Uchaguzi 2020 Freeman Mbowe atia nia kugombea urais kupitia CHADEMA

Hivi kuna chama cha upinzani cha kuishinda CCM kwa sasa? Kwa mikakati ipi hasa? Mwaka 2015 walibadilishia gia angani, wakakaribisha mafisadi ndani ya umoja wao wa UKAWA. Wananchi waliwaunga mkono sana mwaka ule, ila wamewavunja moyo waliowaunga mkono kwa kufanya maamuzi ambayo hayakuwa na tija. Waache tamaa na ubinafsi

Wakae chini, waangalie walipojikwaa na kupanga mikakati thabiti ya muda mfupi na mrefu ya kushinda uchaguzi. Kukishinda chama kilicho na dola na ambacho kimekaa madarakani kwa miaka mingi si jambo rahisi.
 
Huyu aligaragazwa na JK 2005 ndio atamuweza JPM kweli?!

Tupunguze utani wajameni!
Mbowe kajitosa geresha ili ionekane hata yeye anaweza kupigwa chini. Baada ya kutia aibu kwenye Uenyekiti. Mgombea wao tayari wanae.
 
Sasa hii ni demokrasia au Maigizo ya demokrasia?
 
Labda kwa vile anapigiwa kelele kwa kukandamiza demokrasia chamani,kaona azuge kugombea halafu ashindwe ili kuaminisha watu kuna demokrasia ndani ya chama!! Nadhani ndio mpango wa DJ huu
 
Najua katiba ya JMT inasema Rais lazima awe na degree angalau moja. Sasa Mh. Mbowe kasoma lini kupata hiyo sifa?
 
Nini DJ, kuna nchi tena ya ulaya, comedian alishika kiti cha urais. Nadhani bado ni rais hata sasa
 
Uwezekano wa ushindi wa upinzani dhidi ya Rais Magufuli ni mdogo sana (siwezi kuandika haupo kwa sababu lolote lawezekana kisiasa).
Hata hivyo, vyama vya upinzani lazima viweke wagombea wanaoweza kutoa changamoto kwa mustakabali wao.

Mbowe ni mpinzani anayeweza kutoa changamoto (siyo ushindi katika hali ya kawaida), na historia yake inaonesha hivyo.
 
Najua katiba ya JMT inasema rais lazima awe na degree angalau moja. Sasa Mh. Mbowe kasoma lini kupata hiyo sifa?
Kuna rais ana PhD ya kugushi. Ben Saanane alipigia kelele hiyo, badala ya kujibiwa hija yake, akapotezwa. Hakafu rais huyo eti ni mpambanaji wa wanaogushi vyeti! Ila Makonda kamsamehe! Hiyo ndio Tanzania
 
Hawezi kupitishwa. Hiyo ni kiki nyingine baada ya ile ya nyagi kubuma. Hapo anataka nyumbu wasahau kuwa yeye ni sultani na waamini kwamba chadema kuna demokrasia. Eti kwakuwa Mbowe kashindwa kwenye kinyang'anyiro cha kuteuliwa kugombea uraisi
 
Najua katiba ya JMT inasema rais lazima awe na degree angalau moja. Sasa Mh. Mbowe kasoma lini kupata hiyo sifa?
Sifa anayo ndio maana aligombea 2005 labda kama katiba ilifanyiwa marekebisho hayo baada ya mwaka huo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…