Pre GE2025 Freeman Mbowe: Dkt. Slaa na wanaojiita Tanzania Diaspora wanapanga kufanya mapinduzi ndani ya CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mkuu hapa haujaeleweka, hii ni rushwa kivipi? Yaani mwanetu anaumwa yupo MNH tumemchangia. Akitaka kupewa risiti na invoice za malipo unataka lisome jina la nani? Unataka yasomeke majina yetu?
Wenje alimwambia kwamba kuna michango watu walitoa inabidi warudishiwe including na yeye mwenyewe wenje akagoma...invoice itaenda kwa jina lake lissu ila aligoma kurudisha baadhi ya fedha za viongozi walizotoa kwenye account zao.
 
Mkuu hiyo ni michango au mikopo? Michango huwa inarudishwa?
 
Wenje alimwambia kwamba kuna michango watu walitoa inabidi warudishiwe including na yeye mwenyewe wenje akagoma...invoice itaenda kwa jina lake lissu ila aligoma kurudisha baadhi ya fedha za viongozi walizotoa kwenye account zao.
Inawezekana kuna watu walikopa ili wamchangie. Ndio maana Mbowe alitingisha kichwa lilipokuja suala la michango. Hata alipoenda kulipia fomu alisema hatatumia alizochangiwa kwa sababu Sativa amemlipia. Mimi sijasikia alichangiwa ngapi! Michango ya gari ilikuwa inaenda kimya kimya bila updates. Taarifa ya juu ilitoka baada ya kuyangaza nia.Huo uwazi katika masuala ya fedha ni upi?

Amandla...
 
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA @chadematzofficial Freeman Mbowe amesema kuna makundi yanayoratibu kufanyika mapinduzi ndani ya chama hicho na makundi hayo ndiyo yanayomsukuma Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Bara, Tundu Lissu kugombea nafasi ya Uenyekiti.

“Kuna kundi linaloitwa diaspora (watanzania waishio ughaibuni) ni kundi dogo tu wala sio kusema ni diaspora wote wa Tanzania hili kundi dogo linalojaribu kupanga mapinduzi ndani ya CHADEMA wengine hata hatuwajui tunawaona tu kwenye majina ya mitandaoni wanajiita Tanzania Diaspora ni kundi ndani ya Diaspora”

Mbowe ameeleza kuwa zaidi ya kundi hilo kuna kikundi kingine kinachoitwa Sauti ya Watanzania ambacho kinachoongozwa na aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho Dkt. Wilbroad Silaa

“Kuna makundi ya watu kama Dkt. Silaa na kikundi kinachojiita Sauti ya Watanzania, Dkt. Silaa alikimbia CHADEMA mwenyewe akaenda Chama Cha Mapinduzi (CCM) akafungiwa Serena pale(Serena Hotel) baadae akahamishiwa Canada akapewa zawadi ya ubalozi.”

Mbowe ameongeza kuwa amekuwa akishangazwa na wanaomuunga mkono Lissu kuwa sio watu ambao ni wanachama kweli kweli hata hivyo anashindwa kuelewa kwa nini Dkt. Silaa hawekezi nguvu kwenye chama chake bali anawekeza muda na nguvu CHADEMA.

“Kazi aliyoifanya muda wote akiwa balozi(Dkt.Silaa) chini ya utawala wa Magufuli(Hayati Dkt. John Pombe Magufuli) ni kujaribu kuichonganisha CHADEMA na kutoa taarifa na mpaka kuandika kitabu cha uongo eti leo Dkt.Silaa ndiye anafanya kampeni ya Lissu kuchukua uongozi wa chama alisahau nini Dkt Silaa ambacho leo anakitaka”

Hata hivyo Mbowe ameongeza kuwa wengine wanaomuunga mkono Lissu ni pamoja na aliyekuwa Mbunge wa Iringa na Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Mchungaji Peter Msigwa ambaye kwa sasa ni kada wa CCM.

Source: Jambo TV

Leo hii freeman hajui tofauti ya mapinduzi na uchaguzi? Huyu mangi atakufa kwa presha. Kuna damu za watu zinamlilia. Atajuta!

kinachoendelea cdm ni harakati za kufanyika uchaguzi, yeye anasema ni mapinduzi. mliyeko karibu naye mshikeni asi commit suicide
 
Hapana lengo siyo ashinde bali ni kuongeza mtifuano tu kati yake na mwenyekiti hapo ndipo wanapopenda ndiyo maana wanampa support ili azidi kumyuka Mwamba.
Mkuu, huu ni mtazamo wako, Lisu toka wakati anagombea hakumuattack Mbowe, aliweka hoja zake alizoelezea kuwa zimemsukuma kugombea, hata jana kasisitiza m/kiti hakutaka agombee chochote kati ya urais na uenyekiti na hii ni baada ya Mbowe kudanganya, sasa hivi mwamba anafanya personal attack kwa TAL na TAL hajamuattack wala kumtusi.
 
Leo hii freeman hajui tofauti ya mapinduzi na uchaguzi? Huyu mangi atakufa kwa presha. Kuna damu za watu zinamlilia. Atajuta!

kinachoendelea cdm ni harakati za kufanyika uchaguzi, yeye anasema ni mapinduzi. mliyeko karibu naye mshikeni asi commit suicide
Itakuwa anapumulia mashine
 
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA @chadematzofficial Freeman Mbowe amesema kuna makundi yanayoratibu kufanyika mapinduzi ndani ya chama hicho na makundi hayo ndiyo yanayomsukuma Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Bara, Tundu Lissu kugombea nafasi ya Uenyekiti.

“Kuna kundi linaloitwa diaspora (watanzania waishio ughaibuni) ni kundi dogo tu wala sio kusema ni diaspora wote wa Tanzania hili kundi dogo linalojaribu kupanga mapinduzi ndani ya CHADEMA wengine hata hatuwajui tunawaona tu kwenye majina ya mitandaoni wanajiita Tanzania Diaspora ni kundi ndani ya Diaspora”

Mbowe ameeleza kuwa zaidi ya kundi hilo kuna kikundi kingine kinachoitwa Sauti ya Watanzania ambacho kinachoongozwa na aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho Dkt. Wilbroad Silaa

“Kuna makundi ya watu kama Dkt. Silaa na kikundi kinachojiita Sauti ya Watanzania, Dkt. Silaa alikimbia CHADEMA mwenyewe akaenda Chama Cha Mapinduzi (CCM) akafungiwa Serena pale(Serena Hotel) baadae akahamishiwa Canada akapewa zawadi ya ubalozi.”

Mbowe ameongeza kuwa amekuwa akishangazwa na wanaomuunga mkono Lissu kuwa sio watu ambao ni wanachama kweli kweli hata hivyo anashindwa kuelewa kwa nini Dkt. Silaa hawekezi nguvu kwenye chama chake bali anawekeza muda na nguvu CHADEMA.

“Kazi aliyoifanya muda wote akiwa balozi(Dkt.Silaa) chini ya utawala wa Magufuli(Hayati Dkt. John Pombe Magufuli) ni kujaribu kuichonganisha CHADEMA na kutoa taarifa na mpaka kuandika kitabu cha uongo eti leo Dkt.Silaa ndiye anafanya kampeni ya Lissu kuchukua uongozi wa chama alisahau nini Dkt Silaa ambacho leo anakitaka”

Hata hivyo Mbowe ameongeza kuwa wengine wanaomuunga mkono Lissu ni pamoja na aliyekuwa Mbunge wa Iringa na Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Mchungaji Peter Msigwa ambaye kwa sasa ni kada wa CCM.

Source: Jambo TV
Kiufupi tu, Chadema wakimruhusu awe Mwenyekiti wao, hawataamini kuwa yeye ndiye na Mbowe sie!
 
Sasa kuna tofauti gani kati ya huyu Mbowe na let say... Kangi Lugola, ni Mtanzania gani atamkomboa Mtanzania mwingine wakati wote hawatofautiani?!

Angalao Mungu katuletea Lissu na Heche wako tofauti nawaasa Wajumbe kama mnataka kuingia kwenye vitabu vya historia ya ukombozi wa Mtanzania basi tupeni LISSU na HECHE msiiachie hii CHANCE 🔥🔥🔥🔥 🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿
 
Mbowe hana tofauti na huyu Francis Atwoli ambaye amekuwa katibu wa chama cha wafanyakazi kenya[ COTU] tangu 2001 .

Amefanya kazi chini ya marais 4 , Daniel Arap Moi, Emilio Mwai Kibaki, Uhuru Kenyatta , na William Samoei Ruto.

Huyu mzee amekuwa ni fisadi wa kutupwa na hana msaada kwa wafanyakazi

Kila wanapomuuliza lini ataachia ngazi analeta stori kama za Mbowe kuwa nafasi yake ni ya kuchaguliwa hivyo watu wanamuhitaji bado na "wanamuomba agombee" kila akisema anastaafu.

Yaani kiongozi unakilia ofisi miaka 24 hakuna jipya na bado unasema watu wanakuomba ugombee wakati wafanyakazi wanaonewa na migomo haiishi kila mwaka?
images - 2025-01-07T220355.750.jpeg
 
Hana hekima za kuhuburi demokrasia wakati yeye haongozi kidemokrasia anakumbuka kuhusu demokrasia anapokuwa nyuma ya mikamera hasa wakati wa chaguzi
MBOWE ni mnafiki na mjasiriamali anayetumia platform ya siasa kujitajirisha akituhadaa kuwa ni mwanahakati aliyejivisha kinyago cha uzalendo.........

Mimi tangu tukio la kuchange gia angani na kumleta Lowasa CHADEMA dakika za jioni kabisa.....nikajua tu huyu ndugu yetu kwenye siasa za Tanganyika ana jambo lake....
 
Huahirisha kufikiri kwa nafsi a k.a kujizima data
 
Back
Top Bottom