Muda huu M/Kiti wa CHADEMA na viongozi waandamizi 9 wa chama hicho wapo Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.
Tutarajie jambo gani jipya? Ndo ukurasa mpya wa Siasa za Tanzania?
UPDATE:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameongoza Kikao cha majadiliano pamoja na Viongozi Wakuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Ikulu Chamwino Jijini Dodoma tarehe 20 Mei, 2022.
Baadhi ya Viongozi wa CHADEMA waliohudhuria Kikao hicho ni Mwenyekiti Freeman Mbowe, Makamu Mwenyekiti Zanzibar Saidi Issa Mohamed, Katibu Mkuu wa Chama hicho John Mnyika pamoja na Baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu na Sekretarieti ya Chama hicho.
Itakuwa wanataka kuachana na ile kesi ya mchongo ya Kina Mdee. Au wanataka kufikia muafaka kabla ya haya makongamano ya Katiba mpya yanayotakiwa kuanza.
Tangu Mbowe aanze kwenda huko hakuna hata jambo moja lililowahi kufanyiwa kazi na serikali, sijui ugumu wa Samia kufanya hivyo unatoka wapi, na sijui uvumilivu wa Mbowe utaendelea mpaka lini, naona utani unazidi.
- Lissu bado hajarudi nchini, hii inawezekana bado hajahakikishiwa usalama wake.
- Mikutano ya vyama vya siasa bado haijaruhusiwa japo ni takwa la kisheria.
- Wale wahujumu uchumi 19 bado wanakumbatiwa na Spika kule bungeni kinyume cha sheria.
Tindo mbonà unaniweka angle nyingine with regard to your credibility on JF. Mandela alizungumza na De Klerk akiwa gerezani and mazungumzo beared some positive results, ngoja wamsikilize. Mtu hakatai wito hukataa analoitiwa
Katiba mpya itoke wapi? We endelea kufanywa mpira wa dana dana huku mwenyekiti na genge lake wakiendelea kuupiga mwingi kupitia mialiko ya raisi. Mmeshaambiwa siku zote hakuna mkate mgumu mbele ya chai. Jamaa anatengeneza pesa ndefu kupitia siasa uchwara, huku akiwaacha watu wenye misimamo thabiti na chama wakiendelea kutokwa mapovu huko belgium na canada. Endelea na kazi ya kuwarubuni wana mbeya ili itapokuwa inaanzishwa michango ya chama wawe mstari wa mbele kukichangia.
Tangu Mbowe aanze kwenda huko hakuna hata jambo moja lililowahi kufanyiwa kazi na serikali, sijui ugumu wa Samia kufanya hivyo unatoka wapi, na sijui uvumilivu wa Mbowe utaendelea mpaka lini, naona utani unazidi.
- Lissu bado hajarudi nchini, hii inawezekana bado hajahakikishiwa usalama wake.
- Mikutano ya vyama vya siasa bado haijaruhusiwa japo ni takwa la kisheria.
- Wale wahujumu uchumi 19 bado wanakumbatiwa na Spika kule bungeni kinyume cha sheria.
Mkuu chadema ya sasa chini ya mwenyekiti wake itakupa presha ya bure. Jamaa anaangalia kwanza masilahi yake na ya familia yake, nyinyi wengine mmeachwa mtetee chama tu mitandaoni. Wengi mtaishia kulalamika tu lakini hamna ujanja wa kumfanya chochote.