Freeman Mbowe kusema aliokoa maisha ya Tundu Lissu ni kauli ya kufuru na ya ovyo

Maneno mazito sana,hakika wewe ni miongoni mwa watu wachache JF wenye akili kubwa.
 
Na alie toa chopa ni mwanaccm tena wa visiwani na nadhani ashatangulia mbele za haki. Mengine anazidi kujionesha kuwa akimsaidia mtu basi hataki huyo mtu amzidi kwa lolote. Bi aibu na inamshushia heshima aliyoyojijengea kwa miaka
 
Ni aibu kwake na Wenje kuanza kusema kuna hela wanamdai Lissu kwa kumsaidia kwenye matibabu yake.
Inakuwaje aibu kusema hela unayoidai kwa mtu?
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imeanzisha mpango wa kuwafichua wadaiwa wake. Je, hiyo ni aibu kwa Bodi na serikali?

 
Kwanini Mbowe awatume wapambe wake kumshambulia Lissu?
 
Inakuwaje aibu kusema hela unayoidai kwa mtu?
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imeanzisha mpango wa kuwafichua wadaiwa wake. Je, hiyo ni aibu kwa Bodi na serikali?

View attachment 3195815
Ni aibu kubwa kwa HESLB. Hawana rekodi za wadaiwa wao? Wanashindwa nini kuwasiliana na NIDA, TRA, Immigration, RITA na mamlaka zingine ili kujua wadaiwa wao walipo?
 
Mbowe ana upep mdogo sana wa kufikiri
 
Mimi binafsi Lissu alipopigwa Risasi niliumia sana hata nilimpigia simu Mchungaji wangu Ili amwombee Lissu, lakini Mbona sijawahi kumsikia Lissu popote akitamka kuwa anamshukuru Mungu Kwa kumuokoa?

Zaidi ya kusikia "hatuwezi kuingilia faragha", kinyume na maagizo ya Mungu?
 
Napigilia Msumari..."Lissu kupona ni miujiza ya Mungu na sio Mbowe wala mwanadamu mwingine yeyote." Hilo tu ndilo watu wanashupaza Shingo na kukataa kulijua.
 
Tuweke mambo ya siasa pembeni, ukweli ni kwamba Mbowe aliokoa maisha ya Lissu na asingewahishwa Kenya angemaliziwa hata kwa sindano ya simu.
Binadamu huokoana, huuana, hutiana matatizoni nk. Upumbavu wa kumuhusisha huyo Mungu(imaginary supernatural 'thing') katika kila jambo inamaana hata ajali za barabarani, vifo vya kina mama wakati wa kujifungua hupangwa na Mungu.
 
Swali kwako mkuu. Ukisaidiwa huna haki ya kujipambania zaidi hata kumchallange alie kisaidia..? Ni jambo baya na ovu kuona mtu fulani hastahili kupingwa
 
Pia watu wakisha kujua kuwa hushauriki na hutaki kuachia cheo husika lazma watafute mbinu. Si amini kuwa lissu yupo peke yake. Kuna vigogo wengi tu na wanachadema wengi tu hawamtaki mbowe kwa sasa na ipo wazi aina ya siasa zake kwa sasahazina maajabu tena
 
Sasa wewe K ulitaka kiongozi mkuu wa chama afanye nini kama sio kuhakikisha mwanachama wake anakuwa salama?
Sasa mbona unajijibu mwenyewe? Unalalamika nini sasa kwa Mbowe kudai aliokoa maisha ya Lisu?
 
Ulisikia popote Mbowe akiyasema hayo uliyoyaandika? au ndiyo style ya kuweweseka huku tarehe za BOX kusogea ukumbini zikiwadia.
 
Mbowe alifanya yote na CCM only few, walifanya yote na Kenya walifanya yote na Ubelgiji walifanya yote na familia walifanya yote kuokoa maisha yake na hakuna anayepaswa kudai. Mbona Samia alikuja Nairobi kumsalimia, lakini kisiasa Lissu bado anamkosoa vilevile.
 
Hii ndio maana ya "Tenda Wema uende zako....!"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…