Freeman Mbowe apendekezwa mwanasiasa bora wa Upinzani

Freeman Mbowe apendekezwa mwanasiasa bora wa Upinzani

Kimbunga ni wewe ama umeandikiwa?

Molemo kawa hao Maprofessor wanaomuunga mkono? Dhambi ya Molemo ni nini?

Molemo ni sauti iletayo habari tu..
Mkuu Molemo maprofessor wako wapi hapo? Umesema professor Mpangala na Dr. Emmanuel Makaidi kisha una conclude kwamba ni maprofessor!
Haya tuseme ameungwa mkono na maprofessor kwamba ndiye kiongozi bora wa upinzani kuliko viongozi wote wa upinzani na tunasema vyama vikubwa vitatu vimeungana chini ya UKAWA na tunategemea vyama hivyo visimamishe mgombea mmoja. Huku tukifahamu kwamba Mbowe ndiye kiongozi bora kuliko wote, kwa nini tuhangaike kutafuta mwingine ambaye si bora wakati tunaye aliye bora?
 
Last edited by a moderator:
Kamanda wa anga, Mbowe anastahili pongezi kwa kukijenga chama chetu pamoja na kuwaunganisha opposition chini ya mwavuli wa UKAWA.Hii ndio sababu hata magamba hawapendi kulisikia jina la Mbowe kwani amekuwa mwiba kwao kwa muda mrefu. Hongera sana kamanda Mbowe.
 
Mkuu Molemo maprofessor wako wapi hapo? Umesema professor Mpangala na Dr. Emmanuel Makaidi kisha una conclude kwamba ni maprofessor!
Haya tuseme ameungwa mkono na maprofessor kwamba ndiye kiongozi bora wa upinzani kuliko viongozi wote wa upinzani na tunasema vyama vikubwa vitatu vimeungana chini ya UKAWA na tunategemea vyama hivyo visimamishe mgombea mmoja. Huku tukifahamu kwamba Mbowe ndiye kiongozi bora kuliko wote, kwa nini tuhangaike kutafuta mwingine ambaye si bora wakati tunaye aliye bora?

mkuu, usivuke mto kabla hujaufikia. utaratibu wa kutafuta mgombea ndani ya UKAWA haujafika, muda ukifika jina lake litapendekezwa. sisi sio kama kama magamba wanaofanya mambo yao kama mapanya.
 
Last edited by a moderator:
Kwa wapinga ufisadi ruswa na kula mali ya umma lazima waseme chadema na ukawa inatosha
 
Ukitaka kuona uthamani na ushupavu wa Mbowe hauhitaji kusikiliza maprofesa ndio uamini but just look around uone kizaazaa kilichopo ACT sasa, angalia jinsi ACT wanaumana ndo utaelewa kwanin wanamageuzi wote wanamuheshimu Mbowe.


Long live Mbowe.
 
maadam sisi kina gogo la shamba tulishamkubali Mbowe kama mtu mwenye busara ya hali ya juu ndivyo itakavyokuwa maana kazi yetu sisi ni kusema yale yaliyo ya kweli
 
KAMA MAKENGEZA NDIO SIFA KUU BASI USIWASAHAU WAFUATAO..
EDWIN MTEI
BOB MAKANI
hahaaaaaaaa yaani nyie lazima muongozwe na wenye makengeza!!!!!!!!!!!!!!!!!!
nawadharaaaaaaauuuuuuuu
 
Wanajamvi, dunia hii huwa ina binadamu wachache wenye sifa za kipekee. Leo naomba nimuongelee Freeman Mbowe. Huyu jamaa anatokea kwenye Familia yenye pesa, inasemekana ni mali za urithi. Wanamiliki Hotel, lakini pia ukumbi wa Bilcanas, tukumbuke enzi hizo Bilcanas ilikuwa inaingiza pesa nyingi kwa mwezi, sijui kwa sasa. Lakini pamoja kwamba huyu jamaa tayari ana maisha bora, alihamua kujitoa Muhanga kwa ajili ya kuwapigania wanyonge angalau nao wapate kidogo.

Mheshimiwa huyu pamoja na pesa zake lakini amekumbana na Mabomu, Risasi, matusi, kuwekwa Rumande, vitisho, kukatishwa tamaa lakini hayo yote hakuyajali, yeye ameendelea kupaza sauti kwa ajili ya wanyonge. Mbowe ni special na ni unique. Mimi baada ya Nyerere huyu ndie Role Model namba mbili.

Ni matajiri wangapi wenye moyo kama wa Mbowe?, au wanaamvi mnasemaje?
 
Zote hizo kodi za wananchi , waliiba kipindi baba mkwe yuko B.O.T
 
Kamanda anastahili kupewa heshima hiyo kwa uongozi wake wa siasa za tz hasa akiwa kama kiongozi wa upinzani
 
Kitu ambacho kama utakuwa mkweli uwezi kukikataa kutoka kwa bwana Mbowe ni leader by nature. You got to awe his commanding abilities kwa sasa in my perspective ni second to none katika wanasiasa wa Tanzania wa pande zote. Tatizo lake maarifa yake na uwezo wa kuchanganua mambo ndio utata if only angejenga timu imara ya kumshauri angeipeleka CDM mbali sana.
 
Back
Top Bottom