Pre GE2025 Freeman Mbowe: Viongozi wa CHADEMA na Watanzania wasio na Vyama wanaoendelea kutekwa na Vyombo vya Usalama vya Nchi yetu

Pre GE2025 Freeman Mbowe: Viongozi wa CHADEMA na Watanzania wasio na Vyama wanaoendelea kutekwa na Vyombo vya Usalama vya Nchi yetu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Black Butterfly

Senior Member
Joined
Aug 31, 2022
Posts
130
Reaction score
368

Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe.​

Leo nitazungumza mambo mawili mahususi ambayo sisi kama Chama tunaamini yanagusa Watanzania na yanazua taharuki na hofu, nitazungumza kuhusu sakata la wimbi kubwa la Viongozi wa CHADEMA, Watanzania wengine wasio na Vyama wanaoendelea kutekwa na Vyombo vya Usalama vya Nchi yetu na Vyomvo hivyo vikaendelea kukaa kimya, kuwateka Watu katika taratibu ambazo sio za kisheria, kutowafikisha Vyombo vya Kimahakama kwa utaratibu wa kisheria na wengine kuuawa”

“Tumeamua tupaze sauti kuwataka wenye Mamlaka Nchini kutambua kwamba thamani ya maisha ya kila Mtanzania mwenzetu ni kubwa kuliko chochote, kwahiyo sisi kama Jamii ya Tanzania ni wajibu wetu kusimama kuhakikisha haki kwa Watu wote inapatikana na tusiendelee kuruhusu baadhi Vyombo vya Dola viendelee kuwaua , kuwatesa na kuwapoteza Watanzania na sisi tukakaa kimya, lazima tuseme na tunasema kwa kujiamini na tunasema tukijiua kwamba athari zake ni nini hata kwa maisha yetu binafsi lakini lazima tuseme ili hatimaye ukatili huu usionekane kama ni mzaha au ngonjera”

“Siku za hivi karibuni Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kilitoka na tamko kuhusu kuongezeka kwa utekaji nyara, TLS walitoka na orodha kubwa ya Watu zaidi ya 80 kwa majina na maeneo waliyotoka, taarifa ya TLS imetoka August 09 mwaka huu ikionesha majina ya Watu waliotekwa na walipotekewa na wengine waliokutwa wamekufa katika vyumba vya kuhifadhi maiti, inapotoka taarifa hii halafu Vyombo vya Dola vikakaa kimya ili ni jambo ambalo limetulazimisha sisi kuungana na TLS kupasa sauti

Soma Pia:

  • Freeman Mbowe: Dar es Salaam kuna kikosi kazi cha utekaji
  • TLS, yatoa orodha ya watu waliopotea na kutekwa na tamko juu ya ongezeko la vitendo vya utekaji na upoteaji wa watu nchini

  • “Kama Chama tumechunguza kutoka vyanzo vyetu vya ndani na vingine vya ndani ya Jeshi la Polisi na Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama, nitaeleza kwa kifupi tulichogundua na tunaowaonyooshea vidole ili Polisi na hao wengine watusute watuambie Mbowe mnasema uongo, uchunguzi wetu unatupeleka wapi? moja kuna kitu kwenye Kanda Maalum ya Dar es saalam kinaitwa Task Force ya Ulinzi na Usalama, Task Force hii iliundwa ikishirikisha Wadau kutoka Jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa na hata JWTZ, katika hatua ya baadaye Jeshi la Wananchi liliondoka katika oparesheni hii, na Task Force hii ilipoundwa kwa mara ya kwanza iliundwa kama Kikosi maalum cha kupambana na wizi ambacho kinasimamiwa na ZCO ambaye sasa hivi anayeongoza Ofisi hiyo anaitwa ASP Faustin Mafwele huyu ndio Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda Maalum ya Dar es salaam ambaye anasimamia Kikosi hiki”

 
Chama kikubwa kinatoa tamko

TOKA MAKTABA:

19 Agosti 2024

Temeke Dar es Salaam , Tanzania

KUTOWEKA VIONGOZI WA CHADEMA MKOA WA WILAYA DSM KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA CHADEMA WATOA TAMKO


View: https://m.youtube.com/watch?v=nfBNEaVqMBE

Benito Mwapinga mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Temeke akiongoa na waandishi wa habari kisha kubainisha viongozi Deusdedith Soka na wenzake walipigiwa simu tarehe 18 Agosti 2024 kutoka kituo cha polisi Changombe kuwa ....




Maoni ya wananchi :
N.B :

Jeshi la polisi linatakiwa kufumuliwa hasa ngazi ya SACP kwenda vyeo vya CP wastaafishwe wote.

Hii itasaidia kurejesha usimamizi wa nidhamu na utendaji wa walio chini yao kuzingatia kanuni na GPO ya polisi wanapotumwa askari kwenda kukamata watuhumiwa.
 
Huko Chadema anazungumza yeye na lisu tu.

Wengine wanaongea.
 
Nukuu toka kwa vyama vidogo vya siasa nchini Tanzania

TOKA MAKTABA :
Mzee John Cheyo - "Hili la vyama vinavyojiita Chama Tawala na Chama Kikubwa kuteka agenda za nchi halikubaliki"
 
Chadema wekeni basi hotuba baada ya kutumia MB zetu kusikiliza vitu ambavyo vya kila siku?
 
Makombora mazito yanapitishwa hapa Lumumba leo mnakazi ikibidi usiku Mtangaze TENGUWA nyingine.....
 
Back
Top Bottom