Freeman Mbowe: Nimetolewa gerezani kwasababu nguvu ya umma ilikuwa imezidi nguvu ya vyombo vyao vya dola

Freeman Mbowe: Nimetolewa gerezani kwasababu nguvu ya umma ilikuwa imezidi nguvu ya vyombo vyao vya dola

Inawezekana Zitto aliomba Mbowe asamehewe, hata kama ni kuomba kwa unafiki; lakini najua Lissu hawezi kuomba Mbowe asamehewe kwa kosa ambalo halikuwepo.

Viongozi wa dini hawakuomba Mbowe asamehewe. 'Spin' za namna hiyo zielekeze kwa wajinga.
Mbowe kasamehewa na Rais Samia end of story.

Hapo hata ubinuke vipi lakini hiyo inafahamika na kila mtanzania.
 
Kwanza usipotoshe Rais hana mamlaka ya kumsamehe mtu aliye na Kesi inayoendelea,

Mbowe hajatoka kwa msamaha bali ni kukosekana kwa ushahidi wa kutosha kumtia hatiani jambo ambalo lilionekana tangu awali na halikuzingatiwa awali na watoa haki.

Pili mwanasiasa wa kweli anayetimiza wajibu wake ipasavyo asiyekuwa "kanjanja" mtaji wake mkubwa ni nguvu ya umma ambayo hupaza sauti pale anapoonewa.

Wanasiasa wanaopigania matumbo yao hata wakiwa na hoja ya maana na pengine hata wanapoonewa na kubagazwa Wananchi (nguvu ya umma) huweza kunyamaza tu. Mfano ni Ndugai, polepole, nk.
Hiyo n.k., namuweka Zitto... wa miaka hii.
 
Mbowe kasamehewa na Rais Samia end of story.

Hapo hata ubinuke vipi lakini hiyo inafahamika na kila mtanzania.
EeeenHeeeee.

Una maslahi gani na mambo haya mkuu, naona yanakunyima usingizi na kukuondolea amani kabisa akilini mwako.

Inasikitisha sana kuona mtu kama wewe unakuwa 'irrational' hivi. Ina maana umewekeza kila kitu, pamoja na utu wako kiasi hiki!
 
Mbowe kasamehewa na Rais Samia end of story.

Hapo hata ubinuke vipi lakini hiyo inafahamika na kila mtanzania.
Haya ni mawazo yako ama ya ujinga wa sheria au ni mwendelezo wa uhai wa utafiti wa TWAWEZA.

Lakini pia haya unayoyasema hapa hatushangai maana Ndiyo mliyoanza kuyatengeneza baada ya kuona hakuna ushahidi wa maana aibu ikawa inawaandama na mkaanza kutafuta "nitoke vipi" kwa kupitia Zitto, tcd, dini nk.

Hata hivyo mlikutana na uimara wa Mbowe mkaamua kuweka mpira kwapani. Subiri msamaha wa Rais utausikia desemba.
 
ikiwa huku niliko wakazi wake wote wanawaza CCM tu.

Huko uliko kuna wakazi wangapi.!??? au Tanzania yote ipo huko..

Kuna wakati tunafahamu akili hamna sawa,,, ila basi hata macho hamuoni.?
 
Huyu jamaa ni zero brain,ndo maana alipata zero kwenye mtihani wa kidato Cha sita,na Wala asitake kuudanganya umma kuwa eti nguvu ya umma imemtoa kutokana na kupendwa kwake,huyu Ni muuongo mkubwa,watanzania wapi hao wanaompenda ikiwa huku niliko wakazi wake wote wanawaza CCM tu.

Aache Mara moja kuupotosha umma,auambie umma pamoja na wafusi wake kuwa isingekuwa huruma na busara za mama Samia angekufia jela!!
Wale mabalozi wa nchi mbalimbali sio umma wakimataifa?
 
Back
Top Bottom