Freeman Mbowe: CHADEMA kufanya Mikutano Nchi nzima kuanzia Mwezi wa nne. Bado tunahitaji kujua waliomuua Aquilina

Uzuri mpaka uchagani walishawastukia uongo wenu, kauli yake haina tofauti na kauli ya mlevi kutishia nitakufumua huku mwenyewe hata kusimama hawezi. Taasisi anayoishutumu ni kubwa kuliko mtu na haitalegeza msimamo wa kulinda amani.

Swala la Upinzani haliko uchagani hii ni Tanzania nzima wewe.
 
Mbowe ametangaza vita na Magufuli
Baada ya jamaa kujua Mbowe ataongea leo na wao wakaweka maigizo yao ati Mh anaenda Morogoro lakini kila mahali ana simama kusikiliza kero. Kwa fikra kwamba watu wataacha kumsikiliza Mbowe wahamie kwake. Kumbe watu wana hamu na hotuba ya Mwamba na sio yeye

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swala la upinzani haliko uchagani hii ni tanzania nzima ww utopolo
Ewe mbuyuyu, uchagani kuna viumbe mnadhani mna haki miliki ya urais, mnadhani mna haki miliki ya nyazifa za juu serikalini, na kwa sababu mianya ya rushwa mmezibiwa na ninyi mlizoea kuiba na ni wezi ndiyo maana mnapata tabu sana na chuki zenu binafsi.
 
Baada ya jamaa kujua Mbowe ataongea leo na wao wakaweka maigizo yao ati Mh anaenda Morogoro lakini kila mahali ana simama kusikiliza kero. Kwa fikra kwamba watu wataacha kumsikiliza Mbowe wahamie kwake. Kumbe watu wana hamu na hotuba ya Mwamba na sio yeye
Mawazo ya kiufipa ufipa haya. Unadhani hiyo safari ilipangwa jana usiku?
 
Mikutano ya vyama vya siasa ipo kisheria na hata katiba ya nchi inalitambua hilo
Katazo la rais ndio lipo kinyume na katiba na mh rais amekuwa akiivunja katiba ya nchi kwa miaka yote aliyokuwa madarakani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ewe mbuyuyu, uchagani kuna viumbe mnadhani mna haki miliki ya urais, mnadhani mna haki miliki ya nyazifa za juu serikalini, na kwa sababu mianya ya rushwa mmezibiwa na ninyi mlizoea kuiba na ni wezi ndiyo maana mnapata tabu sana na chuki zenu binafsi.
angalau kwasababu awamu hii unapumua kwa kubebwa lazima ukaze msuli
 
Mboe simamia hapo hapo...vijana tumechoka..ajira hamna, mazingira mabovu ya wanyabiashara, haki ya mfanyakazi wa umma imeteketezwa, huduma mbovu za jamii...mimi kama kijana nipo tayari kufa kutetea haki yangu na kizazi kijacho....stand up for my rights..
Mkutano wa Mwenyekiti wa CHADEMA NA WAANDISHI, Machi 16,2020.

====
Updates
View attachment 1389820

“Watanzania walifikiri mashtaka yetu yanahusika na kumuua Akwilina, hatuwezi kufunga faili la kesi ile bila kujua hatma ya Akwilina”.Mhe.Mbowe.

“Waliohusika wasiachwe wakacheza na maisha ya watanzania, hawa watu wachukue hatua mkononi kuwajua askari wote waliomuua Akwilina" Mhe.Mbowe.

“Mimi nikiwa jela kule nikiwa shambani zimepigwa risasi zaidi ya 13, za moto,wanapambana na Halima Mdee, Ester Bulaya, na Jesca Kishowa, hawa ni wamama, hata katika sheria za magereza wanaoruhusiwa kushughulika na wanawake ni wanawake tu, lakini hapa ni wanaume wenye vifua, wenye silaha, wanamshughulikia Halima wamemuweka mtu kati”. Mhe. Mbowe.

Mimi na viongozi wenzangu waandamizi tulipohudhuria sherehe za Uhuru uwanja wa Kirumba Mwanza nilipopewa nafasi ya kusalimia na nikamtaka rais aone ulazima wa kutengeneza maridhaino kuleta maridhiano… alisema nimesikia”.Mhe.Mbowe.

Sisi tulipoyataka maridhiano ya Kitaifa hayakuwa kielelezo cha uoga, ilikuwa kielelezo cha kuitaka amani katika nchi yetu kwa sababu tunaona tunakokwenda siko…”.Mhe.Mbowe.
''Natangaza rasmi kuwa kuanzia mwezi ujao wa nne tutaanza kufanya mikutano ya hadhara nchi nzima bila kujali kuna katazo la Rais Magufuli na tuko tayari kwa lolote, tumekuwa waungwana vya kutosha na sasa hatutarudi nyuma kwenye hili'' - Freeman Mbowe

"Nawatangazia viongozi wote wa Chadema nchi nzima kuanzia Majimbo, Kanda, Kata, Vijiji na Mitaa kufanya mikutano ya hadhara nchi nzima, kwanza ni kudai tume huru na pili ni maandalizi ya Uchaguzi Mkuu"
"Subira yetu, uvumilivu wetu na upole wetu umedharauliwa vya kutosha. Kama watatumia polisi na magereza kutufunga wote, watufunge. Tuko tayari kwa lolote. Kama wanafikiri mabomu, risasi na jela ni suluhu, basi wakatumie," Mbowe, Mwenyekiti Chadema

yes kamanda mbowe
 
Back
Top Bottom