Hakuna anayepinga hilo, hata CCM wanaojielewa walikuwa upande wa haki kwenye issue ya Mbowe ndio maana pressure ikazidi kwa mamlaka.
Laiti kama moto ule wangeuelekeza kwenye Katiba Mpya leo tungekuwa na Tanzania mpya kabisa isiyo na matabaka ya aina yoyote huku wote tukiwa kitu kimoja kwenye taifa moja.
Sasa asubiriwe Mbowe na viongozi wa chama chake waje kuongea na waandishi wa habari na watz kwa ujumla kama alivyosema juzi, yeye ndie atatoa "a way forward" juu ya nini kinafuata kwenye harakati za kudai haki.
Sio kuokoteza maneno ya mitaani Mbowe amejisalimisha kwa watawala, wengine eti CCM wanajua michezo ya siasa, wangeijua hiyo michezo wasingeiba kura kila uchaguzi mkuu unapofika, wamezeeka hakuna wanachojua.