Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Mheshimiwa Freeman Mbowe amekamatwa na Jeshi la Polisi katika mapori ya HALUNGU akiwa njiani anaelekea Mbozi baada ya kutoka Mlowo ambapo mkutano wale ulizuiwa na Jeshi la Polisi kwa Kutawanya Watu kwa mabomu ya machozi
Magari yameharibiwa kwa kuvunjwa Vioo,Watu waliokuwa katika msafara wa Mbowe wamepigwa vibaya mno,wamepoteza simu na fedha.
Polisi wamempakia Mheshimiwa Mbowe katika Defender na Kutoweka naye pasipo Julikana.
Viongozi wengine waandamizi wamekamatwa na Kupakiwa katika gari tofauti na ile iliyombeba Mheshimiwa Freeman Mbowe.
Pia soma
-
LGE2024 - Polisi watawanya Mkutano wa Mbowe kwa Mabomu. Kosa kaingilia ratiba ya ACT-Wazalendo
View attachment 3158721