Freeman Mbowe: TRA walinidai Kodi Bilioni 2, Wakafunga akaunti zangu zote za biashara mpaka binafsi, Wakachukua hela

Freeman Mbowe: TRA walinidai Kodi Bilioni 2, Wakafunga akaunti zangu zote za biashara mpaka binafsi, Wakachukua hela

2018 Mbowe alipelekwa gerezani kwa kosa gani? na alikaa kwa muda gani?

Kama alipewa siku 30 za kufanya appal na anadai alikuwa jela kwanini asingeenda mahakamani kudai akupata fursa ya kujibu kwa sababu alikuwa jela na TRA awakusaliana na mtu msimamizi mwingine yeyote wa biashara zake.

TRA walikadiria vipi kodi bila ya kukutana na mwakilishi wa biashara zake, ata mmoja?

Hela ya kujikimu huko nje ya nchi na kutafuta fursa nyingine alizitoa wapi, kama account zake mpaka binafsi zilifungiwa.

Kama ana account nje ya nchi, biashara na assets zingine je zimeorodheshwa kwenye form ya maadili serikalini na bungeni au hizo hela za kufanyia hayo mambo kazitoa wapi?

Ni uongo mtupu, tatizo lenyewe Mhede hayupo TRA kujibu hizi tuhuma, wametengeneza mazingira ya kumchafua Magufuli kila sehemu bila ya watu sahihi kuweza kujibu.

Hata Dotto angefukuzwa kabisa serikalini sasa hivi kungekuwa na uongo wa wizara ya fedha.

The whole story is pathetic ya kudanganya watu wajinga tu.
 
Account zimefungwa, ulitegemea akae tu amsubiri JPM?
Kweli wewe ni mnyonge. Ukidondosha hela, unalala njaa, kuzisubiri mpaka uzipate hizo hela ndiyo ukale?
Wamefunga account na siyo hela. Unaweza kufungua account lenye jina la mwanao na ukafanya miamala km kawaida.
Mkuu uko serious?
 
Hayo mengine, utajibiwa tu hapa, lakini la Doto, usijifanye mtabiri, yajayo yana julikana! Kichere alishapewa kazi ya kuleta hesabu za January - March! Kama Wewe ni Bashiru au Doto, stay tuned!
 
Nenda kwa yule anaefufua watu pia ana kanisa ni ash khouf na Mbupe hihihi mwambie afufue yule boss wako unaonekana hutaki kuamini ukweli..poole saana kima wewe..
 
Jamaa yangu wa TRA aliniuma sikio, nikatoa zote na kuhifadhi shambani. Huko bank ilibaki hela ya kuzuia tu, biashara nikafunga nikabaki nalima tu.

Mkuu acha uongo bhana[emoji23][emoji23]. Kuna mbinu nyingi sana za kulipa kodi ya serikali nenda kasome TAX ADMINISTRATION ACT, 2015. Huwezi kimbia kama ukikutwa na TRA sheria inawaruhusu kushikilia hadi assets mzee. Hii iliwakuta wafanyabiashara wakubwa lakin kama ulikua unasikiliza wito wao, mkayajenga hawakufungii account. Sisi nakumbuka tulifsnyiwa audit tukabargain yakaisha.
 
Hayo mengine, utajibiwa tu hapa, lakini la Doto, usijifanye mtabiri, yajayo yana julikana! Kichere alishapewa kazi ya kuleta hesabu za January - March! Kama Wewe ni Bashiru au Doto, stay tuned!
Ni vilaza kama nyie ndio mnaoweza amini huo upuuzi wa Mbowe? Mahakama zilikuwa zimefungwa alipotoka jela kwa hivyo akuweza kwenda kujitetea.

Leo Mbowe hana biashara hata moja Tanzania? Na kama zipo zime-survive vipi muda wote huo wakati kwa madai yake account zilikuwa zimefungwa mpaka majuzi.

Kiazi ni kiazi tu atakiongopa story yake lazima itakuwa na gaps ambazo ajafikiria.

Ni story ya kuchota wapuuzi tu sio watu wenye akili zao timamu.
 
Nenda kwa yule anaefufua watu pia ana kanisa ni ash khouf na Mbupe hihihi mwambie afufue yule boss wako unaonekana hutaki kuamini ukweli..poole saana kima wewe..
Tatizo ni huu uongo, Mbowe leo hana biashara ata moja Tanzania? Hizo ni story ni kwa wapuuzi kama nyie nyumbu mnaoamini kila ujinga unaotoka mdomoni kwa viongozi wa CDM.
 
Mbowe ni muongo.

Mbowe anasema alifungiwa akaunti zote lakini akaamua kwenda kufanya Biashara Dubai, hizo hela za kwenda kuanzisha biashara Dubai zilikua akaunti gani kama akaunti zake zote TRA walifungia?
Jogoo hafi kwa utitiri Mkuu.
 
Mbowe ni muongo.

Mbowe anasema alifungiwa akaunti zote lakini akaamua kwenda kufanya Biashara Dubai, hizo hela za kwenda kuanzisha biashara Dubai zilikua akaunti gani kama akaunti zake zote TRA walifungia?
Mtu mwenye hadhi kama Mbowe,hawezi kukosa wafadhili,usijiringanishe nae,ukitaka kuelewa waza kama tajiri,ana mke,ana watoto,wenye vipato,marafiki,asingeshindwa kupata fedha ya kuanzia.
 
MJGSLH.jpg



Katika hotuba yake Mhe.Freeman Mbowe ameelezea suala la kufungiwa akaunti zake za benki. Mhe.Rais Samiah alipokua akiapisha mawaziri alilizungumzia pia, na kutaka wafanyabiashara waliofungiwa akaunti zao zifunguliwe.

Kufungia/kufreeze akaunti maana yake unaona hela kwenye akaunti yako lakini huwezi kuzitoa. Kwa nchi zilizoendelea akaunti inaweza kufungiwa kama mhusika anajihusisha na biashara ya madawa ya kulevya, utakatishaji pesa, ugaidi etc, ili kupisha uchunguzi. Lakini huwezi kufungia akaunti ya mtu kwa sababu za kisiasa.

Ni unyama.Lakini wakati wa mwendazake tulishuhudia wafanyabiashara, wanasiasa, wanaharakati, wanamichezo etc wakifungiwa akaunti zao. Halijawahi kuwa jambo la kawaida kwenye tawala zilizopita zaidi ya utawala wa mwendazake.


Kuna wanasiasa walifungiwa akaunti bila sababu yoyote ya msingi, walipoulizwa wakaambiwa ni amri kutoka juu. Vivyo hivyo kwa wafanyabiashara na wanaharakati. Kuna wafanyabiashara walifungiwa akaunti zao kwa kuonekana tu karibu na viongozi wa upinzani.

Wafanyabiashara wengi walifilisika. NGO nyingi zikafa. Mzunguko wa pesa mtaani ukapungua. Halafu bila aibu mwendazake akawa anashangaa kwanini pesa zimepungua mtaani?

Athari za kufunga akaunti sio tu inapunguza pesa kwenye mzunguko, bali inachochea "black market" kwenye biashara ya pesa. Mfanyabishara akiwa na hela zake anaogopa kupeleka bank kwa kuhofia akaunti zake zinaweza kufungwa, anaamua azitunze ndani.


Shinyanga kuna mfanyabishara alifariki zikapatikana malioni 400 amehifadhi kwenye ndoo. Unadhani mtu kama huyo hakujua umuhimu wa kuhifadhi pesa bank? Ni kwa sababu ya "ujinga" wa kufungia akaunti ndio maana watu wanaamua bora wabaki na pesa zao ndani. Jambo hili ni baya katika uchumi wa nchi.

Mbowe alifungiwa akaunti zake zote za biashara. Akafungiwa na akaunti ya mshahara. Tangu mwaka 2018 amelipwa mshahara lakini hawezi kuutoa kwenye akaunti. Mwaka jana alilipwa kiinua mgongo cha ubunge lakini hakuweza kukitoa. Anaona tu "digits" kwenye akaunti lakini hawezi kutoa. Waswahili husema kula kwa macho.

Mwaka huu ndio akaunti zake zimeachiwa baaada ya mwendazake kuitwa akhera madukani. Kwa mara ya kwanza baada ya miaka mitatu, Mbowe ameweza "kuaccess" account zake baada ya Mama kushika madaraka. Kwahili tumpongeze sana mama kwa moyo wake wa utu.Tumshangae mwendazake kwa unyama huu. Unamnyima mtu mshahara miaka mitatu, bado unafunga akaunti zake za biashara unataka aishije? Yeye angefanyiwa hivyo angejisikiaje? Halafu alijiita mpenzi wa Mungu. Ni Mungu gani huyo?

Mbowe sio mwanasiasa wa kwanza kulalamikia suala hili, wapo wengine japo wamelalamika kimya kimya. Waziri mkuu mmoja mstaafu amewahi kulalamika kufungiwa akaunti zake zote, hadi alipoamua kuunga juhudi ndipo zikafunguliwa.Tulijengwa katika misingi ya matabaka na unyanyasaji kwa sababu tu ya itikadi zetu za kisiasa. Lakini aliyetuingiza kwenye ubaguzi huo alijifanya ni kiongozi wa wote na kutusisitiza tusibaguane kisiasa. Maneno na matendo yake yalitofautiana.

Hili liwe fundisho kwa wafuasi na viongozi wa vyama vya upinzani. Njia ya upinzani haijawahi kuwa rahisi. Kuna watu wamefukuzwa kazi, wamefilisiwa biashara, wamepata ulemavu kwa sababu tu ya kuwa wapinzani. Lakini hawatetereki, hawakati tamaa, hawavunjiki moyo.

Mbowe alivunjiwa Billicanas, akaharibiwa shamba lake na kupoteza zaidi ya Bilioni 1.3, akavamiwa hotelini kwake na DC ambapo wafanyakazi wake walipigwa na mali za hoteli kuharibiwa, akafungiwa akaunti zake za biashara, kama haitoshi akafungiwa akaunti yake ya mshahara. Lakini pamoja na yote hayo hajawahi kutetereka wala kukata tamaa. Mara zote amekua imara zaidi kuliko awali.

Sio kama akina "mzee Halima" wamekosa mshahara wa mwezi mmoja tu, njaa zikawapanda kichwani. Wakasahau udhalimu wote waliofanyiwa na kuamua kuunga mkono juhudi. Hivi wangepitishwa kwenye tanuru la moto kama Mbowe ingekuaje? Shame.!

By Malisa Godlisten
 
Mbowe ni muongo.

Mbowe anasema alifungiwa akaunti zote lakini akaamua kwenda kufanya Biashara Dubai, hizo hela za kwenda kuanzisha biashara Dubai zilikua akaunti gani kama akaunti zake zote TRA walifungia?
Mbowe mwongo ila wewe mjinga usiyewaza. Uko low hadi aibu. Mbowe si level yako ndugu. Jiongeze kujua km alifungiwa akaunt pesa katoa wapi za kwenda kuwekeza nje ya nchi.

Naona umepata likes nyingi tu za wajinga wenzio.
 
Kama hakufata sheria..alitaka iweje!!! Kama alifata aende mahakamani..

Ila nawashangaa wengi.. maneno mengi kama vile uongozi wote umebadilika ukaja mpya kutoka sijui safari ipi.. na sheria za nchi zimekutwa..

Waendelee tu kuongea...........
Mbumbumbu mzungu wa reli ktk ubora. Kichwa empty kabsa. Yaani hapo umewaza umemaliza [emoji1787][emoji1787]
 
Kukumbushia tu Mbowe alikuwa ni mdaiwa sugu ata NHC ndio kilichopelekea kunyang’anywa jengo alikokodi Billcanas na ofisi za Magazeti yake; aitokuwa jambo la kushangaza kama alikuwa na malimbikizo TRA yanayofikia billioni mbili.
 
Aisee kumbe tunayoambiwa na Mh. Rais wetu Samia Suluhu Hassan ni kweli? John Joseph Pombe Magufuli kwa hili sitakaa nikusamehe au kukusemea jema milele. Ulipwe unayostahili huko uliko motoni. Ulitesa mno Watanzania kwa visasi binafsi na kisiasa.

Mungu akulinde Rais wetu ambaye Nawe ulikuwa unajeruhika na MATENDO ya yule Bwana. Mungu alisikia vilio vya walioteswa. Kumbe Mbowe aliteswa hivi? Na alikaa kimya. Sasa anawekeza nje ya nchi na kodi analipa huko huko.
My take: unamtesa Mbowe ambaye kwao alizaliwa akaiikuta pesa na vitega uchumi mpaka nje ya nchi. Ni wivu huo. Eti tuishi kama mashetani. Laiti angalijua Mungu ni kiboko ya wote hata wake wanaojifanya Mungu watu kwa Mungu ni nukta.
 
Mbowe ana biashara gani kwani mbona haitaji. TRA mje na majibu ya huyu kilaza
 
Back
Top Bottom