Freeman Mbowe atuhumiwa kwa Ugaidi na kupanga njama za Kuua Viongozi wa Serikali

Upelelezi wa kina na wa kitaalamu ufanyike maana huu mtandao wa kigaidi ambao kiongozi wake ni Mbowe ulisambaa kila eneo la nchi yetu, hivyo tunaomba upelelezi wa kitaalamu ufanyike na unase mtandao wote ulio kuwa ukiratibu shughuli za kigaidi kwa maelekezo ya Mbowe.
 
Bila shaka wewe ni naibu shetani. Hakuna mtu mwenye akili asiyejua hii sanaa. Watu kama wewe, waabudu shetani, wasiokuwa na hofu ya adhabu baada ya mauti yao, pale wataposimama mbele za Mungu, hata kama hawamtaki, hamuwezi kushindwa kutunga matukio na kutoa ushahidi wa uongo. Hata Yesu Kristo alitungiwa mashtaka na mashahidi wa uwongo. Hakuna jipya unalolifanya.

Unaweza kutuambia matukio gani ya ugaidi aliyoyafanya ama kuyaasisi Mheshimiwa Mbowe? Mwogopeni Mungu. Matumbo yenu ni mifuko ya funza. Maisha ni mafupi. Mungu anaowaona na anachukia hila zenu.

HAKI HUINUA TAIFA. NCHI YANGU INAMASUALAL MENGI YA KUJIVUNIA BADALA YA MIKAKATI HOVYO YA KUUMIZA WATU WASIO NA HATIKA KWA JINSI ISIYO HALALI. SHAURI LENU!
 
Mkuu kwani sukuma gang si walishakomesha na mama kwa mujibu wa Malisa
 
Mkuu kwani sukuma gang si walishakomesha na mama kwa mujibu wa Malisa

Kwa sasa mama wa kambo hana jinsi zaidi ya kuwaridhisha sukuma Gang baada ya kuanza kumchimba. Hayo ndio matatizo ya urais wa kurithi.
 
Kwa sasa mama wa kambo hana jinsi zaidi ya kuwaridhisha sukuma Gang baada ya kuanza kumchimba. Hayo ndio matatizo ya urais wa kurithi.
Urais wa kurith vipi wakati ana power yote na mnasema anatawala kwa katiba ambayo ina mpa nguvu kubwa sana rais? Kwamba anaweza kutamka lolote mpaka hao sukuma gang wakapoteana?
 
Hakika umeandika vizuri na kwa busara ya hali ya juu. CDM bado ni chama imara, ilq kinakosa agenda za kuungwa mkono kama ilivyokuwa miaka ya 2010s. Viongozi wa juu wa chama chao wanalazimika kutumia nguvu nyingi, pamoja na drama kurudisha attention yao kwenye jamii. The way wanafanya, watawala wanawaona kama tishio, hasa kwenye ustawi wa amani juu ya nchi, ukiona yaliyoyokea south Afrika, serikali ya Tanzania inakua na la kujifunza.

Ushauri wangu kwa CDM, waangalie namna mpya ya ku capture mioyo ya vijana, ambao ni wengi na wana hali ngumu ya maisha, pamoja na kukosa ajira kulikokithiri. Waje na ajenda zinazogusa maisha ya watanzania moja kwa moja na namna bora ya kutatua hizo changamoto.

Hakuna kijana aliyokosa ajira na kua na maisha duni, ataenda kuandamana kudai katiba mpya na uhuru wa kutoa maoni. Vijana wataandamana kudai ajira na mazingira mazuri ya kujenga uchumi wao. CDM badilikeni.
 
Urais wa kurith vipi wakati ana power yote na mnasema anatawala kwa katiba ambayo ina mpa nguvu kubwa sana rais? Kwamba anaweza kutamka lolote mpaka hao sukuma gang wakapoteana?

Anaweza kufanya lolote, lakini sio dhidi ya sukuma Gang. Anaweza kufanya lolote kwenye kuminya haki, lakini sio kwenye kulinda maslahi ya majizi wenzake wa kura. Pamoja na nguvu zote wanazopata kupitia katiba hii, ukweli wa kuwa yuko madarakani kwa wizi wa kura haufichiki, hivyo ni aidha asimamie kwenye haki ile kwake, au alinde maslahi ya majizi wenzake. Na kwa sasa ameamua kusimama na upande wa majizi wenzake.
 
Mkuu kwani kwa mujibu wako huyu mama si siyo dhalimu kama Magufuli?

Sasa haya ya sukuma gang yanatoka wapi?

Yeye ni muungwana sana kwa mujibu wako,
Kwa mujibu wako halindwi na mabunduki kama dhalimu wako, kwa sababu yeye siyo dhalimu kwa hiyo haogopi chochote.

Na kwa vile siyo dhalimu kama unavyosemaga si anaweza kuifutilia mbali hiyo sukuma gang yako unayoisema?
 
Bila kupinga maelezo yako mengine mazuri, unataka Mbowe asamehewe kwani amefanya kosa gani? Au asamehewe kubambikiwa kesi? Sioni msingi wowote wa yeye kusamehewa wakati hana kosa. Tusitake kuwapa wahalifu haki ya kuhukumu wenye haki, yaani watu kuwa viongozi haimaanishi wasemacho ni kweli, maana huko kubambikizia kesi sio jambo geni, ila tutawapa uhalali hao walevi wa madaraka kutaka wamsamehe mtu wanayemuonea.
 

Narudia tena, huyo mama sio dhalimu kama yule ibilisi, ila amekubali kuridhisha hilo kundi la wadhalimu kwani ana cheo cha urithi, tena cheo cha wizi wa kura. Hivyo hana namna zaidi ya kutumikia kundi la waouvu, kwani utawala wake umepatikana kwa uovu hata yeye hilo analijua. Angekuwa yuko madarakani kwa kura halali angeweza kulifuta hilo kundi la sukuma Gang, ila sio kwa namna madaraka hayo yalivyopatika. Habari ndio hiyo boss.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Ana power yote inayosapotiwa na katiba mnayotaka ibadilishwe!

Vyombo vyote vya usalama vinamtii yeye!
.
Sasa inakuwaje hana hiyo nguvu ya kuvunjilia mbali hilo genge wakati yeye siyo dhalimu kama yule dhalimu wako?
 
UGAIDI, hata Maana ya UGAIDI hamjui, mpo shabikia tu, twende tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…