Freeman Mbowe ndiye mpigania haki maarufu zaidi barani Afrika kwa sasa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426

Gwiji la siasa za Mageuzi Nchini Tanzania Freeman Mbowe, ama Mtemi Isike, Laingwanan au Ustaadh Aboubakar Mbowe kama anavyofahamika huko Zanzibar, sasa anatajwa kama ndiye mpigania haki, demokrasia na uhuru anayeheshimika zaidi barani Africa, wachunguzi wa siasa za dunia wanamuweka Mbowe juu ya Mwl Nyerere, Mandela, Nkurumah na wapigania uhuru wengi wa zamani, kwa vile yeye anapambana na watawala makatili wa kiafrica ambao wamejitwisha udikteta kutokana na kulewa madaraka baada ya kuchukua madaraka kutoka kwa wazungu.


Tukumbuke kwamba kupambana na Mkoloni mweusi ni hatari zaidi kuliko mkoloni mweupe, hii ni kwa sababu wako tayari kukufanya chochote ili waendelee kufaidi utamu wa madaraka ya nchi yaliyojaa neema kibao za marupurupu walizojiwekea wao wenyewe kwa kutumia katiba mbovu walizoziandika wenyewe kwa matakwa yao.



Vitisho vyote hivi kutoka kwa watawala weusi Mbowe anavijua lakini hakuwahi kuogopa wala kusalimu amri, hakuwahi kujidhalilisha wala kusaliti umma unaotaka Uhuru wa kweli kama wafanyavyo Mamluki wengine mnaowafahamu, ambao walipoona vitisho na njaa vinazidi wakaamua kusalimu amri. Hii ndio maana pamoja na kufahamu kwamba watawala wa Tanzania hawataki Katiba mpya wala Tume huru ya uchaguzi na kwamba kama angeendelea kuipigania angeuawa ama kukamatwa na kupewa kesi mbaya lakini hakuogopa.


Wapigania uhuru wa zamani waliungwa mkono na weusi wenzao kwa vile lengo lilikuwa kupata uhuru, lakini kwenye harakati za sasa za Mbowe na Chadema ni kuleta usawa kwenye nchi kwa kuleta katiba itakayowaondoa miungu watu, hii kazi si nyepesi na imejaa mamluki wengi mno, hapa ndipo Mbowe anapokuwa tofauti na wale wa zamani na ndio panapomuweka juu yao, ni hatari sana kufanya siasa kwenye nchi iliyojaa mamluki wanaotega mitego ya usaliti ili walipwe bakhshishi na watawala, hata hivyo Mbowe ameruka vihunzi vyote na kushinda na sasa anapambana na Polisi tu, wanasiasa walio madarakani wanamuogopa vibaya sana.

 
Naunga mkono hoja:

"Tukumbuke kwamba kupambana na Mkoloni mweusi ni hatari zaidi kuliko mkoloni mweupe , hii ni kwa sababu wako tayari kukufanya chochote ili waendelee kufaidi utamu wa madaraka ya nchi yaliyojaa neema kibao za marupurupu walizojiwekea wao wenyewe kwa kutumia katiba mbovu walizoziandika wenyewe kwa matakwa yao."

Kwa maneno ya mzee baba mwenyewe, hawa ni wa kulala nao mbele!
 
Tulishasema hapa Mbowe ni mgumu sana kwenye siasa kwasababu wazee wa Dar-es-salaam wanamuaona kama mtoto wao. Mbowe anajulikana tokea miaka ya 1980's na wamemuona akikuwa na biashara zake leo hii hawawezi kukuelewa ukimwita majina ya ajabu.

Kwa ufupi wanamjua kuliko viongozi wengine wote wa vyama vyote. Kwasababu hii haohao CCM wa Dar ndiyo watakuwa wakwanza kukuchukia na sio hata upinzani. Siasa zina mipaka na hapa serikali imeruka mipaka yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…