Pre GE2025 Freeman Mbowe: Dkt. Slaa na wanaojiita Tanzania Diaspora wanapanga kufanya mapinduzi ndani ya CHADEMA

Pre GE2025 Freeman Mbowe: Dkt. Slaa na wanaojiita Tanzania Diaspora wanapanga kufanya mapinduzi ndani ya CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mkuu hiyo ni michango au mikopo? Michango huwa inarudishwa?
Ulimsikiliza Wenje vizuri? Kuna fedha alitoa za michango kutoka mfukoni mwake ili baadae zije kurudishwa maana aliamini kwamba zitakuja kurudishwa na bunge then kupewa yeye...Kuna baadhi ni michango ya wananchio haitorudishwa na mingine michango lakini ilitakiwa irudi pale bunge liki-refund.
 
Dr Slaa nilikuwa naye Kamati ya Mapokezi ya Papa Yohanne Paul Mimi nilikuwa kituo cha Luhuwiko Songea

Ni Mtu makini Sana 😂😂😂
Mtu makini asingetusaliti wakati wa vita ya kuiondoa CCM mwaka 2015, badala yake akahamia huko na kuanza vita ya chini kwa chini ya kutaka kuibomoa CHADEMA, amesahau nini? Kwa nin asibaki huko huko alikonunuliwa?
 
Mbowe ni mfamaji mwacheni atapetape mpumbav yule, hivi akifa hicho chadema nacho kitakufa siku hiyohiyo au mbona amekuwa king'ang'anizi sana ana hoja za kijinga ambazo hazina mashiko
 
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA @chadematzofficial Freeman Mbowe amesema kuna makundi yanayoratibu kufanyika mapinduzi ndani ya chama hicho na makundi hayo ndiyo yanayomsukuma Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Bara, Tundu Lissu kugombea nafasi ya Uenyekiti.

“Kuna kundi linaloitwa diaspora (watanzania waishio ughaibuni) ni kundi dogo tu wala sio kusema ni diaspora wote wa Tanzania hili kundi dogo linalojaribu kupanga mapinduzi ndani ya CHADEMA wengine hata hatuwajui tunawaona tu kwenye majina ya mitandaoni wanajiita Tanzania Diaspora ni kundi ndani ya Diaspora”

Mbowe ameeleza kuwa zaidi ya kundi hilo kuna kikundi kingine kinachoitwa Sauti ya Watanzania ambacho kinachoongozwa na aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho Dkt. Wilbroad Silaa

“Kuna makundi ya watu kama Dkt. Silaa na kikundi kinachojiita Sauti ya Watanzania, Dkt. Silaa alikimbia CHADEMA mwenyewe akaenda Chama Cha Mapinduzi (CCM) akafungiwa Serena pale(Serena Hotel) baadae akahamishiwa Canada akapewa zawadi ya ubalozi.”

Mbowe ameongeza kuwa amekuwa akishangazwa na wanaomuunga mkono Lissu kuwa sio watu ambao ni wanachama kweli kweli hata hivyo anashindwa kuelewa kwa nini Dkt. Silaa hawekezi nguvu kwenye chama chake bali anawekeza muda na nguvu CHADEMA.

“Kazi aliyoifanya muda wote akiwa balozi(Dkt.Silaa) chini ya utawala wa Magufuli(Hayati Dkt. John Pombe Magufuli) ni kujaribu kuichonganisha CHADEMA na kutoa taarifa na mpaka kuandika kitabu cha uongo eti leo Dkt.Silaa ndiye anafanya kampeni ya Lissu kuchukua uongozi wa chama alisahau nini Dkt Silaa ambacho leo anakitaka”

Hata hivyo Mbowe ameongeza kuwa wengine wanaomuunga mkono Lissu ni pamoja na aliyekuwa Mbunge wa Iringa na Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Mchungaji Peter Msigwa ambaye kwa sasa ni kada wa CCM.

Source: Jambo TV
Kama uchaguzi ni mapinduzi, mwache tu apinduliwe hakuna namna. Anataka awe mwenyekiti wa maisha? Mbona yeye anapigiwa chapuo na CCM hatusemi au naye alisahau ninj CCM? CHADEMA sio mali yake na ukoo wake tu. Ni mali ya watanzania. Akae atulie sundano zimuingie, aache kuweweseka.
 
Mkuu hiyo ni michango au mikopo? Michango huwa inarudishwa?
Lissu na Maria Sarungi walitudanganya wee tukachanga na kuchanga eti tumnunulie gari, gari lenyewe hakununua wala nini na hao Diaspora kama wanampenda walishindwa hata kumtumia gari? Katumwa tu kutuvuruga
Mkuu hiyo ni michango au mikopo? Michango huwa inarudishwa?
 
Ni wakati wake wa kupumzika kwa heshima, Ameitoa mbali CHADEMA na ameifanyia mengi
Unapumzika unapopata mtu sahihi wa kukiongoza chama sio Lissu aisee, jamaa ataiua Chadema makusudi. Ni kama vile Wakili Mwabukusi alivyopewa TLS kwa mihemko tu kisa mropokaji, hadi sasa amefanya nini sana sana sijui nae kapewa asali maana kimyaaaa, watu wanatekwa, watatoweka, wanapewa kesi za ajabu ajabu hachukui hatua kisa tu anasema eti TLS haina hela za kuzifikia kesi zote kwani akitoa mwongozo wa sheria watu watashindwa kuchanga?
 
Mkuu, huu ni mtazamo wako, Lisu toka wakati anagombea hakumuattack Mbowe, aliweka hoja zake alizoelezea kuwa zimemsukuma kugombea, hata jana kasisitiza m/kiti hakutaka agombee chochote kati ya urais na uenyekiti na hii ni baada ya Mbowe kudanganya, sasa hivi mwamba anafanya personal attack kwa TAL na TAL hajamuattack wala kumtusi.
Lissu ni mwanasheria kwa hiyo hataki kushikwa red handed. Anatumia sana surrogates wake ndio maana hautamsikia hata siku moja akimkanya Msigwa. Hii ni kwa sababu Msigwa anasema yale ambayo yeye hawezi kusema.

Mfano mwingine ni pale Lissu aliposema Abduli alimtajia watu wanaopokea mshiko kutoka kwake bila kuwataja majina. Lakini ukifikiri ni jina la nani linaweza kutumika ili kum convince Lissu kuwa ni salama kupotea utagundua ni la Mwenyekiti wake tu.

Mwingine, ni hapa juzi tu, Lissu amesema kuna watu wanachangia sana lakini hata TIN za biashara zao au ofisi zao hazijulikani. Unadhani alikuwa anamzungumzia nani na alikuwa ana maanisha nini kama sio kuwa hizo pesa ni pesa chafu?

Lissu ametangaza mapema sana kuwa atagombea urais. Sijamsikia Mbowe akimkataza. Alichokisema Lissu ni kuwa yeye Lissu alipendekeza yeye agombee uenyekiti na Mbowe urais lakini Mbowe akasema ni mapema mno yeye kufikiria kugombea urais. Kusema hivyo ndio kumzuia Lissu kugombea urais?

Kwenye suala la Uenyekiti, kuna ubaya gani Mbowe kumshauri Lissu agombee Umakamu Mwenyekiti na sio Uenyekiti? Kwangu mimi ni ushauri mzuri tuu maana bado Lissu ana nafasi ya kugombea Uenyekiti mwaka 2030. Wangefanya hivyo wangeepusha mpasuko katika chama. Pamoja na hayo Lissu alikuwa na haki kukataa na kusema interest yake ni Uenyekiti na sio uRais ingawa sitashangaa hapo mbeleni akikazia nia ya kugombea urais hata kama alikubaali kuwa hio nafasi igombewe na Mbowe.

Ninachokiona hapa ni kuwa Lissu hataki ushindani. Alitangaza nia ya kugombea urais mapema ili kuwafanya wale ambao walikuwa na nia kama hiyo kusita. Na kuzuia mpango wowote wa kutafuta mgombea kutoka nje ya chama.

Lissu amesema kuwa ameamua kugombea uenyekiti kwa sababu anaamini Mwenyekiti alimtuma Wenje kum challenge kwenye nafasi ya umakamu Mwenyekiti. Hayo ya ukomo, uwazi katika uendeshaji wa chama n.k. yalikuja baadae. Wenje asinge mchallenge angeendelea kumuunga Mwenyekiti hadharani na kusema kila kitu ni safi.

Hata Heche amesema kuwa Wenje ndie aliyekifikisha chama hapa kilipo.
Lissu hataki challenge yeyote. Anapenda kuzungukwa na sycophants ambao hawatamchallenge. Na siku hao wakina Heche wakianza kumhoji atawatupa chini ya basi.

Amandla..
 
Ulimsikiliza Wenje vizuri? Kuna fedha alitoa za michango kutoka mfukoni mwake ili baadae zije kurudishwa maana aliamini kwamba zitakuja kurudishwa na bunge then kupewa yeye...Kuna baadhi ni michango ya wananchio haitorudishwa na mingine michango lakini ilitakiwa irudi pale bunge liki-refund.
Alikubalina na nani kipindi anachanga kua zitarudishwa?.
 
Lissu ni mwanasheria kwa hiyo hataki kushikwa red handed. Anatumia sana surrogates wake ndio maana hautamsikia siku moja akimkanya Msigwa. Anasema Abduli alimtajia watu wanaopokea mshiko kutoka kwake bila kuwataja. Lakini ukifikiri ni jina la nani linaweza kutumika ili kum convince Lissu kuwa ni salama kupotea utagundua ni Mwenyekiti wake tu. Juzi amesema kuna watu wanachangia sana lakini hata TIN za biashara zao au ofisi zao hazijulikani. Unadhani alikuwa anamzungumzia nani na alikuwa ana maanisha nini kama sio hizo pesa ni pesa chafu?

Lissu ametangaza mapema sana kuwa atagombea urais. Sijamsikia Mbowe akimkataza. Alichokisema Lissu ni kuwa yeye Lissu alipendekeza yeye agombee uenyekiti na Mbowe urais lakini Mbowe akasema ni mapema mno yeye kufikiria kugombea urais. Kusema hivyo ndio kumzuia Lissu kugombea urais?

Kwenye suala la Uenyekiti, kuna ubaya gani Mbowe kumshauri Lissu agombee Umakamu Mwenyekiti na sio Uenyekiti? Kwangu mimi ni ofa nzuri tuu maana bado Lissu ana nafasi ya kugombea Uenyekiti mwaka 2030. Wangefanya hivyo wangeepusha mpasuko katika chama. Pamoja na hayo Lissu alikuwa na haki kukataa na kusema interest yake ni Uenyekiti na sio uRais ingawa sitashangaa hapo mbeleni akikazia nia ya kugombea urais.

Ninachokiona hapa ni kuwa Lissu hataki ushindani. Alitangaza nia ya kugombea urais mapema ili kuwafanya wale ambao walikuwa na nia kama hiyo kusita. Na kuzuia mpango wowote wa kutafuta mgombea kutoka nje ya chama.

Lissu amesema kuwa ameamua kugombea uenyekiti kwa sababu anaamini Mwenyekiti alimtuma Wenje kum challenge kwenye nafasi ya umakamu Mwenyekiti. Hayo ya ukomo, uwazi katika uendeshaji wa chama n.k. yalikuja baadae. Wenje asinge mchallenge angeendelea kumuunga Mwenyekiti hadharani na kusema kila kitu ni safi.

Hata Heche amesema kuwa Wenje ndie aliyekifikisha chama hapa kilipo.
Lissu hataki challenge yeyote. Anapenda kuzungukwa na sycophants ambao hawatamchallenge. Na siku hao wakina Heche wakianza kumhoji atawatupa chini ya basi.

Amandla..
Mbowe anapenda watu wa kum Challenge?. Kwa nini anaita wanaogombea uwenyekiti wanataka kumfanyia Mapinduz?.
 
Nikiwaambia Lisu ni kibaraka Huwa qanabisha
Mbowe ni mamluki na kibaraka wa Samia! Yuko radhi Chadema ife lakini mradi yeye asiukose uenyekiti!!
Mbowe ni adui wa maendeleo ya Chadema na Tanganyika kwa ujumla wake.
Samia na.ccm wanatumia fedha nyingi kumfadhiri Mbowe aendelee kuwa Mwenyekiti lakini wanashindwa kumpa ndiko za Mbowe kama walivyoshindwa kumpandikiza mtu wao kuongoza TLS
 
Mbowe ni mamluki na kibaraka wa Samia! Yuko radhi Chadema ife lakini mradi yeye asiukose uenyekiti!!
Mbowe ni adui wa maendeleo ya Chadema na Tanganyika kwa ujumla wake.
Mbowe angekuwa adui wa Chadema wala isingefika mwaka huu, ingejifia tangu Magu alivyoingia madarakani maana aliahidiwa kila kitu aachane na upinzani lakini akakataa, Lissu katumwa kidogo tu na kuonyeshwa hela na Diaspora kaingia kingi
 
Bora Chadema Kufa kuliko kuacha chama Kwa vibaraka wa Mabeberu na diaspora uchwara.

Chama ni Cha kwake,na nyie kaanzisheni vyenu, kibaraka Lisu si yupo anakubalika au? 😁😁
 
Mbowe angekuwa adui wa Chadema wala isingefika mwaka huu, ingejifia tangu Magu alivyoingia madarakani maana aliahidiwa kila kitu aachane na upinzani lakini akakataa, Lissu katumwa kidogo tu na kuonyeshwa hela na Diaspora kaingia kingi
Mbowe hana tena nguvu ya kuendeleza Chadema he is exhausted ,, hana jipya!! Atumie busara apumzike awe mshauri wa chama kama walivyo kuwa watangulizi wake akiwemo mkwe wake Mzee Edwin Mtei na marehemu Makani!! Kung’ang’ania kuendelea na uenyekiti kutamvunjia heshima ndogo aliyobaki nayo!
 
Tundu Lissu ana jipya gani zaidi ya kufokafoka na kuropoka hata asiyoyajua?
 
Tundu Lissu ana jipya gani zaidi ya kufokafoka na kuropoka hata asiyoyajua?
Mbowe is compromised by the ccm system but Tundu Lissu is not and that’s the reason ccm and its system is spending a lot of money in support of their stooge Mbowe.
 
Mbowe is compromised by the ccm system but Tundu Lissu is not and that’s the reason ccm and its system is spending a lot of money in support of their stooge Mbowe.
Hujui kitu, anayesapotiwa sasa ni Lissu ili wamtoe Mbowe Chadema ife baada ya kujaribu kila njia kummaliza Mbowe na kumshindwa. Waliua biashara zake, wakaua mashamba yake wakazuia akanti zake lakini mwamba akawa imara kukilinda chama. Wameona sasa wamtumie Lissu kwa mlango wa mbaaali sana, wewe huwezi kuuona kwa sasa, ili amvuruge Mwenyekiti chama kife halafu malengo yao yatimie, wagonge glasi na kujipongeza
 
Back
Top Bottom