Pre GE2025 Freeman Mbowe: Viongozi wa CHADEMA na Watanzania wasio na Vyama wanaoendelea kutekwa na Vyombo vya Usalama vya Nchi yetu

Pre GE2025 Freeman Mbowe: Viongozi wa CHADEMA na Watanzania wasio na Vyama wanaoendelea kutekwa na Vyombo vya Usalama vya Nchi yetu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe.​

Leo nitazungumza mambo mawili mahususi ambayo sisi kama Chama tunaamini yanagusa Watanzania na yanazua taharuki na hofu, nitazungumza kuhusu sakata la wimbi kubwa la Viongozi wa CHADEMA, Watanzania wengine wasio na Vyama wanaoendelea kutekwa na Vyombo vya Usalama vya Nchi yetu na Vyomvo hivyo vikaendelea kukaa kimya, kuwateka Watu katika taratibu ambazo sio za kisheria, kutowafikisha Vyombo vya Kimahakama kwa utaratibu wa kisheria na wengine kuuawa”

“Tumeamua tupaze sauti kuwataka wenye Mamlaka Nchini kutambua kwamba thamani ya maisha ya kila Mtanzania mwenzetu ni kubwa kuliko chochote, kwahiyo sisi kama Jamii ya Tanzania ni wajibu wetu kusimama kuhakikisha haki kwa Watu wote inapatikana na tusiendelee kuruhusu baadhi Vyombo vya Dola viendelee kuwaua , kuwatesa na kuwapoteza Watanzania na sisi tukakaa kimya, lazima tuseme na tunasema kwa kujiamini na tunasema tukijiua kwamba athari zake ni nini hata kwa maisha yetu binafsi lakini lazima tuseme ili hatimaye ukatili huu usionekane kama ni mzaha au ngonjera”

“Siku za hivi karibuni Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kilitoka na tamko kuhusu kuongezeka kwa utekaji nyara, TLS walitoka na orodha kubwa ya Watu zaidi ya 80 kwa majina na maeneo waliyotoka, taarifa ya TLS imetoka August 09 mwaka huu ikionesha majina ya Watu waliotekwa na walipotekewa na wengine waliokutwa wamekufa katika vyumba vya kuhifadhi maiti, inapotoka taarifa hii halafu Vyombo vya Dola vikakaa kimya ili ni jambo ambalo limetulazimisha sisi kuungana na TLS kupasa sauti

Soma Pia:

“Kama Chama tumechunguza kutoka vyanzo vyetu vya ndani na vingine vya ndani ya Jeshi la Polisi na Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama, nitaeleza kwa kifupi tulichogundua na tunaowaonyooshea vidole ili Polisi na hao wengine watusute watuambie Mbowe mnasema uongo, uchunguzi wetu unatupeleka wapi? moja kuna kitu kwenye Kanda Maalum ya Dar es saalam kinaitwa Task Force ya Ulinzi na Usalama, Task Force hii iliundwa ikishirikisha Wadau kutoka Jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa na hata JWTZ, katika hatua ya baadaye Jeshi la Wananchi liliondoka katika oparesheni hii, na Task Force hii ilipoundwa kwa mara ya kwanza iliundwa kama Kikosi maalum cha kupambana na wizi ambacho kinasimamiwa na ZCO ambaye sasa hivi anayeongoza Ofisi hiyo anaitwa ASP Faustin Mafwele huyu ndio Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda Maalum ya Dar es salaam ambaye anasimamia Kikosi hiki”

 

View: https://www.youtube.com/live/JGCNth0mHCo
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe anatoa tamko la chama hiko juu ya masuala mbalimbali yanayoendelea nchini Tanzania.

Mhe. Mbowe huyu Bi. Kizimkazi unayemtaka afanya hivyo vitu asipofanya mna mkakati gani wa kufanya nje ya maagizo ilihali mkitambua kuwa huyu Bi anathani yeye ndio kila kitu nchini? Badilikeni muwe kama akina Odinga J. Odinga wa Kenya; huyu hawezi kuitisha maandamano Serikali ika relax kama ninyi msivyo na meno kwa sasa!
 
Nilitegemea mruhusu maswali ili wenye akili wamuulize Mbowe hizi sanaa ataacha lini? Hii siyo CDM ya akina Dr. Slaa ambayo ilikuwa serious na ishu. Swali la msingi Serikali isipotekeleza mtafanyaje?
 
Je John Mnyika status yake ikoje kwenye chama?
 
Naamini Amiri Jeshi Mkuu na Mfariji Mkuu amesikia na atachunguza ukweli wake ili kufanyia kazi. Mama anaupiga mwingi na atathihirisha kwa vitendo.
 
Nilitegemea mruhusu maswali ili wenye akili wamuulize Mbowe hizi sanaa ataacha lini? Hii siyo CDM ya akina Dr. Slaa ambayo ilikuwa serious na ishu. Swali la msingi Serikali isipotekeleza mtafanyaje?
Ulishawahi kumuuliza swali Mkiti wa CCM Samia hata moja
 
Mimi Sina chama,ila hii speech imenifanya nimetokwa na machozi😭
 
Back
Top Bottom