeye haonekani na hasikiki au kapigwa ban ya Jumla?

Ile kuhamia Chadema walimuona msaliti,wakaondoa kinga.Alipoonja joto la jiwe,walianza kumuandama kuhusi umilikaji wa ardhi huko Morogoro.

Hata kule alipokuwa amehamia ikafika muda akataka kugombea kiti cha Mwenyekiti ndipo mwenye chama chake alipomwambia sumu haionjwi.
CHadema mbowe alifanya yale kwa maagizo kutoka ccm ilu kumkata nguvu Sumaye.

Mbona Wasira alihama na sasa ndiye makamu mwenyekiti wa ccm taifa?

Au huu usaliti una viwango vyake?
 
Ukiona MTU ana kichwa kidogo au mviringo ujue anakuwa poor Cognitive ability .

Kwahiyo yeye kuwa PM hakikuwa Kazi ngumu .

Ila ukweli unajulikana kuwa jamaa chenga
Duh kweli mbaomfahamu mpi. Weka maelezo na sisi tumfahamu zaidi.
 
Hana cha kushauri kawa PM kwakuwa alikuwa analipa fadhila
Okay, fadhili alikuwa analipwa au analipa?

Alikuwa ana mlipa nani hizo fadhila na kwanini?

Hiyo nafasi alipendekezwa na Rais Mkapa mara mbili!

Huyu mtu alikuwa PM kulipa fadhila kwa nani?
 
Okay, fadhili alikuwa analipwa au analipa?

Alikuwa ana mlipa nani hizo fadhila na kwanini?

Hiyo nafasi alipendekezwa na Rais Mkapa mara mbili!

Huyu mtu alikuwa PM kulipa fadhila kwa nani?
MKAPA unajua serikali yake ilitegemea mifumo na sio one man show.
 
Huko ccm mbona kina Sofia Simba, Nchimbi, Adam Kimbisa waliwahi kuimba wana imani na Lowasa lakini walisamehewa yeye alikosea wapi?

Au kwenda CHADEMA ilikuwa kosa?

Na Mbona Lowassa alirudishwa ccm na kafa akiwa mwana ccm?
Sophia Simba unamwonaga wapi, Sumaye alishaharibu haaminiki tena
 
Fredrick Sumaye alikuwa waziri mkuu kwa miaka 10 lakini sioni kama ccm au nje ya ccm anaongelewa kabisa.

Alikosea wapi huyu mtanganyika mwenzetu?

Mkapa anapewa sifa lukuki lakini yeye aliyekuwa waziri mkuu kwa vipindi viwili vya uongozi wa Mkapa hana hata moja zuri alilolifanyia taifa hili?

Tangu atoke chadema hasikiki kabisa, au alipigwa ban ya jumla huko ccm?

Pinda anaonekana sana, lakini huyu Sumaye utadhani kahama nchi au yuko kizuizini?
Hajapigwa ban ila aliambiwa akiongea atanyang'anywa staiki zake zote .hii ni baada ya kumwenda cdm aliporudi alipewa masharti hayo
 
Pinda mfumo.

Si walisema ukishakatwa mkia hata ukirudi unakuwa tofauti na wenzio.

UMri umeenda pia , ameamua kujipumzisha nje ya siasa.
Kimsingi hakuwahi kuelewana na Kikwete, Pinda alikuwa waziri mkuu wa Kikwete kwa miaka 8, Kikwete sahivi ni mshauri mkuu wa mama, Sumaye hawezi kuwa pamoja na hilo kundi. Bila JK Samia hawezi kujiamini
 
Sophia Simba unamwonaga wapi, Sumaye alishaharibu haaminiki tena
Sofia Simba alikuwa mbunge wa kuteuliwa yani viti maalumu hakuwa wa kuoneka popote.

Mbunge wa kupewa na mbu ge wa kychaguliwa hawalinganishwi.

Sumaye alikywa Mbunge wa jimbo na Hanang, na waziri mkuu kwa vipindi viwili.

Huwezi kuwafananisha hao watu wawili.
 
Mifumo ikiwa imara hata ukiwa kilaza unaweza kuwa PM mzuri kwakuwa unakuwa unatembea na mfumo
Mifumo iliharibika lini sasa?

Huyu jamaa mnamnyima anachostahili.

Mkapa kamteua mara mbili, au mkapa naye alikywa kilaza?
 
Hajapigwa ban ila aliambiwa akiongea atanyang'anywa staiki zake zote .hii ni baada ya kumwenda cdm aliporudi alipewa masharti hayo
Wasira alipitoka nncr yeye alikuwa huru kufanya chochote, basi kweli mtandao wananguvu.

They can make you or destroy you.
 
Kimsingi hakuwahi kuelewana na Kikwete, Pinda alikuwa waziri mkuu wa Kikwete kwa miaka 8, Kikwete sahivi ni mshauri mkuu wa mama, Sumaye hawezi kuwa pamoja na hilo kundi. Bila JK Samia hawezi kujiamini
Pinda alikuwa waziri wa kikwete hivyo ni mwana mtandao naye?
 
Back
Top Bottom