Pre GE2025 Freeman Mbowe: CHADEMA nipo, nitakuwepo na nitagombea. Anayetaka kugombea tukutane kwenye sanduku la kura

Pre GE2025 Freeman Mbowe: CHADEMA nipo, nitakuwepo na nitagombea. Anayetaka kugombea tukutane kwenye sanduku la kura

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wakati wowote kuanzia sasa Mhe Freeman Mbowe kutoa tamko rasmi la ama atagombea Uenyekiti wa CHADEMA ngazi ya Taifa ama laa.

Mtakumbuka Mhe Freeman Mbowe ameitumikia nafasi hii kwa zaidi ya miongo miwili sawa na miaka 21 mfululizo.

Endapo atatangaza kugombea tena atakuwa ni mgombea wa nne nyuma ya Tundu Lissu na Odero Odero,

Je, kama Taifa tunatarajia nini kutoka Upinzani kuelekea 2025?

Usiondoke hapa Jf kwa habari zaidi

=======================================

Siku ya leo Disemba 12, 2024 Freeman Mbowe ametangaza rasmi kugombea kwa mara nyingine nafasi ya Uenyekiti wa CHADEMA Taifa.

Mbowe amsema kuwa kutokana na Uchaguzi mkuu ambao unakuja si vyema kubadilisha "makamanda" na kwamba bado yupo sana kuongoza chama hicho na mara baada ya mkutano anaenda kuchaukua fomu kwenye makao makuu ya chama hicho, Mikocheni.

"Kwa kuzingatia yote haya na mengine mengi ambayo sitaki kuwachosha. Nilisema mara nyingi kuwa nilitamani kuondoka lakini siwezi kuondoka katikati ya minyukano iliyopo. Kwa hiyo CHADEMA nipo, nitakuwepo na nitagombea"

View attachment 3181677



View: https://www.youtube.com/live/8WGa7Xv3hKo?si=JjooipgRmN035_2F

Ningeshangaa yaani uache chama Kwa wahuni na mawakala wa Mabeberu? 🤣🤣
 
🥱😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭😭
So sad
 
Hapo tayari tushajua kugombea kwake ni maelekezo. Tukishindwa kwenye kura tutamuachia chama chake
Hichi ndicho ninachotaka kukiona mimi kama mnadhani kujenga chama mpaka kikubalike ni mzaha.

Zitto Kabwe ameshawauzia ACT Wazanzibar kakaa zake pembeni anajuwa kujenga chama Tanganyika si shughuri ya kitoto.

Sasa ni zamu yenu kuonesha kwa vitendo kama mna uwezo huo, uchaguzi ni namba, Mbowe ameshashinda uchaguzi kabla haujafanyika, kwahiyo kama ni kuondoka ondokeni sasa msipoteze muda.
 
Back
Top Bottom