Pre GE2025 Freeman Mbowe: Nitatoa uamuzi wa kugombea Uenyekiti siku ya Jumamosi saa 5 asubuhi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mitanzani ni mijitu minafiki Sana ivi imagine baba wa Taifa angelazimisha kukaa madarakani mwaka 1985 halafu aje labda atolewe kwa nguvu na jeshi angekuwa na heshima yeyote katika nchi hii?

Lazima tujifunze kuwajibika kwenye Jambo lolote hakuna mtu special kwenye taasisi anayeweza kukaa miaka 20 taasisi inaanguka halafu bado anataka kukaa tu pale huu ni ujinga.

Hili sio hata swala la kujiuliza kwa masaa 48 ni swala la kusema tu kwamba Mimi sigombei over!

Mbowe mbowe mbowe nimekuita Mara tatu Kama utabishana ukweli utakuwa na mwisho mbaya Sana kwa laana za Watanzania wapenda mabadiliko!!

Watu account zetu zilishafungwa kwa sababu ya hiki chama

Tenda zetu tulishazuiwa kulipwa kwa sababu ya hiki chama

Watu wameteswa wengine hawana hatia Kama wakina Akwilina maisha yao yamekatishwa Leo hii chama hiki kiishie hewani tu aisee!!

Think twice leave!!
 
Chairman haya maigizo ni ya kizamani inamana huko cdm hakuna akili mpya.
 
Maigizo ya kizamani kinoma! Mambo ya hovyo kwelikweli.
Ndio maana upinzani hauaminiki.
Kabla yake kulikuwa na wengine, na hawakung'ang'ania.
Ukiona mtu ana 'back up' ya CCM wote, mjue huyo ni 'mjasiriamali' kupitia siasa.
 
18 December 2024

Wafuasi wa CHADEMA Wakifunguka Mbele ya Freeman Mbowe, "Mission Bado Haijakamilika"


View: https://m.youtube.com/watch?v=pYLhxzLmB2cViongozi mbalimbali wa CHADEMA pamoja na wafuasi wao wakizungumza nyumbani kwa Freeman Mbowe, Mikocheni Jijini Dar es Salaam wakimtaka Mwenyekiti huyo wa CHADEMA aliyekaa madarakani kwa miaka 21 achukue fomu ya kugombea tena.
 
Sasa laana za watanzania kafanyaje? mbona watekaji wanaendelea ijapokuwa wanalaaniwa kila siku au laana zinaangalia ntu na ntu? muache achukue fomu ili wachuane kwenye box la kura hiyo ndio demokrasia, kwani amekiuka katiba mahali?
 
Aseme tu kwamba anagombea,kigugumizi cha nini?
Ni dhahiri Mbowe hawezi kukiacha hiko cheo hadi pale atakapoona hakina maslahi tena kwake.
 
18 December 2024
Mikocheni, Dar es Salaam

Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Iringa atoa ujumbe mzito


View: https://m.youtube.com/watch?v=KWrIrTnVOoEWilliam Mungai ambaye ni mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Iringa ameongea mazito leo wakati akitoa hotuba ya kumshawishi Freeman Aikaeli Mbowe kugombea tena uongozi wa CHADEMA kwa Awamu ya Tano kwa sababu wanaamini wao wana hoja za msingi.

Katika mkutano huu hoja mbalimbali zimezungumzwa ikiwemo utulivu na usikivu, pamoja na namna alivyopitia misukosikuo na wanachama hawa wanaamini mbowe bado ana nguvu za kuiongoza CHADEMA.

Hata hivyo wachama hao wamesema Mbowe ni jenerali mzuri wa Vita na kusisitiza kuwa hakuna shinikizo lolote la kumshawishi Mbowe kugombea zaidi ya wao kuona bada anafaa kuwaongoza.
 
Dalili za haraka haraka zinaonyesha anagombea huyu!
 
Mbowe agombewi kuepusha lawama anarudisha chama ukweni mtoto wa mtei ndio mrith wake
 
Meena alifoka bei.
Lipumba akafika bei.
Mbowe anaonekana dhahiri, ila muda utathibitisha au kukanusha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…