Freeman Mbowe apendekezwa mwanasiasa bora wa Upinzani


Kimbunga unachanganya mambo kwa malengo unayoyajua mwenyewe..

Hapa hatafutwi mgombea wa Urais.

Isitoshe wewe ama Molemo si wasemaji wa Ukawa.
 
Last edited by a moderator:

- I agree with this 100%,

Le Mutuz
 
Mboe ni kamanda kweli amejiunga na upinzani toka kuanzishwa vyama vingi mpaka leo ajawai kubadilika
 
Mboe ni kamanda kweli amejiunga na upinzani toka kuanzishwa vyama vingi mpaka leo ajawai kubadilika

Ni kweli Kamanda.Hajawahi kusaliti mageuzi hata mara moja.
 
Mbowe anahitaji kila sifa ya kuweza kuwa mbunifu hadi kufikisha CHADEMA hapa kilipofikia.Wakati mwingine amekuwa akitumia juhudi zake binafsi ili kuhakikisha mikakati ya chama inafanikiwa.Kwa kweli viva Mh.Mbowe kwa juhudi zako hizo.
Watu wanazungumzia kuhusu elimu,hata hao waliosoma sana,wameweza kulifanyia taifa kitu gani?,acheni kuleta hoja zisizo na msingi.
 
Lazima ikumbukwe katika historia ya Upinzani vyama vilivyoibuka kama vyma vyenye nguvu baada ya uchaguzi mkuu havikuweza kudumu vilisambaratika baada ya uchaguzi mkuu tu, Mbowe ameisimamia Chadema imepita katika vipindi vigumu sana na hatari, kwani huyu Kiongozi asitunukiwe nishani? anastahili kabisa kama kiongozi wa Upinzani nchini.
 

Mwalimu nyerere alitabiri chadema itachua nchi kwa kuwa ni chama makini
 
CDM nichaukweli...... Hata Mbowe akileta mamboa ya ajabu anapigwa chini maana cdm ni kipenzi cha watanzania (wafanyakazi na masikini).
Nakwambia hata yeye mwenyewe anafaham kua hatuna utani.
 

Utata kifipi tuambie ulitaka afikishe chama wapi zaidi ya hapa kilipo ameweza kupambana na mkakati wa maccm kua cdm amefaulu kwenye bunge alizima mpango wa maccm ambao ilishafanikiwa wa kumwambia mwizi achague hukumu
Atakayo hukumiwa na mapendekezo ya Change yalisha pita na Zitto alishatoa baraka yapite kwenye hoja zote kamanda Mbowe alipo simama mwishoni mafisadi wakiwa wamejipanga kushangilia alipotoa hoja zito zakupinga walichokuwa wanakifanya uongozi wa bunge na mawaziri walichanganyikiwa wakaenda kumbeleza akubali ikashindika tukubali tu kwamba nikiongozi mwenye kitu cha ziada tatizo letu mtu akifa ndiyo tunatoa sifa zake
 
WAKATI Prof. Kitila Mkumbo, Zitto Kabwe na Samson Mwigamba, wakijiitayarisha katika kile walichokuja kukiita baadaye, "Mkakati wa Mabadiliko" ndani ya Chadema, waliibuka na hoja moja kubwa.

Kwamba, Freeman Mbowe, mwenyekiti wa taifa wa Chadema hataki kuwapo kwa demokrasia ndani ya chama hicho. Wakadai Mbowe ni mbinafsi, dikteta na anakitumia chama hicho kwa manufaa yake binafsi.

Mkakati wa mabadiliko uliokuja na majina bandia ya M1 M 2 na M3, uliishia kwa kufukuzwa kutoka ndani ya chama hicho, Prof. Kitila, Zitto na Mwigamba.

Leo hii ni mwaka mmoja tangu watatu hao wafukuzwe Chadema na kujiunga na chama kipya cha ACT-Tanzania.

Ukipima kile walichokuwa wanakihubiri na hiki kinachotokea sasa katika ACT, utaweza kubaini kuwa Mbowe, pamoja na kuwa na elimu ndogo ukiliganisha na Zitto na Kitila, lakini amewapiku katika busara, hekima, maarifa na maono ya kuendesha chama cha siasa.

Kwa mfano, wakati Kitila, Zitto na Mwigamba, wanatuhimuwa kupanga njama za mapinduzi ndani ya chama kinyume cha taratibu, Mbowe "asiye na elimu" alitumia kikao halali cha chama – Kamati Kuu (CC) – kuendesha kesi na kutoa hukumu.

Watuhumiwa wote walipewa nafasi ya kuhojiwa. Baadaye mashitaka yakaandaliwa. Wahusika wakapewa siku 14 kuwasilisha utetezi.

Wote watatu wakaitwa katika kikao kingine cha CC kufafanua utetezi wao. Kamati Kuu ikateuwa jopo la wanasheria kuwahoji wahusika. Utetezi wote ukapimwa. Hatimaye hukumu ikatoka.

Ni tofauti na wanavyofanya wao ndani ya ACT. Wametumia kikao batiri cha Kamati Kuu kuwafukuza viongozi. Watuhumiwa hawakupewa mashitaka. Hawakupewa nafasi ya kujitetea.

Kama hiyo haitoshi, waliodai kuwafukuza, ndiyo walewale ambao waliendesha kikao cha kuwafukuza Prof. Kitila, Mwigamba na "Zitto wao."

Hawa ndiyo waliokuwa wanadai mabadiliko ndani Chadema! Hakika, wameonyesha kufeli, tena kwa kiwango kikubwa.

Mbowe aliyetuhumiwa dikteta, ameonyesha demokrasia na waliojiita wanademokrasia, ndiyo wamegeuka madikteta. Hongera Mbowe!
 
Do you really understand the term 'vision' or 'visionary leader'?Your heading doesn't relate to the content
 
nafikiri zitto hakuchaguliwa kwasababu hana chama,
zitto anakuwa mwanasiasa bora wa kipindi chote
 
Mmmh apewe nishani ya mwanasiasa bora YA upinzani kwa lipi haswa? Hilo la kumfanyia zengwe zitto kabwe ili asiwe mwenyekiti chadema na kuhakikisha anamfukuza kwenye chama?
 
Mbowe akiwa rais wa nchi hii naihama,labda lipumba au slaa au lissu ndani ya ukawa ila sio mbowe.
acha kiherehere amekwambia anautaka urais.By the way kama Mungu kapanga siku moja aje kuwa Rais atakuwa tu
 
CCM aishindi kwa sababu tu ya kupendwa sana, bali imejiweka kama chama cha kuaminiwa kwa mambo mengi ya kitaifa ambapo wengine wanajiaminisha tofauti kwenye maswala hayo kwa hisia kuliko uhalisia; muungano likiwa moja wapo.

Sasa usishangae miaka zaidi ya 20 ya vyama vya upinzani 20% ya chaguzi kupata bado ni kasheshe, wewe unaweza kuona labda CCM inapendwa sana, mimi naona kama vile watanzania bado wanakiamini chama sio mtu kama msimamizi wa taifa lao.

Sasa sijui watanzania wataawamini vipi watu wasiotaka muungano, watu wasio gusia kero zao kila wakipita ni ufisadi tu. Binafsi naona kama ni swala la kukosa tactic za kugusa hisia haswa za jamii ndio maana vijana wanaweza tembea kutoka geita mpaka dar kutaka kumuona raisi huku wamevaa bendera ya Tanzania na mkononi wameshika ya Tanganyika kama sio kuchanganyikiwa ni nini huko kutokana na confusion wanazopewa na CDM.

Mbowe is a good commander and disciplinarian sikatai ni kitu muhimu kwa CDM kwa sasa na bado ana nafasi kubwa sana kwenye kukijenga kutokana na yale tunayoyasoma kuhusu vyama vingine kuvurugika. Lakini lazima akubali he is not an idea man, hapo anahitaji kuwapa wengine uwanja.
 
Ni ukweli ulio wazi Mh. Mbowe kwa sasa ni regulator wa joto la siasa nchini.Ndie mtu anayeweza "kukinukisha" au "kukipoza" mda wowote iwe ni ndani ama nje ya bunge!

CCM wanapojadili ajenda ya hali ya siasa nchini kila mchangiaji ni lazima aitaje CHADEMA.Misimamo na hoja zake za dhati zimezaa matunda kwa kasi sana.

Vijana walianza kuhamasika,wakafata wazee,leo hii wamama zetu wanaimba CHADEMA!wanaogopa na kuona aibu kushabikia CCM.

Tumeona mziki wa CHADEMA uchaguzi serikali za mitaa!Mbowe amewatia ujasiri sana watu,wanakosoa waziwazi.Leo hii wafanyabiashara hawaoni shida kupandisha bendera ya Makamanda ofisini kwake.

Kwa kuwa Mh.Mbowe umekuwa kipenzi cha watanzania,Kwa kuwa Mh.Mbowe umekuwa mmoja wa wenyeviti waliona haja ya kuunganisha nguvu kisiasa bila kujali itikadi zao.

Naomba ukubali kuwa wewe ndiye KAKA WA TAIFA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…