Freeman Mbowe, Mnyika na Viongozi CHADEMA wakutana na Rais Samia na Viongozi wa CCM Ikulu ya Chamwino - Dodoma leo 20/5/2022

Freeman Mbowe, Mnyika na Viongozi CHADEMA wakutana na Rais Samia na Viongozi wa CCM Ikulu ya Chamwino - Dodoma leo 20/5/2022

.... Dah; Mbowe kulikoni tena? Mbona unasaliti mageuzi?
 
,[emoji116]
Walienda ikulu kujadili nini kama sio siasa za kinafiki wakati CCM haifai kabisa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza Kikao cha majadiliano ya pamoja na Viongozi Wakuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakiongozwa na mwenyekiti wa Chama Mhe. @freemanmbowetz, Ikulu Chamwino Jijini Dodoma tarehe 20 Mei, 2022. https://t.co/fHyVu2FDaf
View attachment 2232222
Subiri atatuletea mrejesho, kuanza kutukana nikukosa busara
 
Sawa haifai ebu njoo na solution tunafanyeje
 
Ata timu pinzani zinakutana uwanja mmoja na kucheza dakika tisini. Huwezi kuita usaliti kwenda kucheza na timu pinzani.

Huu ni mzunguko wa siasa
 
Mbowe awe makini, CCM sio wa kuamini kuwa wanaweza kuweka mazingira yatayoruhusu wao kuachia dola kwa amani.

Anyway, inawezekana strategy ya CHADEMA ni kwanza kutumia meza ya mazungumzo(wasije kulaumiwa kuwa walikataa hiyo fursa), ili kesho na keshokutwa wakitumia mbinu mbadala wasilaumiwe.

Kwa maneno mengine, watayokubaliana yatakuwa documented na kuwa public, hivyo ataenda kinyume, ndio atalaumiwa.

Ni mtazamo wangu.

Ni jambo jema viongozi wakikaa kitako wakazungumza namna ya kutatua mkwamo bila Vita wala mparurano.
 
CHADEMA kutoka kwenye kutekwa na kuteswa Leo mnaramba asali!

Ama kweli baada ya dhiki ni faraja.

Na wewe Kinana kutoka kunyanyapaliwa na kina Musiba Leo unaramba asali!

MEZA IMEPINDULIWA KIBABE!
 
Mbona chadema kama hatujaipromoti sana hii ishu means hatujapenda mtu huru kwenda

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna watu ajira zao zilitegemea malumbano na kuitukana serikali, mtu kama Mdude na Martin Maranja ....Sasa chama hakitawapa posho ya kukaa mtandaoni kutukana, sijui nani katekwa wanaweka hashtag.

Ajira yao inastawi katika mazingira ya migogoro

Muda si mrefu hata maria Sarungi ataukalisha, wanapoteza relevancy, wafadhili hawatampa hela
 
Mbowe awe makini, CCM sio wa kuamini kuwa wanaweza kuweka mazingira yatayoruhusu wao kuachia dola kwa amani.

Anyway, inawezekana strategy ya CHADEMA ni kwanza kutumia meza ya mazungumzo(wasije kulaumiwa kuwa walikataa hiyo fursa), ili kesho na keshokutwa wakitumia mbinu mbadala, wasilaumiwe.

Kwa maneno mengine, watayokubaliana yatakuwa documented na kuwa public, hivyo ataenda kinyume, ndio atalaumiwa.

Ni mtazamo wangu.
Mbinu ya Chadema ni kuionyesha Dunia kwamba Mazungumzo yalishindikana
 
Back
Top Bottom