Pre GE2025 Freeman Mbowe: CHADEMA nipo, nitakuwepo na nitagombea. Anayetaka kugombea tukutane kwenye sanduku la kura

Pre GE2025 Freeman Mbowe: CHADEMA nipo, nitakuwepo na nitagombea. Anayetaka kugombea tukutane kwenye sanduku la kura

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Sasa kama ulikuwa CDM ndio kusema unaogopa uchaguzi au? Hiki ni chama Cha kidemokrasia. Siyo cha kutoa fomu moja. Fomu zimetolewa nyingi na wewe chukua ugombee. Huku CDM nakuna umwinyi wa kutoa fomu moja
Jambo usilolifahamu ni sawa na usiku wa kiza kinene.
 
Ili Kukata mzizi wa fitina kura zihesabiwe hadharani na kila mgombea apewe kura zake ahesabi mwenyewe.

Kukomesha fitina dawa ni hiyo tu.
Ndo ninachokitaka namimi hicho. Nashangaa hawa wahubiri wa demokrasia hawataki wenzao washiriki chaguzi. Mi naona ni wakati sahihi wa Lissu kumshinda Mbowe kwenye boksi la Kura!!
 
Wakati Chacha Wangwe anataka kugombea uenyekiti.Lissu hakuwa Chadema? ILIKUWA MWAKA 2008.Ninakumbuka Lissu alimlalamikia sana Chacha Wangwe hadi kusema kamsaidia case nyingi mno.I wish niupate ule uzi niuperuzi.Lissu alikuwa upande wa Mbowe .
Hivi wewe unaelewa kiswahili kweli? Lisu amejiunga na Chadema gari likiwa limeshawaka ndio sababu kuu ya yeye kuondoka Nccr Mageuzi kujiunga Chadema ili kuongeza nguvu na akagombea Ubunge kwao akashinda.

Hakuna cha unabii wowote Wabongo mnapenda sana porojo.

Sasa ni wakati wa Lisu kumuangusha Mbowe kwenye uchaguzi huru na wa haki kama alivyofanya Jacob Zuma kumuangusha Thabo Mbeki Urais wa ANC na akiwa Rais wa nchi Mbeki pia.

Sasa Mbowe hana dola mnatokwa mapovu, nendeni kwenye box mkamng'oe, akishinda maana yake yeye ndiye anayekubalika na tutaangalia margin vote ni tofauti ya kura ngapi.
 
Cha msingi wajumbe wajipange na kumpigia kura anayefaa ,binafsi sioni shida hapa ,ni haki yake kwa mjibu wa katiba sass shida iko wapi
Wajumbe wananunuliwa kwa pesa au kwa ahadi za kupewa nafasi za kugombea ubunge mwakani au nafasi za viti/u
maalum za ubunge.Hivyo vitu Lissu hawezi kuvifanya kwa sababu sio mnafiki.

Siasa za kiafrika huwezi kuzimudu kwa muda mrefu kama sio mnafiki.Either utaondolewa mapema au utachafuliwa kwa propaganda ambazo jamii ya kinafiki ya kiafrika itazichukua na kukupondea nazo kichwani.Mbowe ni mzuri kwenye hizo negotiations za kimaslahi ya pande zote mbili.

Kwahiyo tegemea kuwa Mbowe kabla ya kuamua kugombea ameshajua kura zake zitatoka wapi.

Mtu msafi kama Lissu ni vigumu kupigiwa kura na watu wanaotaka wafaidike na hizo kura zao kupitia yeye.Mbowe kwakuwa tu maslahi yake yanahakikishwa basi yeye pia
hana nongwa kuwapa maslahi yao watu waliompa maslahi yake.

Tegemea wale covid 19 kurudi/kusamehewa baada ya ushindi wa Mbowe.Ni maslahi maslahi maslahi....
 
Bado tuna nafasi ya kwenye sanduku la kura,TLS akishindwa namshauri aanzishe chama kingine cha Siasa,surely I'm telling you hicho ndio kitakuwa chama kikuu cha upinzani Tanzania!
Sasa chama kimepasuka sana, tundu Lissu keshashindwa tayari, sasa imebaki kuçhafuana na kukashfiàna.
Hawa jàmaa wote ni walafi. Mbowe hawezi kumpa fungu Lissu aachane na uçhaguzi aende zake ubelgiji ili kutuliza hali ya hewa.
Lissu nae hakubali kumwachia Mbowe mnofu wote.
Tungoje covid 19 wanasemaje.
 
Back
Top Bottom