Pre GE2025 Freeman Mbowe: Dkt. Slaa na wanaojiita Tanzania Diaspora wanapanga kufanya mapinduzi ndani ya CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA @chadematzofficial Freeman Mbowe amesema kuna makundi yanayoratibu kufanyika mapinduzi ndani ya chama hicho na makundi hayo ndiyo yanayomsukuma Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Bara, Tundu Lissu kugombea nafasi ya Uenyekiti.

“Kuna kundi linaloitwa diaspora (watanzania waishio ughaibuni) ni kundi dogo tu wala sio kusema ni diaspora wote wa Tanzania hili kundi dogo linalojaribu kupanga mapinduzi ndani ya CHADEMA wengine hata hatuwajui tunawaona tu kwenye majina ya mitandaoni wanajiita Tanzania Diaspora ni kundi ndani ya Diaspora”

Mbowe ameeleza kuwa zaidi ya kundi hilo kuna kikundi kingine kinachoitwa Sauti ya Watanzania ambacho kinachoongozwa na aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho Dkt. Wilbroad Silaa

“Kuna makundi ya watu kama Dkt. Silaa na kikundi kinachojiita Sauti ya Watanzania, Dkt. Silaa alikimbia CHADEMA mwenyewe akaenda Chama Cha Mapinduzi (CCM) akafungiwa Serena pale(Serena Hotel) baadae akahamishiwa Canada akapewa zawadi ya ubalozi.”

Mbowe ameongeza kuwa amekuwa akishangazwa na wanaomuunga mkono Lissu kuwa sio watu ambao ni wanachama kweli kweli hata hivyo anashindwa kuelewa kwa nini Dkt. Silaa hawekezi nguvu kwenye chama chake bali anawekeza muda na nguvu CHADEMA.

“Kazi aliyoifanya muda wote akiwa balozi(Dkt.Silaa) chini ya utawala wa Magufuli(Hayati Dkt. John Pombe Magufuli) ni kujaribu kuichonganisha CHADEMA na kutoa taarifa na mpaka kuandika kitabu cha uongo eti leo Dkt.Silaa ndiye anafanya kampeni ya Lissu kuchukua uongozi wa chama alisahau nini Dkt Silaa ambacho leo anakitaka”

Hata hivyo Mbowe ameongeza kuwa wengine wanaomuunga mkono Lissu ni pamoja na aliyekuwa Mbunge wa Iringa na Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Mchungaji Peter Msigwa ambaye kwa sasa ni kada wa CCM.

Source: Jambo TV
Huyu mzee na chama chake wangeshika nchi tungeumia sana.

..................Yaani chama tu hataki kuachia sijui angeonja utamu wa kuwa Rais ingekuwaje?
 
Wanataka kukiteka chama, na wana hela zinamwagwa kama jungu hasa kanda ya ziwa.
Dr. Slaa kaahidiwa ujumbe wa kamati kuu.

Mbowe wabananishe, watanzania tupo na wewe tunajua ulipotutoa hadi leo tulipo.

Pipooozzzz - kama hutaki tangulia TLP haina mwenyewe.
 
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA @chadematzofficial Freeman Mbowe amesema kuna makundi yanayoratibu kufanyika mapinduzi ndani ya chama hicho na makundi hayo ndiyo yanayomsukuma Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Bara, Tundu Lissu kugombea nafasi ya Uenyekiti.

“Kuna kundi linaloitwa diaspora (watanzania waishio ughaibuni) ni kundi dogo tu wala sio kusema ni diaspora wote wa Tanzania hili kundi dogo linalojaribu kupanga mapinduzi ndani ya CHADEMA wengine hata hatuwajui tunawaona tu kwenye majina ya mitandaoni wanajiita Tanzania Diaspora ni kundi ndani ya Diaspora”

Mbowe ameeleza kuwa zaidi ya kundi hilo kuna kikundi kingine kinachoitwa Sauti ya Watanzania ambacho kinachoongozwa na aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho Dkt. Wilbroad Silaa

“Kuna makundi ya watu kama Dkt. Silaa na kikundi kinachojiita Sauti ya Watanzania, Dkt. Silaa alikimbia CHADEMA mwenyewe akaenda Chama Cha Mapinduzi (CCM) akafungiwa Serena pale(Serena Hotel) baadae akahamishiwa Canada akapewa zawadi ya ubalozi.”

Mbowe ameongeza kuwa amekuwa akishangazwa na wanaomuunga mkono Lissu kuwa sio watu ambao ni wanachama kweli kweli hata hivyo anashindwa kuelewa kwa nini Dkt. Silaa hawekezi nguvu kwenye chama chake bali anawekeza muda na nguvu CHADEMA.

“Kazi aliyoifanya muda wote akiwa balozi(Dkt.Silaa) chini ya utawala wa Magufuli(Hayati Dkt. John Pombe Magufuli) ni kujaribu kuichonganisha CHADEMA na kutoa taarifa na mpaka kuandika kitabu cha uongo eti leo Dkt.Silaa ndiye anafanya kampeni ya Lissu kuchukua uongozi wa chama alisahau nini Dkt Silaa ambacho leo anakitaka”

Hata hivyo Mbowe ameongeza kuwa wengine wanaomuunga mkono Lissu ni pamoja na aliyekuwa Mbunge wa Iringa na Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Mchungaji Peter Msigwa ambaye kwa sasa ni kada wa CCM.

Source: Jambo TV
Duh!...yaani Lissu anatumika tu?... tuhuma nzito hizi.

Fundi Mchundo Retired Quinine JokaKuu
 
Uko.sahihi
Uchaguzi huu ni mchuano kati ya diaspora na wazawa

Wazawa tutawavwaga Diaspora. Na Diaspora wao Lisu atarudi kwao ubelgiji nikono mitupu bila cheo chochote
Nimekuwa nikiuliza hili swali, ukibaraka wa lissu ni upi wapi na lini? Prove kuna ni kibaraka na ni kibaraka gani masikini?
 
Muda mwingi yuko ubelgiji sio.Tanzania hata sasa hivi hayuko nchini yuko ubelgiji
 
Mbona Mandela muda mwingi alikuwa Tanganyika hadi akasahau viatu vyake Kwa mama Massawe? 🐼

Usiwe tutusa meku 😂😂😂
Wapigania uhuru walikuwa wanaandaliwa Tanzania kwenda kupigana Africa kusini.Makambi yao yalikuwa Tanzania Mandela hakuwa Tanzania kuishi tu

Lisu anaandaa nani ubelgiji?

Usilinganishe Lisu na Mandela
 
Back
Top Bottom