OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Nilifungiwa akaunti zote za bank za kampuni yangu. Nikafungiwa akaunti zote za biashara. Hata akaunti yangu binafsi ya mshahara wa ubunge ilifungwa toka mwaka 2018, nikazuiwa kupokea mshahara ambao ni haki yangu kisheria" Mhe.Freeman Mbowe akizungumza na wanahabari.
My Take:
Natengua msamaha nilioutoa kwa Magufuli
====
MBOWE: NILITUMIWA MADAI YA KUDAIWA KODI NIKIWA JELA
Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema alitumiwa madai ya kudaiwa kodi ya Tsh. Bilioni 2, kwenye email binafsi akiwa jela ambapo alishindwa kuiona.
Barua pepe ya kwanza ilimtaka kupeleka malalamiko ndani ya siku 30 kama hakubaliani nayo, kwa kuwa alikuwa jela hakuweza kuijibu, wakatuma nyingine kusema kuwa kwa kuwa amekaa kimya ameonekana kukubaliana nayo.
Alivyotoka jela, akadaiwa kodi ambayo amedai kuwa haikuwa sawa kwa kuwa ili biashara ilipe kodi ya Tsh. Bilioni 2 lazima iwe imetengeneza faida ya Tsh. Bilioni 12 kwa mwaka, na biashara yake ni ndogo isingeweza kutengeneza faida hiyo.
Ili Mamlaka ya mapato kuipata kodi hiyo walifungia akaunti zake zote ikiwemo aliyokuwa anapokelea mshahara wa ubunge. Kwa sababu hiyo aliondoka nchini ili kutafuta fursa za kuwekeza nchi nyingine.