Freeman Mbowe atangaza kufanya Makongamano ya Katiba mpya nchi nzima, la Mwanza kufanyika wiki hii

Ni katiba mpya ya nchi, kwa nini Mbowe mwenyekiti wa chama cha siasa ndiye aidhinishe makongamano? Au makongamano ya katiba mpya ni ya CHADEMA tu?
 
Nikajua unamsemea Aboubakar Shekau wa Nigeria
 
Mjue tu kuna delta variant, na Mbowe ameshachanjwa sasa nyie nendeni mkakongamane yeye anajua pa kujitibia[emoji1787][emoji1732][emoji205]
Si huwa mnasema hakuna corona na kama ipo tuonyeshe jirani hata mmoja aliyekufa kwa covid
 
Ila we jamaa unapenda kulambisha Mambo Moto daah, halaf eti mtemi isike cjui nn cjui
 

Jidanganyeni. Uzuri ni kuwa hata huwa hamkumbuki mliwahi kusema nini.



Vyawa wa Mama na wa legacy kwenye katiba mpya lao moja.

Wa legacy wao ni wahanga wa ujinga na brainwashing. Wamebakia kuwa misukule kamili ya yule bwana akiwa hai au mfu.

Wa Mama wao wako kimaslahi zaidi.

Au nasema uongo ndugu zangu.
 

Chawa wa Mama kwenye ubora wako.

Tatizo hoja, nondo, au points zenu ni zipi za kuwapinga wengine kudai katiba mpya?

Kwanini mnakereka mno mkisikia katiba mpya? Angalau mngekuwa mna address hilo.

Kwani nyie kama hamna haja nayo kwanini kuwanyanyapaa wanaoitaka?

Hivi hata nyie wenyewe hamjishangai?
 
Chadema tuhurumieni wafuasi wenu kwa kweli.

Punde tu mama ametoka kutufikiria punguzo la tozo za kizalendo ghafla Mbowe anawaambia polisi atafanya mikutano nchi nzima wakitaka wamkamate.

Yaani mwenyekiti wa Chadema anatangaza kuvunja sheria hadharani kisha siye na akina Mrangi tutaombwa michango ya wakili wa kumtetea.

Ufipa acheni hizo bhana.

Nawasalimu kwa jina la JMT!
 
Mkuu hoja zetu ni zilezile:

1)Serikali 2 ndio UTULIVU wa hivi ilivyo Tanzania(wale wanasiasa wa G55 wangetupeleka siko).

2)Katiba hata iwe nzuri kiwango cha kusifiwa na malaika....wanasiasa wanabaki kuwa ni kundi lisiloridhika(kuridhika kwao ni kuwepo madarakani tu).Hapa wapiga nzumari za katiba mpya ni haohao wanasiasa tu....tena KUNDI LA UPINZANI!!!

3)Afrika ya kusini ina katiba inayoweza mpaka kumshtaki RAIS...Ila bado haikuzuia VURUGU na MACHAFUKO YA KIJINGA baada ya Rais mstaafu kushtakiwa.

4)Ukipunguza NGUVU ZA MADARAKA ZA RAIS umeyatafuta matatizo kwetu WAAFRIKA.....kupinduana na Kusababisha kukosekana UTULIVU wa nchi kutakuwa kila uchao.Hilo pia limeonekana kule HAITI....katiba yao haimpi Rais wao hayo MADARAKA MAKUBWA.....
 
 
CHADEMA haikuhusu wewe mtafute Madelu muongee nae tukutane DK 45 leo usiku kama kitarushwa
 
Kwa hiyo Tanzania mnaishi kwa hisani ya Rais?
 
Reactions: BAK
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…