MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Hii kauli ni kufuru. Lissu kupona ni miujiza ya Mungu na sio Mbowe wala mwanadamu mwingine yeyote. Pia mchakato wa kumtoa Lissu Dodoma hadi Nairobi ulihusisha watu wengi sana na sio Mbowe tu. WanaCCM wengi tu walishiriki kumkimbiza Lissu hospitalini. Kauli ya Mbowe kuwa aliokoa uhai wa Lissu ni kauli ya kipuuzi mno.
Mbowe kama kiongozi mkuu wa CHADEMA hakuwa na jinsi ya kukwepa jukumu la kuhakikisha Lissu anapata huduma. Macho ya watu wote yalikuwa kwake. Alichofanya ni moja ya majukumu yake na sio lazima atake fadhila kwa Lissu.
Tatizo huyu mtu anaangalia kila kitu kama fursa ya biashara. Ni aibu kwake na Wenje kuanza kusema kuna hela wanamdai Lissu kwa kumsaidia kwenye matibabu yake.
Ninamsihi Sultani Mbowe ajaribu kujenga hoja za kisomi badala ya kuachia hoja za kipuuzi kama mpambe wake Yericko.