Pre GE2025 Freeman Mbowe: Dkt. Slaa na wanaojiita Tanzania Diaspora wanapanga kufanya mapinduzi ndani ya CHADEMA

Pre GE2025 Freeman Mbowe: Dkt. Slaa na wanaojiita Tanzania Diaspora wanapanga kufanya mapinduzi ndani ya CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
MBOWE aache kutapa tapa....aache kulalama.....kila mwana chadema mwenye vigezo na sifa ana haki ya kuwa mwenyekiti.....hicho kiti hakijawekwa akae peke mpaka akiwa maiti...

Kwanini kila msimu wa uchaguzi CHADEMA kunazuka mtafaruku kwa wagombea webgine kana kwamba wanafanya jambo baya......
Hana hekima za kuhubiri demokrasia wakati yeye haongozi kidemokrasia anakumbuka kuhusu demokrasia anapokuwa nyuma ya mikamera hasa wakati wa chaguzi

He is an opportunity seeker while calculating risk
 
Bila shaka Lisu hakuweka wazi jina la kiongozi wa kiroho, huyu kitenge sijui alitoa wapi hilo jina!!, anyway hakuna ubaya kwa kiongozi wa kiroho kupatanisha watu maana imeandikwa heri wapatanishi
Na aliyewatafuta hao viongozi wa kiroho ni yeye mwenyewe Mbowe. Huyu kitenge naye si ndiyo wote wanufaika wa hela ya DP World kama alivyo Mbowe.
 
Kweli tupu. Kuna pia wale ambao kwa namna moja au nyingine wanaamini kuwa hawajatendewa haki katika uongozi wake. Hii ni pamoja na Lissu mwenyewe ambae amesema wazi kuwa Mbowe alitaka kumtilia kauzibe kupitia Wenje. Kuna wale walioshindwa au mtu wao alishindwa ( k.m. Msigwa)chaguzi tofauti.

Na pia wako ambao kwa dhati kabisa wanaamini kuwa kuna haja ya kuibadilisha Chadema ili ionekane kuwa inampambania mtanzania wa kawaida. Hawa wa mwisho hawataki kabisa CDM ipasuke ila hawana jinsi.

Amandla...
...Mbowe kafanya madudu mengi Sana kwa Mgongo wa uwenyekiti wa chadema
 
Sijawahi kumuona Mbowe akiwa under pressure, kumbe akiwa depressed anakuwa boya kiasi hichi, imagine huyu angaukwaa uraisi wa Tanzania angepiga marufuku hata neno UCHAGUZI na KATIBA. hata Mobutu Sese seko huko aliko angaionea huruma Tanzania.
Haahaa kutamka neno demokrasia ni rahisi Sana, vitendo ndo kazi ..
 
Kampeni hasa za chama namaanisha wote mnajenga nyumba moja si vizuri kuanza kuchambana ,uchaguzi ndani ya chama wajikite kwenye hoja/sera na si attacks ...siasa za attacks ni Chama A kwenda Chama B.

Lissu ana attack viongozi wake sasa na kiongozi akiwa attacked lazima ajibu ili kuweka mambo clear na hapo ndipo yanapotokea malumbano.

Ukiona unasifiwa na adui basi jua unakosea...Lissu anasifiwa sana na anapata support kubwa kutoka sisiemu.
Kwa maoni yangu Lissu hafanyi attacks bali sera na misimamo yake inawavua wengine nguo.
Huwezi kusema nitaondoa rushwa na ubinafsi bila kuwaambia watu unaondoa rushwa ipi. Usipoonyesha viashiria vya rushwa maana yake unataka kuondoa kitu kisichokuwepo.

Kwa wingi wa tuhuma za Mbowe huwezi kusisema kistaarabu hata kidogo, huwezi kupaka paka mafuta mtu anayekiuka misingi ya Utawala bora
 
Tetesi toka Twitter zinasema mwamba kalambishwa asali ya 12B + na bado anataka asali zaidi. Dr slaa kazungumzia hilo clubhouse ya Twitter anasema kapewa Taarifa na vijana wa system. Vijana wa system wameona wampe taarifa slaa

Video ya sauti ya Dr slaa akielezea watu wanavyolamba asali ipo hapo

View: https://youtu.be/lU_QbyAtMUM?si=w_g-bndY2v_e58vQ

..Chadema bila mbowe kuondolewa kwenye uwenyekiti watakuwa na wakati mgumu Sana...
 
Kwa mujibu wa Lissu yupi ulisikiliza mahojiano yake ya jana? Mbona laiweka wazi hasa kilichomsukuma kugombea hicho kiti, Mbowe Mwenyewe ndo kafanya agombee hicho kiti, kwa kujifanya yeye ndo master
..Mbowe anahubiri demokrasia huku mwenyewe akiikandamiza..m
 
Kwa maoni yangu Lissu hafanyi attacks bali sera na misimamo yake inawavua wengine nguo.
Huwezi kusema nitaondoa rushwa na ubinafsi bila kuwaambia watu unaondoa rushwa ipi. Usipoonyesha viashiria vya rushwa maana yake unataka kuondoa kitu kisichokuwepo.

Kwa wingi wa tuhuma za Mbowe huwezi kusisema kistaarabu hata kidogo, huwezi kupaka paka mafuta mtu anayekiuka misingi ya Utawala bora
Hata na yeye ni mla rushwa , michango ya matibabu wamechanga viongozi wa chadema na wanacnhi ila invoice amezidai zote 800m kama zake huo ni wizi/utapeli kukosa uhadilifu.

Hana uhakika nani aliyekula rushwa bali ni hisia zake tu ,kama ana uhakika watu wamevuta mabilioni ya abdul apeleke kwenye kamati ya maadili watu wachukuliwe hatua.
 
Kampeni hasa za chama namaanisha wote mnajenga nyumba moja si vizuri kuanza kuchambana ,uchaguzi ndani ya chama wajikite kwenye hoja/sera na si attacks ...siasa za attacks ni Chama A kwenda Chama B.

Lissu ana attack viongozi wake sasa na kiongozi akiwa attacked lazima ajibu ili kuweka mambo clear na hapo ndipo yanapotokea malumbano.

Ukiona unasifiwa na adui basi jua unakosea...Lissu anasifiwa sana na anapata support kubwa kutoka sisiemu.
Lisu anaungwa mkono na watu gani vile? Kwamba Lisu alishinda uenyekiti CCM watafurahi sio?
 
Sijawahi kumuona Mbowe akiwa under pressure, kumbe akiwa depressed anakuwa boya kiasi hichi, imagine huyu angaukwaa uraisi wa Tanzania angepiga marufuku hata neno UCHAGUZI na KATIBA. hata Mobutu Sese seko huko aliko angaionea huruma Tanzania.
Vichwa panzi kutiwaambia hata yale mateso aliyokuwa anapitishwa nyingi zilikuwa script za kaole sasa anachezeshwa game lisilo na director ndio ndio tunaona rangi yake halisi
 
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA @chadematzofficial Freeman Mbowe amesema kuna makundi yanayoratibu kufanyika mapinduzi ndani ya chama hicho na makundi hayo ndiyo yanayomsukuma Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Bara, Tundu Lissu kugombea nafasi ya Uenyekiti.

“Kuna kundi linaloitwa diaspora (watanzania waishio ughaibuni) ni kundi dogo tu wala sio kusema ni diaspora wote wa Tanzania hili kundi dogo linalojaribu kupanga mapinduzi ndani ya CHADEMA wengine hata hatuwajui tunawaona tu kwenye majina ya mitandaoni wanajiita Tanzania Diaspora ni kundi ndani ya Diaspora”

Mbowe ameeleza kuwa zaidi ya kundi hilo kuna kikundi kingine kinachoitwa Sauti ya Watanzania ambacho kinachoongozwa na aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho Dkt. Wilbroad Silaa

“Kuna makundi ya watu kama Dkt. Silaa na kikundi kinachojiita Sauti ya Watanzania, Dkt. Silaa alikimbia CHADEMA mwenyewe akaenda Chama Cha Mapinduzi (CCM) akafungiwa Serena pale(Serena Hotel) baadae akahamishiwa Canada akapewa zawadi ya ubalozi.”

Mbowe ameongeza kuwa amekuwa akishangazwa na wanaomuunga mkono Lissu kuwa sio watu ambao ni wanachama kweli kweli hata hivyo anashindwa kuelewa kwa nini Dkt. Silaa hawekezi nguvu kwenye chama chake bali anawekeza muda na nguvu CHADEMA.

“Kazi aliyoifanya muda wote akiwa balozi(Dkt.Silaa) chini ya utawala wa Magufuli(Hayati Dkt. John Pombe Magufuli) ni kujaribu kuichonganisha CHADEMA na kutoa taarifa na mpaka kuandika kitabu cha uongo eti leo Dkt.Silaa ndiye anafanya kampeni ya Lissu kuchukua uongozi wa chama alisahau nini Dkt Silaa ambacho leo anakitaka”

Hata hivyo Mbowe ameongeza kuwa wengine wanaomuunga mkono Lissu ni pamoja na aliyekuwa Mbunge wa Iringa na Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Mchungaji Peter Msigwa ambaye kwa sasa ni kada wa CCM.

Source: Jambo TV
Mbowe amefimisika kisiasa anatumia mbinu za kijinga kabisa wakati wenzake wanapinga ufisadi na uhuni wa kisasa unaowasanabisha watanzania kukata tamaa ya kupiga kura .

Yaani Mbowe anatumia mbinu zile zile za CCM na vyombo vya dola vya kuwasingizia wapinzani kuwa eti kuna watu wanataka kufanya mapinduzi.

Mbowe anatumia mbinu za CCM kushinda uchaguzi lakini ajue wazi kuwa anafuata nyayo za akini Mrema na Lipumba .

Kwani suala la rushwa na kula pesa za chama na kukifanya chama kuwa taasisi ya kikabila na Sacoss imeanza kusemwa na Lisu ?
Kwa nini Mbowe anamshambulia sana Lisu wakati Mbowe ameanza kutuhumiwa tangu 2014 mpaka leo .
Ametuhumiwa na CCM na ametuhumiwa na Wanachama na viongozi wenzake kama Slaa, Zito,Kafulila , Msigwa na Mkumbo . Mapaka wengine wakakimbia chama kwa hofu ya kushughulikiwa na mbowe.

Mbowe anafikiria akimshinda Lisu atatoboa mbele ya CCM
Hakuna CCM anayetaka kupoteza kiti cha ubunge wala udiwani . Watamshughulikia kisawasawa maana ana tuhuma nyingi na wanaushahidi wa kutosha na yeye anajua.

Kuliko Mbowe ashinde kwa uhuni na ufisadi na tamaa yake ni bora chadema ife mana sio dini wala mama watu wala baba ,ni chama tu lilichoanzishwa . Kama kanu iliyokua na dola na utajiri mkubwa wa Wakikuyu na wakalenjii ilikufa Chama ni nini mpaka kibaki kuhadaa watanzania kuwa kuna demokrasia wakati ni uhuni mtupu.

Mbowe na samia watapata mshtuko mkubwa saa kwa sababu watakosa kura na pesa zitaliwa na hakuna wa kumdai.

2025 Mbowe hata akishindwa Lisu anaweza kupata kura nyingi sana bila Msaada wa mbowe lakini Mbowe bila msaada wa Lisu hana kitu na atapoteza kura nyingi . Chadema ya Mbowe haiwe kupata zaidi ya kura laki mbili nchi nzima uchaguzi ujao wa ngazi ya urais
 
Lisu anaungwa mkono na watu gani vile? Kwamba Lisu alishinda uenyekiti CCM watafurahi sio?

Hapana lengo siyo ashinde bali ni kuongeza mtifuano tu kati yake na mwenyekiti hapo ndipo wanapopenda ndiyo maana wanampa support ili azidi kumyuka Mwamba.
 
Hata na yeye ni mla rushwa , michango ya matibabu wamechanga viongozi wa chadema na wanacnhi ila invoice amezidai zote 800m kama zake huo ni wizi/utapeli kukosa uhadilifu.
Mkuu hapa haujaeleweka, hii ni rushwa kivipi? Yaani mwanetu anaumwa yupo MNH tumemchangia. Akitaka kupewa risiti na invoice za malipo unataka lisome jina la nani? Unataka yasomeke majina yetu?
 
Back
Top Bottom