Freeman Mbowe: Nimetolewa gerezani kwasababu nguvu ya umma ilikuwa imezidi nguvu ya vyombo vyao vya dola

Freeman Mbowe: Nimetolewa gerezani kwasababu nguvu ya umma ilikuwa imezidi nguvu ya vyombo vyao vya dola

Wanasiasa wanajua sana kucheza za saikolojia ya Umma.
 
Sikutolewa gerezani kwasababu kuna mtu ananipenda, nimetolewa gerezani kwasababu nguvu ya umma ilikuwa imezidi sana
Siyo kweli,ni janjajanja tuu ndio iliyopo sasa,hakuna upinzani Bali ni uchumia tumbo tuu kilichopo,UPINZANI MY FOOLSH.....!
 
Kuwapa heshima chadema ukitegemea kupata heshima in return ni kujilisha upepo. Chadema kinafanya siasa kiuanaharakati, na sote tunajua uanaharakati ulivyo!
Unamfunga mtu miezi 8 halafu ukamtoa kwa shinikizo la watu fulani unakuwa umempa heshima? Akushukuru wewe badala ya waliopiga kelele! Akushukuru kwa lipi hali ya kuwa ulimfunga bila hatia?
 
"NGUVU YA UMMA IMENITOA GEREZANI".


CHADEMA hawajawahi kuishiwa na akiba ya mbwembwe na vituko,kiasi kwamba dola ukiwa na roho nyepesi unaweza ukajutia busara yako kwamba kwanini nilifanya busara hii kwa hawa watu ambao hawana busara ya kusema asante!

Ni siku moja tu baada ya kutoka Magereza pale Ukonga, Mwenyekiti wetu wa CDM Taifa kufutiwa mashitaka ya Ugaidi,jana amenukuliwa na vyombo vya HABARI hasa mtandao wa Mwanahalisi online akisema haya.

"NGUVU YA UMMA NDIO IMENITOA GEREZANI KWANI NGUVU YA UMMA ILIIZIDI NGUVU YA DOLA"[emoji1787][emoji13][emoji13][emoji13].

Mwenyekiti Mbowe amesahau jinsi ambavyo juhudi za kaka yangu Mh. Zitto Zuberi Kabwe zilivyoshindikana kumtoa pale Magereza ya Ukonga,anasahau juhudi za wanawake wa CDM ambao walienda kulala ubalozi wa ujerumani wakiwa na mabango pia zilishindwa,anasahau juhudi za Serikali za ulaya zilizopiga kelele na kuja kisutu pia zilishindwa!

Nguvu za umma ni zipi?yaani baada ya siku moja Mzee wangu Mbowe anataka kuwazodoa maaskofu na mashehe wetu walikwenda Ikulu kumuombea MSAMAHA,yaani anasahau kuwa viongozi wa dini hauwezi kuwaita nguvu ya umma?Hawa wanaweza kuitwa "mediators".

Siku moja tu Mzee wangu Freeman Mbowe kabla hata hajafanya kile nilichokisema jana kwenye makala yangu yaani doing a "POLITICAL GROUP APPRECIATION"kabla hajaamua kusema lolote, ameanza kujitapa kuwa nguvu ya "Umma wa CDM" ndio wamechangia kumtoa magereza.

Ni Mzee wangu Mbowe huyu huyu alipokuwa Ikulu juzi alisema anamshukuru Mh.RAIS Samia kwa usikivu!Je,Mbowe anataka kusema nguvu ya umma ndio ilimfanya Mh.RAIS Samia na serikali waachane na kesi Ile?Mbowe anataka kusema Mh.Rais alipigwa sana na pressure mpaka akaamua kufuta kesi so haikuwa busara Bali nguvu ya CDM na watu wao!Khaa![emoji2371][emoji2371]

Mbowe haoni kuwa anaitukana mahakama ya Tanzania?anamtukana RAIS Samia,zaidi anawatukanisha viongozi wangu wa dini?Haoni!

Mzee wangu Freeman Mbowe jana amenukuliwa akisema"nguvu ya umma iliizidi nguvu ya Dola".ndio Maana yupo nje![emoji13][emoji13][emoji13]

Kwa kifupi anataka kusema Dola ya Mama Samia ndio imeshindwa katika vita ile na nguvu ya CDM ndio imeshinda katika kesi ile?Nguvu ipi?

Ni muhimu sana CDM kwa sasa kupima kauli zao dhidi ya Mh.Rais na la muhimu zaidi wajifunze maneno nililolisema jana kwamba wafanye "Appreciation" kabla ya kuja na kuanza kuongea maneno haya!Gharama yake ni kubwa!

Kwa kifupi maneno yao haya yanafunga njia yao ya baadae katika kujenga mahusiano mazuri DHIDI ya Dola!

Nawaza tu,ni ruhusa kunikosoa!

Kwa ule ushahidi wa kipuuzi uliokuwa unatolewa na jamuhuri utaacha kutii nguvu ya umma? Au unadhani kubambikia mtu kesi ni ticketi ya yeye kukugopa? Hivi nyie majizi ya kura mnataka kumtisha nani? Lugha za kujipendekeza na kujinyenyekeza ziko huko ccm ilimpate vyeo.
 
Kwa hiyo ametoka kwa msamaha wa Rais siyo! Au yule Sheikh?

Maana tunacho fahamu sisi wengine ni kwamba DPP aliamua kuweka mpira kwapani ili kuifichia serikali aibu baada ya polisi wasio waaminifu kumbambikia huyo Mheshimiwa kesi ya ugaidi na madawa ya kulevya.
Hii ndio aina ya NYUMBU wa Bomangombe
 
Hizi thread zisizo na source wanazitengeneza hawa wajinga kwa lengo la kuwadanganya wasiojua kufikiria wenye mihemko kama yao.

Hapa ndipo unapoona namna Mbowe anavyowaendesha, sasa wamebaki kuhangaika kama watoto.

Watahangaika sana. Na bado!

Kwani Moses Lijenje @ Mzee Kakobe wameshasema walikompeleka?
 
Huyu jamaa ni zero brain,ndo maana alipata zero kwenye mtihani wa kidato Cha sita,na Wala asitake kuudanganya umma kuwa eti nguvu ya umma imemtoa kutokana na kupendwa kwake,huyu Ni muuongo mkubwa,watanzania wapi hao wanaompenda ikiwa huku niliko wakazi wake wote wanawaza CCM tu.

Aache Mara moja kuupotosha umma,auambie umma pamoja na wafusi wake kuwa isingekuwa huruma na busara za mama Samia angekufia jela!!
Mpuuzi kweli wewe! Huyo mwenyekiti wenu hakufika hata form six na madarasa ya chini alifeli, mbona hulisemi hilo!
Niamini kuwa una degree nne sawa na zile za mwakyembe, zinakusaidiaje kumudu maisha Yako?
Hayo mavyeti ni makaratasi TU yasiyo na umuhimu kwenye maisha halisi, usitambe nayo kwani hayawezi kuwa dhamana ya mkopo benki!
 
Wanafanya kweli makosa ila wanatumia mwamvuli wa kisiasa kupata huruma kama hivi.

We chukulia mfano tu wa kesi hii ya Mbowe angekua mwananchi wa kawaida.

Kuna ambaye angeliga kelele asamehewe??

Au baada ya kusamehewa aitwe ikulu??

Hawa wanasiasa wanajua kucheza tu na akili za wafuasi wao ila kimsingi sio watu safi sana kama tunavyofikiri.
Hii ni lugha ya kilaghai kweli kweli.

Mbowe "KASAMEHEWA"? Kafanya kosa gani hadi asamehewe?

Mnapotosha kwa kutumia lugha za kipuuzi kama hizi kuficha udhaifu na ubovu wa serikali, viongozi na chama cha CCM, halafu mnadhani watu hawana uwezo wa kujuwa upuuzi wenu?
 
Kuwasamehe tu wanasiasa ni kuwakosea pia hata wale ambao sio wanasiasa na wapo magereza bila kuwa na hiyo nguvu ya umma anayosema Mbowe.
Kwanza usipotoshe Rais hana mamlaka ya kumsamehe mtu aliye na Kesi inayoendelea,

Mbowe hajatoka kwa msamaha bali ni kukosekana kwa ushahidi wa kutosha kumtia hatiani jambo ambalo lilionekana tangu awali na halikuzingatiwa awali na watoa haki.

Pili mwanasiasa wa kweli anayetimiza wajibu wake ipasavyo asiyekuwa "kanjanja" mtaji wake mkubwa ni nguvu ya umma ambayo hupaza sauti pale anapoonewa.

Wanasiasa wanaopigania matumbo yao hata wakiwa na hoja ya maana na pengine hata wanapoonewa na kubagazwa Wananchi (nguvu ya umma) huweza kunyamaza tu. Mfano ni Ndugai, polepole, nk.
 
Kwanza usipotoshe Rais hana mamlaka ya kumsamehe mtu aliye na Kesi inayoendelea,

Mbowe hajatoka kwa msamaha bali ni kukosekana kwa ushahidi wa kutosha kumtia hatiani jambo ambalo lilionekana tangu awali na halikuzingatiwa awali na watoa haki.

Pili mwanasiasa wa kweli anayetimiza wajibu wake ipasavyo asiyekuwa "kanjanja" mtaji wake mkubwa ni nguvu ya umma ambayo hupaza sauti pale anapoonewa.

Wanasiasa wanaopigania matumbo yao hata wakiwa na hoja ya maana na pengine hata wanapoonewa na kubagazwa Wananchi (nguvu ya umma) huweza kunyamaza tu. Mfano ni Ndugai, polepole, nk.isu
Hapa anayepotosha ni wewe Mbowe ametoka kwa msamaha ndio maana akakimbia ikulu kwenda kushukuru.

Mnatwist maneno tu hapa ila kila kitu kiko wazi.
 
Hii ni lugha ya kilaghai kweli kweli.

Mbowe "KASAMEHEWA"? Kafanya kosa gani hadi asamehewe?

Mnapotosha kwa kutumia lugha za kipuuzi kama hizi kuficha udhaifu na ubovu wa serikali, viongozi na chama cha CCM, halafu mnadhani watu hawana uwezo wa kujuwa upuuzi wenu?
Ni kweli kasamehewa maana Lisu, Zito na viongozi wa Dini wote walimwomba Rais amsamehe mbowe.

Bila kusamehewa angakula mvua ya kutosha.

Awashukuru viongozi wa dini.
 
Are you sure?

..kwa muda mrefu CCM imewafananisha wapinzani na nyumbu kiasi kwamba inaonekana ni ajabu kwa mpinzani kutendewa jambo la kiungwana na mamlaka.

..Naamini Rais hata kama hajatamka neno samahani, lakini kitendo cha kumualika Mbowe ni ishara kwamba hakubaliani na yaliyomtokea.

..Nchi kuwa na wanasiasa wanaotumikia vifungo ni aibu na kunajisi taswira ya nchi. Sijui kwanini baadhi yetu walikuwa wanafurahia.
 
Onesha
Hapa anayepotosha ni wewe Mbowe ametoka kwa msamaha ndio maana akakimbia ikulu kwenda kushukuru.

Mnatwist maneno tu hapa ila kila kitu kiko wazi.

Hapa anayepotosha ni wewe Mbowe ametoka kwa msamaha ndio maana akakimbia ikulu kwenda kushukuru.

Mnatwist maneno tu hapa ila kila kitu kiko wazi.
Wewe ama ni mpotoshaji mkubwa au mjinga mkubwa wa sheria kwani inaeleweka kuwa wakusamehewa na Rais ni waliokwisha kufungwa,(waliokuwa na hatia) wewe raia gani hata siku za maadhimisho ya uhuru hauoni wala kusikia, nina mashaka na wewe!!!

Nimekwambia sheria haimruhusu Rais kuwasamehe watuhumiwa,

Sasa wewe kama siyo kupotosha onyesha sheria ipi inayomruhu Rais kuwasamehe watuhimiwa vinginevyo wewe ndiye unaye"twist" maneno yako kupotosha.
 
Ni kweli kasamehewa maana Lisu, Zito na viongozi wa Dini wote walimwomba Rais amsamehe mbowe.

Bila kusamehewa angakula mvua ya kutosha.

Awashukuru viongozi wa dini.
Inawezekana Zitto aliomba Mbowe asamehewe, hata kama ni kuomba kwa unafiki; lakini najua Lissu hawezi kuomba Mbowe asamehewe kwa kosa ambalo halikuwepo.

Viongozi wa dini hawakuomba Mbowe asamehewe. 'Spin' za namna hiyo zielekeze kwa wajinga.
 
Back
Top Bottom