Jumbe Brown
JF-Expert Member
- Jun 23, 2020
- 12,077
- 12,786
🤣🤣🤣
Baada ya upekuzi wa Polisi kukamilika nyumbani Kwa M.Kiti Mbowe, tumepokea taarifa za kushtua na kushangaza kuwa Polisi wamemwambia kuwa ataunganishwa kwenye kesi ya Ugaidi na watuhumiwa walioko gereza mojawapo DSM.Tutaendelea kutoa taarifa za kina hapo baadaye.
View attachment 1862953
====
UPDATES;
=====
TAARIFA KWA UMMA
JESHI LA POLISI LAMTUHUMU MWENYEKITI WA CHAMA
MHE.FREEMAN MBOWE NA "MAKOSA YA UGAIDI"
Mwenyekiti wa Chama Taifa Mhe. Freeman Mbowe alifikishwa Dar es Salaam jana majira ya saa tatu usiku chini ya ulinzi wa Polisi , walimpeleka nyumbani kwake Mikocheni Kwa ajili ya kumfanyia upekuzi ambao ulichukua takribani saa mbili na nusu.
Baada ya upekuzi huo Polisi waliondoka na Kompyuta mpakato (Laptop) na Vishikwambi (tablets) za watoto wake, Kompyuta mpakato moja ya kwake na modem ya Internet Kwa ajili ya uchunguzi wao.
Leo majira ya saa Saba mchana Polisi walimfikisha Mhe. Freeman Mbowe Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano na kuchukua maelezo yake.
Polisi walitaka maelezo kutoka Kwa Mhe. Freeman Mbowe kuhusiana na kosa waliloliita 'KULA NJAMA ZA KUTENDA KOSA LA UGAIDI'
Baada ya maelezo hayo ya Polisi Mhe. Freeman Mbowe alitumia haki yake ya kisheria na aliamua kutokutoa maelezo yoyote Polisi kwa mujibu wa Sheria. Baada ya maelezo hayo Polisi wamemrejesha Mhe. Freeman Mbowe katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay ,Jijini Dar es Salaam.
Aidha , viongozi wengine waliokuwa wanashikiliwa Mkoani Mwanza wameendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi na baadhi yao walifanyiwa upekuzi nyumbani kwao na vyumba vya hotel ambako walikuwa wameshukia .
Waraka wa Mbowe kwa Watanzania
Mwenyekiti Taifa Mhe. Freeman Mbowe ametuma waraka kwa Watanzania kama ifuatavyo;
"Hatimaye madai ya Katiba Mpya yamenisababishia kesi ya ugaidi, nipo tayari kwa mashtaka ya kuchongwa siogopi. Ninaamini Dunia itaujua ukweli wa kile kinachoendelea Tanzania na kile tunachokipitia Watanzania. Lakini pia itajua ukweli juu ya makosa haya ya kuchongwa.
Natoa wito kwa watanzania kuendeleza mapambano, haki hutafutwa” Mhe.
Freeman Mbowe.”
Imetolewa leo Alhamisi tarehe 22 Julai, 2021.
John Mrema
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje.
=====
UPDATE:
View attachment 1863559
View attachment 1863560
Uchaa ujinga wewe bwna, tunataka evidence sio maneno tuu hayo, minyoo Hadi kichwan duuhUchaguzi upi ulimchagua magufuli? Mwananchi yupi? Kura zipi? Tume upi? Hakuna uchaguzi Tanzania kilichofanyika ni CCM kuulawiti kuubaka kuunajisi uchaguzi mkuu kwa njia haramu za kishetani tu
Hahhaahhahaahahaha.Mungu hana mtumishi mwendawazimu, Mungu kaagiza mzitii mamlaka zilizopo maana hakuna mamlaka isotoka kwake, nani mtumishi wa Mungu kati yangu mie nilolishika na kulifuata agizo lake na msu.kule ka wewe usoelewa hata nini unafanya?..[emoji57]
Akitaka kuharibikiwa ni aende tu kinyume cha JPM, sisi the majority tulimchagua JPM na hulka yake na si kwamba hatukujua tunachagua mtu wa namna gani, hilo mnalifahamu vyema na ndo maana mkaanza kumwingiza mother mkenge ili achukiwe na wafuasi wa JPM ambao ndo the majority ya wapiga kura mkitegemea wapige kura za hasira 2025, mama kashtuka ngoja awanyooshe..[emoji4]
Naona kagoma kunyolewa sasa kashika yeye wembe anaanza kula vichwa kimoja kimojaKumbe hana tofauti na Mullah Omar
Ipo siku isiyojulikana. Muda wenu utafika tu na mtakiri kwa vinywa vyenu. Kwa sasa endeleeni kushupaza shingo tu!Mbowe akutwa na tuhuma za ugaidi za kuuwa viongozi wa serikali.
Wampeleke gereza la kisongo akakutane na Sabaya.
Itajulikana tu aliyemuuwa Magufuli
Ndiyo maana LISU alikuwa wa kwanza kusema Magufuli anaumwa na hatapona.
Kama alianguka akiwa amelewa konyagi alafu akatangaza amepigwa na wasiojulikana kwa nini nisiamini?
Tuliache jeshi letu la polisi lifanye kazi yake. Kuhusu ukweli na uongo utajulikana mbele ya safariKuna mzee mmoja nimekutana naye.. yaani ni CCM damu.
Huwa anafurahi sana viongozi au wafuasi wa Chadema wakikamatwa au kufungwa.. Kiufupi hapendi mfumo wa vyama vingi..
Ila leo mwenyewe kasema Polisi wamezidisha chumvi...
Wewe akili yako sio fupi tu. Imekaa mahali isipostahili kukaaHahaahahhahaahhahaahah. Sio Magufuli tena?? Ni Samia sasa sio??? Nyinyi watu akili zenu ni fupi.
Mwanzo mlisema Kikwete ndio worst president ever, then mkasema Magufuli is the worst president ever and now Mama Samia???
Tunawaangalia tu hahahahahahah
Kwa mujibu wa samia alisema Magufuli alikufa kwa ugonjwa wa moyo na amekuwa akisisitiza!!mnajidai hamjui?muulizeni lissu!