Pre GE2025 Freeman Mbowe: CHADEMA nipo, nitakuwepo na nitagombea. Anayetaka kugombea tukutane kwenye sanduku la kura

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hivi ni kweli yule uliye kuwa unasema na kuimba demokrasia, demokrasia....!!! Leo hii wa kung'ang'ania madaraka hadi yanakutia upofu!! Ninani anayekushauri vibaya namna hiyo....
Ninakili tunamshukuru sana TAL kutuonyesha upande wenu wa 2,kumbe CDM chini ya utawala wako hakuna upinzani zaidi ya kuwa msaada kwa CCM!!!
Kwani huyo Lisu wewe unadhani anatafuta nini kama sio utamu wa madaraka?

Mbowe amuachie Ili kitokee nini? 👇👇

View: https://www.instagram.com/p/DEAXfvVIWoV/?igsh=bHNkdG1sb2xpYjFy
 
Hivi ni kweli yule uliye kuwa unasema na kuimba demokrasia, demokrasia....!!! Leo hii wa kung'ang'ania madaraka hadi yanakutia upofu!! Ninani anayekushauri vibaya namna hiyo....
Ninakili tunamshukuru sana TAL kutuonyesha upande wenu wa 2,kumbe CDM chini ya utawala wako hakuna upinzani zaidi ya kuwa msaada kwa CCM!!!
Kaka huo ni mradi wa familia. Yani huna akili au!?
 
Hupendi Demokrasia. Na unathibitisha mnataka Lissu apite bila ushindani.
Ni mawazo yako nitaendelea kuyaeshimu, binafsi nimeangalia katika angle ya kuwagawa wanachama, pia swala la uchaguzi mbele yetu.
 
Nani kati yenu aliwahi kupinga Chadema kubadili Katiba na kuondoa ukomo wa madaraka ya Mwenyekiti? Kipindi kile sie tunapinga si mlikuwa mnamtetea Mbowe nyie? Badala ya kupinga chanzo, eti leo mnalalamikia matokeo? Ndio maana Mimi namwita Lissu mwehu kwasababu alikuwepo na alisimamia uondoaji ukomo wa madaraka ya Mwenyekiti. Leo analoloma nini?
Mwehu ni wewe na mamayenu huko ccm ambao mnajadili kauli za lissu nusu nusu.
 
Ahahahahaha! Povu la nini dogo? Jibu hoja. Wakati mnaondoa ukomo wa madaraka ya Mwenyekiti mlikuwa mnataka nani aendelee kukaa kama sio Mbowe! Ahahahahaha! Sasa hivi povu la nini! Ukimfuga chatu na ukashindwa kumlisha, anakutafuna mfugaji! Ahahahahaha!!!
 
Huo ndiyo ukweli.kama kiongozi anafanya vizuri hakuna haja ya kumtoa
Ndiyo, aongoze hadi mauti itapomtenga na uongozi sababu hakuna aliye bora zaidi yake?
Anyways, waoiga kura wataamua na sisi wabangaizani tutakuwa na wakati na mahali petu pa kupazia sauti.
Time will tell.
 
Hivi ni kweli yule uliye kuwa unasema na kuimba demokrasia, demokrasia....!!! Leo hii wa kung'ang'ania madaraka hadi yanakutia upofu!! Ninani anayekushauri vibaya namna hiyo....
Ninakili tunamshukuru sana TAL kutuonyesha upande wenu wa 2,kumbe CDM chini ya utawala wako hakuna upinzani zaidi ya kuwa msaada kwa CCM!!!
Kamzuia nani mbona mnazusha agenda za kuonewa huruma. Nenda kagombee atakaechaguliwa na wanachama atakua mwenyekiti. Hamna aliezuiwa kugombea wala uchaguzi haujafutwa
 
Sitaki kuamini kama anadhamiri ya dhati ya kufanya uchaguzi uhuru na haki kutokana na Kauli za watu wake. Pia binafsi sikutaka kwa yeye kuingia kwenye ushindani na TAL kutokana na unyeti wa Siasa zetu. Sababu kuu ni Moja kupunguza ahiba kwa mtia nia wa urais pia kupoteza baadhi ya wapiga kura kutokana na matokeo yeyote kati yake na Tundu Lissu.
Uchaguzi huru na wa haki unatakiwa uwe vipi? Weka hapo sifa za huo uchaguzi ili tuone kama hadi sasa zimekiukwa
 
Ni mawazo yako nitaendelea kuyaeshimu, binafsi nimeangalia katika angle ya kuwagawa wanachama, pia swala la uchaguzi mbele yetu.
Sasa kuwagawa wanachama huwrza kutokea kwa namna nyingi. Mfano Mbowr asigombee halafu atangaze kumuunga mkono Odero, Wanachama watagawanyika?
 
Halotel GB mwez 🔥🔥

GB 13 Kwa 14000
GB 14 Kwa 15000
GB 15 Kwa 16000
GB 16 Kwa 17000
GB 18 Kwa 19000
GB 20 Kwa 21000
GB 30 Kwa 29000
GB 33 Kwa 32000

Mwenye uhitaji na hizo GB za halotel inbox
Wewe hizi unazitoa wapi kwa sababu nimewahi kutapeliwa kwa njia hii hii hadi nikatoa angalizo humu.
 
Wakati wowote kuanzia sasa Mhe Freeman Mbowe kutoa tamko rasmi la ama atagombea Uenyekiti wa CHADEMA ngazi ya Taifa ama laa.

Mtakumbuka Mhe Freeman Mbowe ameitumikia nafasi hii kwa zaidi ya miongo miwili sawa na miaka 21 mfululizo.

Endapo atatangaza kugombea tena atakuwa ni mgombea wa nne nyuma ya Tundu Lissu na Odero Odero,

Je, kama Taifa tunatarajia nini kutoka Upinzani kuelekea 2025?

Usiondoke hapa Jf kwa habari zaidi

=======================================

Siku ya leo Disemba 21, 2024 Freeman Mbowe ametangaza rasmi kugombea kwa mara nyingine nafasi ya Uenyekiti wa CHADEMA Taifa.

Mbowe amsema kuwa kutokana na Uchaguzi mkuu ambao unakuja si vyema kubadilisha "makamanda" na kwamba bado yupo sana kuongoza chama hicho na mara baada ya mkutano anaenda kuchaukua fomu kwenye makao makuu ya chama hicho, Mikocheni.

"Kwa kuzingatia yote haya na mengine mengi ambayo sitaki kuwachosha. Nilisema mara nyingi kuwa nilitamani kuondoka lakini siwezi kuondoka katikati ya minyukano iliyopo. Kwa hiyo CHADEMA nipo, nitakuwepo na nitagombea"

View attachment 3181677

View: https://www.youtube.com/live/8WGa7Xv3hKo?si=JjooipgRmN035_2F

Siku za Mbowe zinahesabika
 
Kesho
 
Back
Top Bottom