Loh🤔🤔..!
MamaSamia2025 umepatwa na nini leo? Unamtetea Tundu Lissu na kumponda Freeman Mbowe..?
Hii nimeipenda na kumbe wewe ni mwanasiasa lakini pia una unaujua na kuthamini utu na ubinadamu wa mtu...
Freeman Mbowe ktk fyongo zote, hili amechemka na kutia aibu big time...
Na cha ajabu tunaambiwa huyu ndiye mtu aliye na busara eti? Hivi kwa kipimo cha kawaida mtu mwenye busara anaweza hata kufikiria tu kupanua mdomo wake kusema maneno haya kweli..???
Hivi tujiulize pia kuwa, hivi, yote haya ni kwa sababu ya uenyekiti wa CHADEMA tu ambao kazi yenyewe wanadai huwa ni ya kujitolea tu?
Au Freeman Mbowe ana kitu kingine amekichimbia hapa CHADEMA na hivyo bado anahangaika kukichimbua..?
Kama ni pesa wanamdai Tundu Lissu hebu na waseme ni shilingi ngapi na uhalali wa deni hilo umekaaje ili tumchangie Tundu Lissu awalipe hawa hayawani waache ujinga wao...