Freeman Mbowe alia ubaguzi katika mfumo wa elimu Tanzania

Kwe
Mbowe hataki kukuza lugha ya Kiswahili ili iwe lugha ya kitaaluma?
Mbona wachina, Wajapan, Warusi, Waswede, Wajerumani, wafaransa wanatumia lugha zao kufundishia watoto wao kwa nini kiswahili kisiweze?
Kwenye soko la dunia sisi utatfananinisha na wachina? Ata wahindi na ukubwa wao wanatumia english! Kiswahili hakiwezi kutusukuma mbele kitaaluma na kikitumika kitaaluma sio Kama ndo kitakuwa dhaifu
 
Hapo sasa tunasema,kwa kimombo 'until then' !
 
Labda chama kingene ila mbowe na ubaguzi was kikanda
 
Basi kiswahili kitumike kufundishia Awali Mpk Chuo kikuu na kusiwe na English medium ndani ya Nchi Ili tukuze kiswahili,ila Kwa hali ya Sasa Bora tuwe na English mwanzo mwisho
Mbona kinatumika tu kwenye kufundishia na mtu anaelewa vizuri
 
Uongo mtupu
 
Mkuu kuna ka msemo kanasema,,'kama elimu ni gharama,jaribu ujinga'.. CCM miaka 60 baadae baada ya uhuru ilichagua UJINGA!
 
Point
 
Mkuu, makabils 120+ Kiswahili siyo lugha mama. Ni lugha ya pili.
 
Mbowe atuambie alienda kufanya nini Ikulu baada kutoka jela bila hata kufika nyumban kwake?

Asiudanganye ulimweng na wananchi Chadema sasa haina tena mpango wa kushika dola baada ya manusura

Chadema walikubali kuongea na mama mchana kweupe, biashara ishamaliza
 
Huko mbeleni wanapofika vyuoni mwenye akili zinajionyesha bila kujali alisoma english media au kiswahili media
 
Akihutubia mamia ya wafuasi wake na wananchi waliojitokeza kumpokea katika viwanja vya Bomang’ombe, Mbowe alisema elimu inayotolewa kwa sasa haimjengi Mtanzania kuingia katika soko la ajira kutokana na mfumo wake ulivyo na kwamba i
Wanaomshauri Mbowe, wawe makini sana.

Tatizo siyo kujua lugha ya kiingereza.
Tatizo ni hili hapa lililoelezwa katika mstari huo hapo juu.

Awe mwangalifu sana na jambo hili, kwa sababu inaonekana anachanganya mambo hapa.

Tatizo siyo lugha inayotumika katika kufundisha, ni ubovu wa mfumo wa elimu kiujumla.

Natumaini CHADEMA hili jambo wataliwekea maanani zaidi na kulifanyia uchambuzi ulio makini, kuliko kuja na matamko ya kijumla jumla kama haya yanayosemekana yamesemwa na mwenyekiti wa chama hicho.

Itasikitisha sana kama CHADEMA watakuwa wanatafuta umaarufu kwa wananchi kwa kugusia matatizo makubwa kama kuporomoka kwa elimu yetu bila ya kuelewa tatizo ni nini na bila kuwa na ufumbuzi sahihi wa tatizo lenyewe.

Lazima wawe waangalifu sana kwa mambo kama haya.
 

kwa kiasi kikubwa sisi ndio tunauhitaji kwa sasa, kukomaa na kiswahili itatutesa sana na tutahitaji karne nyingi sana ili tuweze kusurvive, na itawezekana tu kama tutakuwa na uwezo wa kiteknolojia na kiuchumi hapo watu wengi watatuhitaji kuliko tunavyowahitaji...Kwa sasa tunaihitaji sana dunia inayotumia kiingereza kwa kiasi kikubwa kuliko yenyewe kutuhitaji sisi tunaoongea kiswahili....

Kwasasa Kiingereza kitiliwe mkazo jamii ijifunze iweze kuchangamana na dunia ili watu wetu waweze kuishi, kuliko sasa ambapo dunia kwa kiasi kikubwa inahitaji watu wazungumze kiingereza na ukiwa haujua automatically unakosa soko...

Mataifa mengi yanayotumia lugha zao, historically wana maguvu kiuchumi na wanajitegemea kwa kiasi kikubwa na program hizi walizianza zamani kabla dunia haijafika huku..
 
Kumbe kampeni za uchaguzi mkuu zimeanza eh?

anyway; amehama ktk kampeni ya katiba amehamia ktk kiswahili🤗
 
Totally WRONG!

Sijawahi kusikia Ujerumani au Ufaransa wakiwafundisha watoto wao kwa lugha ya Kiingereza. Wala waChina waliotapakaa dunia nzima sasa hivi hawajifunzi masomo yao kwa lugha ya Kiingereza.



Hapa ndipo Mbowe na chama chake wanapolikoroga, wanapodhani Kenya ndio mfano wa kupigia chepuo kwa mambo mazuri yaliyopo huko!

Nina hofu sana juu ya chama hiki kuifanya Tanzania kuwa tegemezi wa nchi hiyo jirani kwa kila kitu. This is a very big put off about this political party.
 
80% ya maarifa ya ulimwengu yameandikwa kwa lugha ya kiingereza ....st kayumba maarifa km ya kwenye kitabu rich dad poor dad hawezi kuyaelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…